Pekua/search

Thursday, June 12, 2014

PAYE: Huyu Mdudu Simpendiiiiiiiiii.Huyu Mdudu PAYE Simpendiiiiiiiiii.    • Sijui leo wanatasemaje   huko Dodoma!!
  • ·Tunahitaji Mfumo wa Haki wa Kodi nchiniiiiiiiiiiiiiiiiiii


Fuatilia Mjadala huu wa Facebook katika siku hii ya Kusomwa kwa Bajeti Kuu ya serikali.

Atukuzwe Asifiwe kinachoudhi sana kuna mwingine anafukua mchanga wetu kwa miaka minne na nusu,,anabadili jina eti GRACE PERIOD,,mwingine anatulaza pale kwenye kona ya Posta mjini kwa miaka ishirini amekuwa na majina matano,,mara Shela,,mara Moven,,mara ili mradi tu grace asimtoke,,si fair

Bupe Berrums yani huyu kwa kweli anauma vibaya sanaa

Florian Msuya mkuu uliebandika hii post nadhan hunifikii mimi kwa kumchukia huyo mdudu nikiangalia salaryslip yangu anavyonikwangua kila mwezi natamani kulia mbaya zaidi haepukk bado ukienda dukani kuna vat utamkut

Agnes Njumbo Umenigusa

Adam Gwankaja ha ha haaaaa mmenichekesha sana ndugu zangu ila ni kicheko cha maumivu makali sana Atukuzwe Asifiwe Bupe Berrums Florian Msuya na Agnes Njumbo. Kinachonikasirisha sana mimi ni: 1. Kwamba sisi wakamuliwa tumetulia tuliiiiiii utadhani tumetwangwa ganzi. Na mara nyingi tuko mstari wa mbele kuwatetea na kuwakingia kifua wakamuaji. Katika makundi yasiyopaza sauti zao ni sisi. Tumekuwa makondooooo. 2. MATUMIZI ya hizo hela tunazokamuliwa- zinaziniwa na matokeo yake wanatuinbox nyuchi zao kwenye mitandao. zinanywewa na kujipanulia uwekezaji wao binafsi...hapo pia ---tumekuwa mstari wa mbele kuwasifia wezi hawa.

Florian Msuya hebu fikiria mwenye duka analipa kodi kwa mwaka less than 100,000/= wewe na kamshahara kako unakatwa 70,000/=kila mwezi bado hutasamehewa kodi ya vat kwenye soda sukari kiberiti nk PAYE ur not fair!!

Atukuzwe Asifiwe Pengine twalia lia sana, pengine tuna namna ya ku-counter,,hawa watu wana mbinu nyingi sana, sasa wako busy kuwadanganya wadanganyika wengi huko vijijini maana ndiko mtaji wao uliko, kama walisema kwa watabibu wetu asiyetaka kazi aache,,kama waliwaambia walimu wetu wawalipe wanafunzi baada ya mgomo wao kukataliwa na Mahakama jumapili,, seuzi sisi jamani? tutasema na hatutaacha kusema maana maumivu haya makubwa sana. Kama wafanya kazi tungekuwa na sauti tungebadili mfumo huu maana pote palipobadilika ni wafanya kazi walipabadilisha

Adam Gwankaja Florian Msuya you are killing me man. Nimependa sana unavyoweka kwa urahisi sana haya masuala mazito. Haswaaaa, Tanzania hadi mimba hutozwa kodi! Wafanyabiashara wakubwa kimsingi hawalipi kodi hususan hiyo VAT maana ni wakusanyaji tu kutoka kwa already taxed lumpen wewe na mimi. kisha kwenye sherehe TRA wanatoa zawadi kwa wakusanyakodi ati ndio walipa kodi wazuri. ptuuuuuuuuuuuuuuuuu

Florian Msuya mbaya zaid paye ni non negotiable wanaikata huko huko halafu wakituonea huruma utasikia basi tunapunguza paye kwa 0.8% jamani jamani nchi hii

Adam Gwankaja Sauti tunayo Atukuzwe Asifiwe tunapaswa tu kuipaaza. Tunapaswa KUKASIRIKA na KUJAZBIKA!!! Sauti tunayo. Lazima tuwe nayo. Tuitazame siasa kama a necessity! Tuitazame machoni na tukubali kuwa inatuhusu.
 
Atukuzwe Asifiwe afu hao wakusanyaji walipogoma vikusanyio hatukuwasaidia

Adam Gwankaja ha hahaaaaa Atukuzwe Asifiwe sie mazumbukukuuuuu
 
Atukuzwe Asifiwe Yaani balaa,,kuna muda nachukia kuujua ukweli

Adam Gwankaja Ha haaaa ni kweli...tena hakika

Kuchangia mada hii bonyeza hapa

Picha kutoka http://www.meetup.com/9Networking/events/95198102/ 

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP