Simlilii Mzee Millinga. Najililia mwenyewe na Wanazuoni wenzangu.
Mpendwa Adam,
Asante kwa kuliangalia hili kwa mtazamo tofauti na wenye kutufikirisha. Ukweli ni kwamba tunadhani kuwa muda wote ni kwa ajili yetu na pia kwa ajili ya mambo yetu (yenye mantiki na hata yasiyo na mantiki).
Linalowezekana leo, lisingoje kesho.
Ngoja ngoja, utakuta mwana si wako.
Nadhani kuna haja ya kufukuzana na wakati katika kutekeleza wajibu wetu ili tusijeulizwa na kulaumiwa na watakaokuja baadaye kwa kushindwa kutimiza wajibu wetu.
'Inawezekana; nikianza kubadilika mimi'
Asubuhi njema.
KISINDA,Octavius Alex
P O Box 13547
Dar es Salaam
Tanzania,The United Republic
Mobile: +255 754 470 321
'..........of all the things, be yourself.'
----- Original Message ----From: lingson adam
Ya kwangu imetoweka kidogo. Namaanisha Amani ya nafsini.
Nimesoma makala ya kamaradi Chambi hivi punde. Ndio maana moyo wangu sasa umegoma kumlilia mzee Millinga. Najuta. Najililia mwenyewe na wanazuoni wenzangu. OLE WETU NA U BIZE WETU, MASKINI SISI.
Nimeelewa sasa maneno ya Bwana Yesu alipoangikwa pale msalabani, alipowaambia wanawake wa Yerusalemu, "Jililieni wenyewe na watoto wenu". Simlilii mzee Millinga. Alifanya yaliyompasa. Sasa katoweka, ANAPUMZIKA KWA AMANI. AMIN.
Najililia mwenyewe kwamba sikuweza kwenda kusikiliza alichotaka kutwambia. Nakumbuka mwaliko ulitoka siku nyingi.Chambi alipiga kelele weeeeeeeeeee. Wengi walihamasika. Adam, mimi sikuwa mmoja wao. Ole wangu. Lakini OLE WENU PIA NINYI AMBAO HAMKWENDA, PAMOJA NA KWAMBA MLIJITOA KUTAKA KWENDA. AH nisiseme zaidi. Ila Ole wetu. Sababu ni kwamba tuko bussy jamani.Bussy bussy bussy saaaaaaaaaaaaaaaaana. SWALI LINALONIJIA NI TUKO BUSSY NA NINI?:
umaskini wetu?
Ujinga wetu?
Woga wetu?
hofu yetu ya kuthubutu?
n.k, n.k, n.k,
MAJI YAMEMWAGIKA, HATUTAYAZOA ASILANI. KAMARADI CHAMBI KAJARIBU KUJIFARIJI KWENYE MAKALA YAKE ETI NDUGU ZAKE WAPO HAI, KWA HIYO TUNAWEZA KUAMBULIA MACHACHE KWAO, SAWA. lakini TUJIFUNZE.
JE NI FURSA NGAPI TUNAZIPOTEZA NA TUTAENDELEA KUZIPOTEZA KWA KUDHANI NA KUTAMANIA KUCHUKUA HATUA? JE WEWE MWANAZUONI UNAESOMA TU MAWAZO YA WENGINE HUMU MTANDAONI, UTASUBIRI HATA LINI KABLA HUJACHUKUA UAMUZI WA KUCHANGIA MAWAZO YAKO? JE UTAANZA LINI?
JE WEWE MWENYE NIA YA KUGOMBEA UONGOZI WA KISIASA UNADHANI UTANGOJA HATA LINI?
JE WEWE MWENYE NIA YA KUJIENDELEZA KIELIMU, KUJENGA NYUMBA, KUOA AU KUOLEWA UTASUBIRI HATA LINI?
SAA YA UKOMBOZI NI 'SASA'
MZEE MILLINGA MIMI SIKULILII. SASA NAILILIA NAFSI YANGU. NAIHIMIZA NAFSI YANGU IJITUME KUAMUA NA KUCHUKUA HATUA PASIPO KUAHIRISHA AHIRISHA SANA.
HII NI HESHIMA YANGU KWAKO BABA YETU MILLINGA.
MAY U REST IN PEACE huku sisi tukihimizwa na Kuhanikizwa kuwa in PIECES.
ADAM, L.
From: Prof. Issa Shivji
Inasikitisha. Mzee Millinga alikuwa mwanzilishi wa vijiji vya RDA. Mnamo mwaka 68 au 69 niliwahi kuwasliana naye na Ibbot kuhusu dhamira yangu kwenda kuishi katika kijiji kimojawapo cha RDA huko Songea wakati wa likizo. Ninakumbuka nilienda kumuona katika ofisi yake ya TYL. Alihamishwa TYL ninafikiri makusudi. Nia ilikuwa kumuondoa kutoka RDA. Ni historia ambayo haijaandikwa wala kueleweka vizuri.
Issa
----- Original Message -----
From: Chambi Chachage
To: Wanazuoni - Informal Network of Young Tanzanian Intellectuals
Cc: Study Group
Sent: Tuesday, July 15, 2008 9:52 AM
Subject: Taarifa ya Msiba
Ndugu Wanazuoni,
Rejea taarifa za masikitiko zilizoambatanishwa hapo chini. Muasisi wa RDA, Mzee Milinga, hatunaye tena. Ni matumaini yangu kuwa sisi kama Wanazuoni tutaendeleza mapambano aliyoyaanzisha Mzee wetu na kuenzi jitihada zake za kujenga jamii inayojitegemea. Mwenyezi Mungu na azidi kuifariji familia yake katika kipindi hiki kigumu.
Amen,
Chambi
----- Forwarded Message ----From: suleman toroka <s.toroka@gmail. com>To: Chambi Chachage
Ndugu Temu,
Ni kweli huu ni msiba mkubwa kwa wale waliomfahamu na kuwa karibu naye katika uhai wake.
Leo mchana anazikwa nyumbani kwake Peramiho
Salaam,
Toroka
On 7/14/08, Apollo BS Temu <atemu@calder- systems.com> wrote:
Ndugu zanguTumepokea taarifa ya msiba za Mzee Millinga kwa masikitiko makubwa tukiwa huku, Scotland. Nimeongea kiasi na Mzee Ralph Ibbot jioni ya leo.Salam zetu za awali za pole kwa familia na marafiki wote. Kuna mengi ya kukumbukia na ku "reflect" kama hatua ya kuheshimu aliosimamia marehemu katika maisha yake.Regards,Apollo TemuEdinburgh, Scotland