tag:blogger.com,1999:blog-2865033805917591468.post9097180893598601635..comments2024-01-01T06:24:14.184-08:00Comments on UPOLE: WHERE DOES OUR CHILDHOOD CREATIVITY VANISH TO??Adamhttp://www.blogger.com/profile/04784485230438493932noreply@blogger.comBlogger3125tag:blogger.com,1999:blog-2865033805917591468.post-81878354611414501652009-08-28T02:55:54.249-07:002009-08-28T02:55:54.249-07:00pole brother adam kwa kuondokewa na babako.Bwana a...pole brother adam kwa kuondokewa na babako.Bwana ametoa,bwana ametwaa,jina la bwana lihimidiweAnonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-2865033805917591468.post-41297732184296731642009-08-15T03:08:20.199-07:002009-08-15T03:08:20.199-07:00Mkuu nimekusoma. Niliiona makala yako nzuri hiyo, ...Mkuu nimekusoma. Niliiona makala yako nzuri hiyo, nikaiwekka kiporo, eti nilikuwa bize, kumbe sikuisoma kabisa - hata ulivyochombeza kuwa 'mimi nami ni mwanazuoni mvumbuzi' nikawa sikio la kufa, sikuweza kukumbuka kuisoma makala yako. LEO NIMEISOMA. NI Ni nzuri.

Vema niongeze mfano mmoja wa 'Raslimali watu iliyopotezwa'. Miaka ya mwishoni mwa tisini nikiandikia gazeti la majira, nilikutana na mtanzania mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari Mbeya almaarufu Mbeya day. Huyu mtu mahiri kweli kweli kwa mambo ya tekinolojia na elektroniki. Nilikutana naye katika shule ya sekondari ya wasichana Loleza alipokuwa akionyesha uvumbuzi wake ikiwemo mitambo mbali mbali aliyotengeneza kkwa kutumia 'mabaki ya chuma, nyaya nk'. Kitu kilichovutia macho yangu hata nikaandika makala gazetini, ni kitu kama kengele ya mlangoni. lakini hii (nadhani ilikuwa digito kweli kweli' maana inafanya mambo lukuki ikiwemo kukuambi subiri,nk kadri mwenye nyumba navyoweza 'kuiprogramu'.
wakati huo nadhani alikuwa kidato cha pili.

Upande wa kuvutia kwa kusikitisha ni kwamba, alipofika kidato cha tatu, alipangwa masomo ya biashara - pengine awe mhasibu - awe na mijihela, siwezi kujua. Hata hivyo kijana yule aliendelea kushinda MAABARA- his 'favaouurite place at school' kama aliivyonijulisha.

Nilipojaribu kumfuatilia miaka ya baadaye kidogo - alinijulisha kuwa alipangiwa na serikali kwenda mzumbe kusoma kitu kama ADCA - sijui ndiyo advanced Diploma ya Certified Accounts footokopi tugeza sijui nini nini huko.Pamoja na hayo aliahidi kunialika kwenye uzinduzi wa HELKOPTA ALIYOTENGENEZA!!! Mkanda ukakatika. sikumsikia tena!!! pengine nitafanya bidii kumtafuta, niusikie ushuhuda wa safari yake.

Nini kiliwazuia walimu au yeye mwenyewe kusoma masomo yanayofanana au yanayoweza kusaidia kukuza karama na vipaji vyake? Sipati picha. sipati jibu.

Naungana nawe Chambi, na hata John Cheyo, Tanzania hatukujaliwa tu raslimali za kipekee kama milima maziwa namadini nk nk; bali zaidi wingi wa vipaji miongoni mwetu.Adamhttps://www.blogger.com/profile/04784485230438493932noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-2865033805917591468.post-16966119819706889962009-08-14T20:48:12.961-07:002009-08-14T20:48:12.961-07:00Mkuu asante kwa picha hii. Tupo pamoja. Kwa upande...Mkuu asante kwa picha hii. Tupo pamoja. Kwa upande wangu mawazo yangu ni yale yale, yaani, haya hapa: http://udadisi.blogspot.com/2009/05/wavumbuzi-wetu-wanapotelea-wapi.htmlChambi Chachagehttps://www.blogger.com/profile/00276865146983534298noreply@blogger.com