TANZANIA HATUJUANI MPAKA TUGOMBEE UONGOZI AU TUTOFAUTIANE NA WENYE MADARAKA
Hussein Bashe 'kada' wa chama tawala, chama dola cha mapinduzi CCM, amezuiwa kugombea ubunge jimboni Nzega, amenyang'anywa uanachama wa chama hicho kwa kuwa 'si raia' wa Tanzania.
Hadi alipogombea na kushinda kura za maoni Bashe alikuwa mwanachama wa CCM na mtanzania safi kabisa. Hivi asingegombea ingekuwaje? Je watu wengine wasio raia halali wa tanzania, ambao hawagombei uongozi inakuwaje? Vyombo vyetu vya usalama na ulinzi wa nchi ikiwemo idara ya uhamiaji, ni vipi?
TUMEZIDISHA 'SIASA'. TUMEENDEKEZA UCHAMACHAMA TUKAENZI MASLAHI YA CHAMA KULIKO TAIFA, TUNASUJUDIA MAKUNDI. TANZANIA IKO SHAKANI. AMANI YETU NI KAMA YA CHURA KWENYE DIMBWI LA MAJI YALIYOTUAMA BARABARANI. TUMEZIDISHA UTANI.
Suala la Bashe limenikumbusha utata wa 'uraia' wa Generali Ulimwengu.
EE MOLA TUNUSURU.
0 comments:
Post a Comment