Pekua/search

Sunday, August 22, 2010

KUANGUKA KWA JK; JITIHADA ZA KUFICHA KILICHOTOKEA NA KUTELEZA KWA ULIMI

Rais Kikwete akiwa amebebwa. Picha kutoka tovuti ya wavuti

Tulishuhudia TV zikielekezwa kwingine baada ya rais wetu Jakaya Kikwete kupatwa na masahibu viwanja vya jangwani wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama cha mapinduzi. Hili labda  lilisukumwa na hofu ya kusababisha taharuki, iwapo mambo mabaya zaidi yangemtokea rais wetu kipenzi (Mungu apishie mbali). Hili sitalijadili zaidi ila ninampa pole mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa masahibu hayo. Kama alivyosema Makamba, Mungu yupo na amjaliye afya tena.
Ninachojadili hapa ni jitihada za baadhi ya magazeti kujitahidi kutolizungumzia kabisa tukio la kuishiwa nguvu na kuanguka kwa rais wetu kipenzi. nitafanya uchambuzi wa gazeti la Nipashe Jumapili. Gazeti hili kwa ujumla halijazungumzia kabisa tukio la jangwani. Hata hivyo, kama wanasaikolojia wanavyozungumzia ‘kuteleza kwa ulimi/ slip of the tongue’ gazeti hili limeishia kutoa msisitizo wa pekee wa kuanguka kwa JK jana.
Kwa maneno rahisi kabisa slip of the tongue ni kukisema kile ambacho kwa sababu moja ama nyingine ‘hakipaswi’ kutajwa. Pamoja na nia ya yeyote au timu yoyote ya gazeti Nipashe Jumapili kutaka kuficha kilichotokea, imeishia kuyamwaga mambo hadharani, indirectly. Hapa pia wanasaikolojia, wanataja sana the power of subconscious mind. Twende pamoja;
kichwa cha Habari kuu kinasomeka; Kikwete: Nitashinda kwa kishindo:
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Hapa neno kishindo linaashiria hamu ya mwandika kichwa hiki kutaka kusema kilichotokea; kutaka kusema ukweli. Je kishindo kipi? Bila shaka ni kishindo cha kiongozi wa watu kuanguka jukwaani.
Kichwa cha habari ya pili kinasomeka; ...CCM yafunika Dar i)
 JK azindua kampeni kwa Kishindo (maana alianguka jukwaani)
ii) Awaambia maelfu: Sitawaangusha (kwa maana ameanguka mwenyewe jukwaani katika siku ya kwanza ya kampeni zake.)
kishindo kimerejewa mara mbili, na kuanguka kumetajwa mara moja, nadhani inatosha kwamba yeyote aliyehusika alikuwa na msongo wa kutosha kutaka kusema kilichotokea kiuhalisia.

3 comments:

Inyinogono sya njanga August 22, 2010 at 11:44 PM  

Napata tabu kujua nianzie wapi kutoa hiki kijicomment changu, lakini kwa haraka haraka mara tu baada ya Rais wetu kipenzi kuanguka jukwaani kumbukumbu zangu zilinipeleka mwaka 2005 wakati Chama Cha Mapuinduzi kinafunga kampeni zake kwa uchaguzi wa mwaka 2005. Kiongozi huyu huyu aliangunga jukwaani lakini hakuna kituo chochote cha luninga kilicho rudia tukio ilo kwenye taarifa zake.

Ili limejirudia tena hapo juzi kana kwamba haitoshi na magazeti nayo yameshindwa kuandika tukio ilo kama mwandishi anavyo tanabaisha hapo juu. Swali la kujiuliza nini kimejisha hapo mpaka wananchi wanashindwa kupiwa ukweli wa kile kilichojili katika viwanja vy jangwani?

Anonymous August 25, 2010 at 9:03 AM  

bofya

http://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=0S2AE3xXR-Q

upate raha nkamu gwangu

Adam August 25, 2010 at 10:57 PM  

Ahsante ndugu yangu.
Nimeiona, niliiona, nikatilia shaka spionage ya Tz kwa sasa. Hivi kweli katika pambazuko hili la teknolojia wanadhani watazuia watu kujua kilichotukia? Anyway, wamefanikiwa, maana watanzania wengi hatufikii mitandao hii.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP