Pekua/search

Friday, October 11, 2013

JAMII KUSHIRIKIANA KATIKA KUWALEA WATOTO YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU ILI KUANDAA KIZAZI BORA CHA BAADAE.

 Bwana na Bibi Gilbert Kabati(waliokaa) walezi wa watoto yatima wa The maasai Foundation center(waliosimama nyuma yao) na Bibi Bernadette Bachubila, mmoja wa viongozi wa kikundi cha kina mama cha Tumaini, akihamasisha na kuikumbusha jamii juu ya umuhimu wa kuwalea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu ili kuwa na taifa bora na lenye nguvu.

Kikundi  cha Tumaini, kilichopo njiro jijini Arusha, kutokana na urafiki wa muda mrefu na  watoto wa the Maasai Foundation center waliandaa hafla kwa ajili ya kuwa karibisha watoto hao jijini hapo ili kuweza kufurahi pamoja nao. Hafla hiyo, ilifanyika mwanzoni mwa wiki hii katika ukumbi wa Olasity Garden. 

Mbali na michezo mbalimbali iliyofanyika, watoto hao pia waliweza kuzawadia zawadi mbalimbali kama vile mipira, T-shirts, Mabeg ya shule, sweta za shule, vyakula pamoja na pesa zilizopatikana kutokana na mnada uliofanyika. 


 Watoto wa the Maasai foundation wakiwa  na baadhi ya  zawadi zao walizozawadiwa katika hafla hiyo na pia, hapo chini kina mama wa kikundi cha Tumaini wanaonekana wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali tayari kuwazawadia watoto hao wa the Maasai Foundation Center.
 Familia ya Bwana na Bibi kabati, wamejitolea kuwalea zaidi ya watoto yatima 20, wenye umri kati ya miaka 5 na 15, katika nyumba yao na hivyo, kufanya familia hiyo kuwa na watu takribani 49. Jambo la kufariji zaidi ni kuwa, licha ya ukubwa wa familia hiyo, baraka zimekuwa zikionekana kila kukicha, kwani wamekuwa wakipata milo yote mitatu, huduma ya elimu, afya na mahitaji mengine muhimu ya kifamilia. 

kwa maelezo ya walezi hao, watoto hao wanavipaji kama vile uinjilishaji kupitia uimbaji, na uigizaji. Pia, walipatiwa ujuzi wa kufuga na kulima na kwa sasa wanafanya shughuli hizo kwa ajili ya maisha yao ya baadae, zaidi, ili waweze kujitegemea wenyewe mara watakapotoka kituoni. 

Watoto hawa wana njozi kubwa kwa maisha yao ya baadae, njozi ambazo hawataweza zifikia ikiwa hawatapata ushirikiano wa karibu sana wa kimalezi na kujengewa msingi bora ya maisha yao. Katikati ya watoto hao(kama wanavyoonekana hapo chini) wapo wanaotaka kuwa madaktari, waalimu, wapishi, wakandarasi na hata kushika nafasi ya kuongoza nchi(Rais).
Watoto ndio taifa la kesho, ndio viongozi wa kesho. Kama tukiwatunza vizuri tutakuwa na kizazi angavu. Jamii haina budi kuchukua jukumu la kushirikiana katika kuwalea watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu kwani wanahitaji malezi na mapenzi ya wazazi bila kusahau malezi ya kiroho.
Tukishirikiana kwa pamoja tunaweza kuondoa watoto wa mitaani pamoja na watoto waishio katika mazingira magumu na kuhakikisha kuwa tunakuwa na kizazi angavu na chenye nguvu katika kuliendeleza taifa letu.

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP