Pekua/search

Monday, July 2, 2012

Serikali haina Uwezo wa kuwalipa madaktari 3.5M- inaweza kuwalipa kiasi gani?


Serikali haina Uwezo wa kuwalipa madaktari 3.5M- inaweza kuwalipa kiasi gani? 
Imepledge kiasi gani? 
Mbona haisemi?Tuko baadhi yetu tunaoamini na tunaendelea kuamini kuwa kinachofanya wananchi tuendelee kuteseka kwa kukosa huduma bora za afya ni SERIKALI YENYEWE. Ni jeuri ya serikali yetu hii ya KUGOMA kupata suluhu na madaktari.

Serikali kupitia mtumishi wake mkuu yaani mhe Rais imesema bayana kuwa haiwezi kuwalipa madaktari wanaoanza kazi sh Milioni 3.5. Lakini cha kusikitisha haijasema ili pledge kiasi gani ambacho madaktari walikataa. Mbona rais wetu hakusema hilo? Natufanya tuendelee kuamini kuwa anaendeleza na kuendekeza propaganda, ambazo kwa namna yoyote hazitamsaidia wala kutusaidia wapigakura wake. 

Picha iliyoambatanisha inasema maneno mengi. Hebu na tujaribu kulinganisha kasi ya uboreshaji wa huduma kwa watumishi hawa; MADAKTARI (watalaam ambao kusomea hadi umeitwa daktari si chini ya miaka mitano baada ya kidato cha sita) na WABUNGE (ambao miongoni mwao wako hata wa bla bla tu darasa la saba la nne na wengine PhDs walizopata wakiwa chekechea sijui) ). Kama miaka ya 80 wabunge waliweza kwenda Dodoma kwa usafiri wa pamoja, leo hii kila mmoja anamgari wake, mtasema anakopeshwa (kwanini madaktari wasikopeshwe pia).

Hoja muhimu hapa ni kwamba serikali inatumia nguvu nyingi sana kwenye utawala. Wabunge ni wengi sana, Baraza la mawaziri bado ni kubwa mno na mikoa na wilaya zinazidi kuongezwa, kwa tija ipi?
Wananchi wanahitaji huduma;hospitali zaidi, wataalamu wanaolipwa vizuri zaidi, shule zaidi, masoko ya uhakika zaidi, pembejeo zaidi na sio kuongeza majengo ya ofisi ya mkuu wa mkoa wilaya nk nk. Na kama lipo hitaji la lazima kiutawala basi serikali iongeze HALMASHAURI ZA WILAYA (Miji, manispaa na jiji). Maana hizi ndiyo zinapaswa kuwa TAWALA ZA WANANCHI. SERIKALI ZA WANANCHI.

Picha hii imezungushwa sana kwenye mitandao (Pongezi kwa aliyeileta).

3 comments:

Asifiwe July 3, 2012 at 11:47 PM  

Serikali haiwezi ika-pledge chochote zaidi ya kutuchonganisha na Madaktari, ili tuwaone ndio wabaya,,ndio hawawajari watu,tuendelee kuamini kuwa serikali inatujari sana. Sihoji zaidi kwa kuwa mara zote tumesikia upande mmoja tu ukisema na kujisafisha,mbona hawajawaita kwenye media wakasema na wao, yaani uwe kama mdaharo,,wawachongee tukiwaona.
Nasikitika maana umesemwa mshahara huku kukiwa na madai mengi,,mbona hayajasemwa?
Hakuna marefu yasiyokuwa na ncha

MUNGU TUREHEMU

Adam July 3, 2012 at 11:57 PM  

Naam Mungu aturehemu. Maana ukisia wadanganyika tunavyomeza chambo, ndoana na mshipi hadi ujiti wa wavuvi hawa serikali, utasikitika utamani kujikana nafsi yako. Unasemwa mshahara sa if ni dhambi kupata mshahara mkubwa. Ni aidbu, ni dharau ya hali ya juu. Ila KITAELEWEKA MAPEMA KULIKO TUNAVYODHANI.

Adam July 3, 2012 at 11:57 PM  
This comment has been removed by the author.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP