KWANINI MABASI HAYARUHUSIWI KUSAFIRI USIKU TANZANIA? - Mjadala
mjadala huu ulianzishwa kwenye mtandao wa kijamii facebook http://www.facebook.com/home.php#!/profile.php?id=1253767086
Kwanini mabasi bado tu hayaruhusiwi safari za usiku? Nchi zenye hali tete ya usalama kama Rwanda na Uganda mabasi yanafanya safari za usiku, kunani kisiwa cha amani Tanzania? Muda mwingi unapotea kwa kuusubiri usiku uishe ndipo safari zianze.
Farida Dadu Hata kenya yanasafiri ucku bila hata wasi.
Adam Lingson Mwamsiku Kweli Farida, na inasaidia sana kuchakata masuala mbali mbali na huwafaa raia wenye mahitaji mbalimbali. Hivi kwanini ni rahisi bongo kutrain polisi wa ziada 'kulinda uchaguzi' afu inakuwa muhali kuganya patrol barabarani usiku? Tutaachwa hata kwenye hili soko la pamoja
Leila Sanga
Andulile Raphael hakika ni swali muhimu hilo kaka. Je wanaotengeneza amani Tanzania wako wapi watujibu, maana siku zote wamekuwa wakisema bila wao amani haipo, sasa hilo inaashiria kuwepo kwa amani?
Leila Sanga
Gospa Lulandala ni kweli kabisa ndugu zanguni, tutaachwa sana kwnye hii EAC, usafiri wa usiku ni muhimu sana, mchana watu wafanye kazi jion watu wasafiri.@andulile Amani ya bongo imeshikiriwa na watu wasio na ufahamu, napata shidi kidogo hawa waTz walio wengi na wasio naufahamu siku wakipata ufahamu sidhani kama kutakuwa na kkisiwa cha amani(Sipati Picha hata kidogo) ngoja tuone itakuwaje
Adam Lingson Mwamsiku @Gospa, umenena vema sana ndugu yangu, we r so relaxed! Eti unasubiri usiku upite ndipo upoteze siku nyingine kwa kurundika matako, kumbe ungesafiri usiku ungelala garini asubuhi unapiga kazi
Jojo Massesa Hapa watanzania wachache waliofanya maamuzi haya hawakuona mbele, waliangalia usawa wa pua na nadhani ilikuwa ni nguvu ya kisiasa tu kufurahishana wakubwa. Imagine tunavyopoteza RASILIMALI MUDA. Tuamshane watanzania, hii rasilimali muda ni muhimu sana na bahati mbaya sana huwa hairudi...
Farida Dadu Sure! Bado tu vichwa vya wenda wazimu,wenzetu wako mbali kweli, na lengo lao kuingia kti EAC c market wanajua wazi ni wapi pa kutupata na vichwa vya wendawazimu.
Adam Lingson Mwamsiku Aa wapi Farida, hatujawa vichwa wala miguu ya mwendawazimu. Tulianzishe tu kushinikiza mabasi yaanze safari za usiku na polisi liimarishe patrol kwenye maeneo ‘korofi’
Jojo Massesa Tena hapa Adam mi naunga miguu kabisaaa. Advocating waruhusu muda huu upoteao usiwe limited na kuendelea kufanya watanzania maskini. God gave us time and in time everything happens. Sasa tusipoutumia muda vizuri... Haya tunaanzia chama cha usafirishaji au...
Adam Lingson Mwamsiku U r right kaka. Tuwaandikie au twende fizikali? Mwanasheria Farida hebu funuafunua ni kanuni au sheria gani zinakwamisha hili?au ni amri tu ya mkuu fulani?
0 comments:
Post a Comment