Pekua/search

Monday, June 29, 2015

NANI MWENYE UBAVU WA KUONDOKA CCM katika 40 hawa?


NANI MWENYE UBAVU WA KUONDOKA CCM katika 40 hawa?
  • Wenye Kuvuma, wanayo mengi ya kupoteza wakiondoka CCMMoja ya nadharia (nadharia nyepesi) ya kubomolewa kwa MFUMO KONGWE kama uliojengwa chini ya CCM, ni kwa chama kongwe kama CCM kumeguka kwa wakati muafaka. Kwa jinsi hali ilivyo nchini Tanzania hivi sasa, kumeguka huko kungeweza kutokea kwa mmoja au baadhi ya wagombea kujiondoa ndani ya CCM na kujiunga na Chama kingine cha siasa chenye usajiri wa kudumu. Ni ngumu kuanzisha chama kipya. 

Kwa kuchungua na kutafakari wagombea uteuzi wa CCM wanaofikia 40, SIMUONI YEYOTE ANAYEWEZA  KUONDOKA! Nayaona makundi mawili makubwa: 

Liko kundi la wale wenye mtaji wa MAJINA YAO KUVUMA (kwa sababu mbali mbali ikiwemo UADILIFU wao ama kuwa na MTANDAO MPANA uliojengwa kwa muda mrefu kwa jasho na damu nk); hawa wangeweza kuwa na nafasi kubwa ya kuondoka na kukitikisa chama hicho, hata hivyo kundi hili hata lingekuwa na uungwaji mkono wa watu milioni kadhaa, LINAYO MENGI YA KUPOTEZA likiondoka CCM. Uwepo wao ndani ya CCM ni kama MISHIPA YA DAMU KUTOKA AMA KUELEKEA KWENYE MOYO.

Kundi la pili ni la watia nia ambao, HAWANA KIKUBWA CHA KUPOTEZA wakiondoka ndani ya CCM, lakini hawa tofauti na lile kundi la kwanza, HAWAUZIKI kivile kwa hiyo, kuondoka kwao hakuwezi kuwa na madhara ya maana kwa  CCM.

Uwezekano mkubwa ni kwamba maamuzi yoyote yatakayofanywa na vikao vya uteuzi vya CCM ikiwemo Kamati Kuu KUKATA MAJINA yasiyotarajiwa na wengi, CCM kitaweza kufikia MARIDHIANO kama ilivyo kawaida yake. Tanzania itashuhudia kwa mara nyingine, watia nia wanaosigana hivi sasa wakishirikiana kutafuta ridhaa ya watanzania kuendelea kuwatawala tena kupitia chama chao. 

Bahati kwa CCM ni kwamba tayari imedhihiri kuwa MABADILIKO HAYAWEZEKANI KUTOKEA NDANI YA CHAMA HICHO (kwa kuwatazama wanaowania uteuzi wote). IMESHINDIKANA!!! HIVYO COMPROMISE IS THE MOST LIKELY THING TO HAPPEN.

Bahati pekee (KWA WATANZANIA WAPENDA MABADILIKO) itakayoweza kutokea ni kuwa katika harakati za KUTAFUTA MARIDHIANO na kujaribu kukinusuru chama chao, wanaweza kupitisha jina la mtia nia dhaifu sana. Mtia nia dhaifu ambaye itawawia ngumu kumnadi. 

Tunapoelekea Julai 12, ambayo haiko mbali sana, tushikirikishana mitazamo katika hili!!

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP