Pekua/search

Saturday, December 6, 2014

Ubakaji wa Maeneo ya wazi nchini- Kiwanja Ngoma- Mbeya


Ubakaji wa maeneo ya wazi mpaka lini?

Kisa mkasa cha Kiwanja Ngoma, Sokomatola jijini Mbeya.


Sijui iwapo ndio upangaji miji wa kisasa au nini? Sielewi huko duniani wenzetu miji yao imepangiliwaje!
Ninachojua ni kwamba kumekuwepo na juhudi kubwa hapa nchini, kwa halmashauri zetu (jiji,manispaa, mji ama wilaya) kuyabaka maeneo ya wazi pamoja na maeneo ya burudani hususan ya watoto, kila uchao. Pia ubakaji huu umesababisha utovu wa kipaumbele kwa maeneo haya katika mingi ya miji mipya inayoanzishwa.

Ni adimu sana miaka hii maeneo ya wazi katika miji mingi. Hata kwenye maeneo yaliyorithiwa kutoka kwa wakoloni yakiwa viwanja vya watoto ama burudani, yamekuwa yakibakwa na kubadilishwa matumizi ama kutelekezwa.

Nisiseme mengi, picha zifuatazo, nilizipiga nilipotembelea mjini Mbeya hivi karibuni ambapo nilipata wito nafsini kwenda kuona Kiwanja Ngoma, nah ii ndiyo hali niliyoikuta (labda nilienda eneo jingine- siamini). Ni kama Tumejiroga, sio bure!!!


Nyumba za makazi zinazozunguka Kiwanja Ngoma

Barabara inayopita mbele ya kiwanja ngoma

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP