Pekua/search

Wednesday, May 7, 2008

KANUNI MUHIMU YA BUNGE IWAPAYO NGUVU WANANCHI (LAKINI HAITUMIKI!!!!)

Amani iwe juu yako..
MOTO MKUBWA HUANZA KWA CHECHE” Alhaj Ali Hassan Mwinyi.


Hapa chini nakuleteeni nukuu ya kanuni moja ya Bunge kama ilivyowasilishwa na Dkt. Wilbroad Slaa, hivi majuzi (Mei 2, 2008) kwenye mdahalo wa ulingo wa maendeleo hapa mjini Arusha.

“Kanuni ya 34 ya Kanuni za Bunge inatoa nafasi adimu sana ambayo katika Bunge letu haijawahi kutumika tangu uhuru kwa vile si Wabunge au Wananchi wanaoielewa vizuri kanuni hii. Kanuni hii inatamka ifuatavyo, ‘Mbunge yeyote anaweza kuwasilisha Bungeni maombi kuhusu jambo lolote kwa niaba ya watu wanaotoa ombi hilo…’ Ombi la aina hii linachukua nafasi kubwa Bungeni, na linachukua nafasi ‘precedence’ kuliko hata shughuli za Serikali. Matakwa pekee ni kuwa lazima liwe limewekewa saini na Wananchi (Wasiopungua 200) wenye kutaka ombi hilo liwasilishwe, na mbunge asiwe na maslahi yoyote na ombi hilo yeye mwenyewe. Hii ni nafasi muhimu sana, kama ingeliweza kutumika. Inahitaji uelewa mkubwa, ujasiri wa wananchi na wananchi kutokuwa na uwoga katika kutafuta na kudai haki zao.” Alisema


Je, hapo hapawezi kuwa mahali pa kuingilia ikizingatiwa hii ni kanuni ya Bunge, si ya chama chochote? Je tuendelee kungoja utashi wa wabunge kuwasilisha ‘hoja’ binafsi? Je inatosha wananchi waendelee kuwalaumu wabunge kwamba hawasikilizi kero zao?

Dkt. Slaa anasema, “Inahitaji uelewa mkubwa..”
Nani atawajengea uelewa mkubwa wananchi? Mimi nimekutumia wewe mbiu hii (bila kujali iwapo unajua au la), ni vema ukiimuvuzisha zaidi….
Wasalaam,
Adam, L

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP