Pekua/search

Friday, April 19, 2013

Utawala Bora Chimbuko lake Katiba yetu



Utawala Bora Chimbuko lake Katiba yetu

Katika harakati za kufuta ujinga nimekutana na hii kitu kuhusu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa chimbuko la Misingi ya Utawala Bora:

       Wananchi ndio chimbuko la mamlaka na madaraka ya serikali; Ibara 8 (1)(a);

      Katiba ya nchi ndiyo sheria ya msingi (sheria mama) na sheria zingine zote hufuata masharti ya Katiba – Ibara 64(5);

      Ushiriki wa wananchi katika vyombo vya dola - Ibara 8 (1) (d), Ibara 21;
      Mgawanyo wa madaraka – Ibara 4;

      Serikali kuwajibika kwa wananchi – Ibara 8(C)


      Heshima kwa binadamu na utu wa mtu – Ibara 12;

      Utawala wa Sheria – Ibara 9(b);

      Usawa mbele ya sheria – Ibara 13.  Hiki ni kile kifungu kisemacho, “
Watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ubaguzi wowote, kulindwa na  kupata haki sawa mbele ya sheria.”
.

Thursday, April 18, 2013

Political will will improve the living standard of the poor majority in the country.



In ten years, Tanzania has recorded a 7 per cent GDP growth with the remaining poor living standard of people, whereby, more than 60 percent of the Tanzanians live below the International poverty line despite constancy increase in the country’s GDP.  By the end of 2012 the number of the poor was more than 14 million.

It time now for the government leaders to wake up and commit to ensure the improvement living standard of the poor majority in the country.  There should be a political will as what happened to Franklin D. Roosevelt, the 32nd US president who commits to establish an American standard of living without leaving behind any fraction of his people. He vision for the security and economic liberty of the American people in war and peace. 

“It is our duty now to begin to lay the plans and determine the strategy for the winning of a lasting peace and the establishment of an American standard of living higher than ever before known. We cannot be content, no matter how high that general standard of living may be, if some fraction of our people—whether it be one-third or one-fifth or one-tenth—is ill-fed, ill-clothed, ill-housed, and insecure.”

His words matter as much now as they did over sixty years ago. Our country needs to improve the living standard of the poor majority, most of who lives in rural areas (over 75%) and depend on Agriculture.
   
According to Prof. Ibrahim Lipumba, there must be sustained growth of the agriculture sector that increases the productivity of small-holder farmers to at least 6 percent a year for a decade. Employment creating manufacturing sector that grows at an average rate of 12 -15 percent for a decade can reduce poverty at a fast rate.

“We need an effective state that can manage and use public resources effectively, invest in infrastructure, particularly reliable power, water supply, good roads and promote a better business climate,” 

However, Professor Lucian Msambichaka from the Department of Economics at the University of Dar se salaam once said countries with larger numbers of leaders without political will to develop the people contribute much on people’s poverty as they are not ready to serve the poor.

“Political commitments among key leaders need to focus on the goals they need to achieve to rescue the poor from poverty.”

In order to reduce Poverty in our country, the government should have special attention and focus on agriculture activities, on which about 80% of the Tanzanians depend.  And to improve the sector, Hand hoe (cultivate about 70% of the crops) should be  replaced by the use of tractors and merchandise equipment, there should be value addition to the produce and the improvement of the price of goods produced. 

Let's be content to have true individual freedom in the country; an individual with economic security and independence. 

"True individual freedom cannot exist without economic security and independence. “Necessitous men are not free men.” People who are hungry and out of a job are the stuff of which dictatorships are made".- Franklin Roosevelt.
.







Tuesday, April 16, 2013

KUPANDA KWA BEI ZA NAULI NA ATHARI ZAKE KWA WANANCHI WENYE KIPATO CHA CHINI



Kupandishwa kwa gharama za usafiri kumekuwa na mapokeo hasi kwa baadhi ya wadau jijini Mwanza, hasa ukizingatia gharama za maisha kuwa juu, zaidi kwa watu wenye kipato cha chini. 

Wakiongea na mwandishi wa makala haya kwa nyakati tofauti tofauti, juu ya ni kwa jinsi gani wamepokea kauli iliyotolewa na mamlaka ya uthibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA) juu ya  kupandishwa kwa nauli, wadau tofauti tofauti walikuwa na maoni mbalimbali juu ya suala hilo 

Bwana Gudluck John, mtumishi katika sekta ya umma,  anasema, “nilipokea taarifa hiyo kwa mstuko sana ukilinganisha na hali ya maisha kuwa ngumu. Kiwango kilichopandishwa ni kikubwa sana ukizingatia ukweli kuwa hali hiyo itapandisha gharama  za maisha wakati misharaha haipandishwi.”

“Kwa sasa nitatakiwa kutumia TSH 800/= kwa siku kwa ajili ya usafiri, gharama ambayo kwa mweizi itakuwa takribani TSH 24,000/=. Nikiongeza na nauli ya watoto wangu watatu, ambayo itakuwa takribani TSH  37,000/=, kwa mwezi nitakuwa natumia  zaidi yaTSe3H 61,000/=; gharama ambazo ni kubwa sana ikiwa mshahara utabaki kuwa ule ule ambao nilikuwa natumia nauli ya takribani 32,550/= kwa mwezi,” Bwana Gudluck anafafanua. 

Bibi Angela Willy, mkazi wa Butimba na mtumishi katika sekta binafsi, anasema kuwa hofu yake kubwa ipo kwenye upandaji wa bei za vyakula kutokana na gharama za usafirishaji. “Bajeti yangu kwa ajili ya chakula itaongezeka kulingana na bei ya vyakula itakavyopanda. Jambo ambalo litafanya maisha kuwa magumu kwani mshahara huo huo niupatao ndio  utatakiwa kugharamia gharama hizo”, anasema Bi Angela. 

“Serikali pamoja na waajiri katika mashirika yasiyo ya kiserikali  watufikirie wafanyakazi, kutokana na gharama za maisha kupanda, kwa kutuongezea mishahara ili tuweze kumudu hali hii” anashauri  Bi Angel.

Hata hivyo, kwa kuhusu suala la upandaji wa bei za vyakula, imeelezwa kuwa kupanda huko kwa nauli hakutoathiri bei za vyakula katika masoko ya bidhaa hizo jijini kutokana na msimu wenyewe kuwa ni wa mavuno.   

Athuman Kalinga ni msafirishaji  wa bidhaa mbalimbali za vyakula kutoka Bukoba na kuzileta katika soko kuu jijini humo anasema kuwa, pamoja na kupanda kwa bei za nauli yeye na wafanyabiashara wengine hawatoathirika kiasi cha wao kupandishiwa gharama za usafirishaji wa bidhaa hizo kutokana na sababu kuwa usafiri mkubwa wanaotumia ni kwa njia ya meli na kuwa gharama za usafirishaji zinaendana na kiasi cha bidhaa zinazosafirishwa.

“Asilimia kubwa ya mchele unaouzwa katika maeneo mbalimbali ya jiji hili ni kutoka Mwanza na shinyanga ambapo husafirishwa kwa njia ya marori lakini maharagwe na mahindi hutolewa mkoani Kagera ambapo husafirishwa kwa njia ya meli,” anafananua msafirishaji  huyo.

Zaidi, Bwana Kalinga, ambae pia ni mfanyabiasha wa bidhaa za chakula katika soko hilo, anaongezea kuwa ,kwa aonavyo yeye, hali hiyo pia haitoathiri bei za vyakula. “Bidhaa za vyakula haziwezi panda bei  kwa sababu kipindi hichi ni cha mavuno,” anasema.

Bwana kalinga ameendelea kusema kuwa kwa sasa bei za mchele, kwa mfano, zimeshuka toka kiasi cha TSH 2000 kwa KG moja na kuuzwa kati ya TSH 1700 na 1800; sababu kuwa msimu huu ni wa mavuno kutakuwa na mchele mwingi sokoni, bei ya mchele haitoweza kupanda. 

“ Kama unavyojua kama bei imeshuka huko tunapochukua kwa mkulima hiyo haiwezi kutufanya kupandisha bei za vyakula, ukiangalia maharagwe na mahindi tunanunua Bukoba na tunasafirisha kwa meli lakini katika kusafirisha mzigo mkubwa kama tunaosafirisha melini wala nauli yake haipandi kwa hiyo hatuwezi kupandisha bei” anasisitiza .

Dr. Odass Bilame, mchumi kutoka chuo kikuu cha Mt. Augustine Tanzania (SAUT), amesema kuwa licha ya kuwa kwa sasa ni msimu wa mavuno, baada ya msimu huu kupita kwa kiasi fulani gharama za bei za vyakula zitapanda kutokana na upandaji huu wa nauli kuathiri gharama za usafirishaji. 

Pia, Dr. Bilame anaongezea kuwa mfumuko wa bei utaathiri sana wananchi ambao kipato chao ni cha chini; tabaka kati ya masikini na matajiri litaongezeka. “Mishahara, kwa mafano, wanayopewa walimu ni midogo ukilinganisha na ya mawaziri. Hivyo, kupanda kwa bei za nauli kutaathiri sana gharama za maisha yao na hivyo, kushindwa kutimiza malengo yao ya kuwa na maisha bora,”anasema Dr. Bilame.

Hata hivyo, Dr. Bilame anatoa angalizo kwa serikali kuwa inatakiwa kuangalia mfumuko wa bei wakati ikifanya maamuzi ya bei za vitu kupanda, kama iilivyopandisha bei za nauli kwani mfumuko wa bei unaathiri fursa endelevu za kiuchumi kwa wananchi na hivyo, kuikosesha nchi yetu kushinda tuzo ya utawala na maendeleo ya uchumi katika nchi za Afrika. 

Pia, anaishauri serikali kuwa na mpango maalumu wa kuwashirikisha wadau mbalimbali kabla ya kufanya maamuzi ya kupandisha nauli badala ya kufanya maamuzi hayo pekee yao.
Mwisho, Dr. Bilame aliitaka serikali kupunguza kiwango cha kodi kwenye mafuta kwani ndio sababu kubwa ya nauli kupanda. 

kwa upande wa wasafirishaji, Dr. Bilame anawataka waangalie uwezekano wa kununua vyombo vya usafiri vilivyovipya ili kuondokana na gharama za kununua vipuri mara kwa mara kwa ajili ya vyombo hivyo ambavyo ni chakavu. 

Kupanda kwa bei za nauli kulitangazwa mwanzoni mwa mwezi huu na SUMATRA, chombo chenye mamlaka ya kisheria kufanya mapitio ya bei za nauli; bei hizo zimekwishaanza kazi rasmi tangu jana tarehe 12/04/2013, licha ya wasiwasi unaoonekana katika jamii juu ya kupanda kwa gharama za maisha na hivyo, kufanya maisha kuwa magumu zaidi kwa baadhi ya watu, hasa wenye kipato cha chini.


Wednesday, April 10, 2013

Ingekuwa vipi Rais Kikwete angewalabua vibao Dkt Kawambwa na Mulugo kwa matokeo mabaya kidato cha nne 2012? Tafakari adhabu ya viboko shuleni.


Imepigwa kutoka kwenye kijitabu cha Twaweza- Adhabu ya viboko.

Ingekuwa vipi Rais Kikwete angewalabua vibao Dkt Kawambwa na Mulugo kwa matokeo mabaya kidato cha nne 2012? Tafakari adhabu ya viboko shuleni.

Mhe. Mulogo na Viboko vyao.
Ingekuwa vipi Rais Kikwete ANGEMLABUA kibao Dkt. Kawambwa, au Mulugo kwa 'kufelisha wanafunzi???'. SI VIBOKO NI MUHIMU KTK KULETA UFANISI? Shukrani Twaweza kwa katabu haka kanakofikirisha.
 
Emmanuel Mwakyusa UMEONAAA hapooo hakuna akitu kinaendaa kitumwaa kitumwaa viboko kwa mwananfunzi vinafaa inapohusu sioo njiaa pekee ya kujengaa jamii boraa kwani hataa wakikuaa watahitaji viboko kutoendeshaa garii taa zikiwakaa nyekunduu unakuwa unawafundishaa nidhamu ya wogaa badalaa ya nafs ya kuuuliza na kuelewaa nini hasaa wanatakiwa kufanyaa

Adam Gwankaja haswaaaaaaaaaaaaaa...

Emmanuel Mwakyusa hatupingi vibokoo vinaa vigezo na mashart tenaa visizoelekee ilaa vitumikee kwa kiasi na sababu lakini kama walimu hawalipwi vitabu hakunaa mitaalaa mibovu na mawaziri hawajui hataa MUUNGANO wa nchi yaoo muwatwike viboko wanafunzi kwa misingi ipi hasaaaaa ?

Kusoma michango zaidi katika mjadala huu Facebook bonyeza HAPA

Friday, April 5, 2013

CCM Kitaachwa kiwakumbatie Mafisadi mpaka lini?



CCM Kitaachwa kiwakumbatie Mafisadi mpaka lini?
 
Nape Nnauye. Krediti: Gazeti Mwananchi
Wengi wameshitushwa na habari iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima la Alhamisi tarehe 4 Aprili mwaka huu kuwa kamanda wa upambanaji dhidi ya ufisadi Dkt Harrison Mwakyembe naye ni fisadi (http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=47479 ). Bahati nzuri chama cha mapinduzi CCM kupitia katibu wake mwenezi Nape Nnaye  kimejibu tuhuma hizo na kusisitiza kwamba zabuni hata haijapewa kampuni ya chama hicho bado.   Lipi ni sahihi tunaendelea kuchakata kwenye mbongo zetu na waandishi wa habari uchunguzi watatujuza inshallah.

Katika taarifa ya Nnauye aliyoitoa kwa vyombo vya habari anaeleza yafuatayo,
Lakini tunazo taarifa kuwa uongo huu wamelishwa na baadhi ya mafisadi waliotakakutumia eneo hili la CCM kujaribu kukaa katikati ya mwekezaji yeyote atakayejitokeza na Jitegemee kwa lengo la kujinufaisha wao binafsi. Na huu ni mwendelezo waChadema kutumiwa na mafisadi katika kutimiza mambo yao.”...anahitimisha taarifa hiyo kwa kusema, “Tunawataka wasikatishwe (wizara ya uchukuzi chini ya Mwakyembe)  tamaa na mafisadi wachache,wachape kazi kwa uzalendo huohuo waliouonesha.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa mara nyingine CCM kinaeleza waziwazi kuwa kinawafahamu mafisadi na kwamba kinajua kuwa mafisadi wamekuwa wakikitumia CHADEMA. Hawa mafisadi ni kina nani? Wako chama gani? Yawezekana wakawa chama chochote ama hawana chama kabisa, lakini je  CCM ambacho ni chama tawala pamoja na serikali yake kinafaidika vipi kwa kuwatazama tu hawa mafisadi? Kitaendelea kuwafuga hata lini? Najiuliza tu.

Wakati umefika wa moja ya mambo haya kufanyika;
(i)            CCM kuiagiza serikali yake kuwashughulikia mafisadi au
Watanzania kukiwajibisha chama hiki kwa kukumbatia mafisadi

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP