Pekua/search

Sunday, March 13, 2011

WORKING WITH AND FOR THE PEOPLE: HAVE THE ACTIVISTS DONE ENOUGH?


Maalum kwa wanaharakati (special to activists):
Nimepewa mfano jana, eti mwanaharakati mmoja wa masuala ya sanitation nchi jirani, akawaonea huruma mabinti kwenye shule za sekondari, akajitolea kuwanunulia sanitary towels aka always; alipoanza kuzisambaza na kuwaelekeza namna ya kuzitumia, akastaajabu walipomwambia hawana chupi! wajifunza nini?
Top of Form
Paul Celestine namna tofauti za fikra tofauti kwa watu tofauti katika miktadha tofauti kuhusu mada tofauti na kwa malengo tofauti!
Saimon Kajiba this is the silias case
Magdalena Sylister hahaaaa ! yako mengi sana ya kujifunza - kwamba hao wanafunzi walidhani huyo mfadhili ni Mungu wao kwamba awape kila kitu badala ya wao kushukuru kwa walichopata then kufanya bidii binafsi kutafuta kufuli.
Adam Gwankaja ha ha ha haaaa, Maggie, ngoma ikawa wanazitumiaje? na 'madenti' wafanye juhudi gani binafsi kwa mfano? ukitaka kumsaidia mtu unaanzia wapi?
Saimon Kajiba lakini c jukumu la serikali kuwanunulia nguo za ndani ni wao na walezi wao.....sasa serikali ishughulike na mambo ya msingi tu na sisi jamii tukijitolea kuwahudumia hawa wenzetu wenye mahitaji
Adam Gwankaja ‎@Saimon, hapo serikali iweke tu pembeni kabisaaaa. Mtathimini huyo mfadhili, mabinti na jamii yao.
Negwako Mwakibinga ni huruma!!!!!!!!!!
Saimon Kajiba ebu nijuze nchi gani hiyo? labda ndo utamaduni wao kutokuwa na nguo hizo kama wenzetu wa kaskazini
Saimon Kajiba JAMANI EBUU TUSHEE WOTE NENO HILI: VIGEZI MAANA YAKE NN KWA KISWAHILI?
niwie radhi mwanaharakati adam kuwa nitajaribu kuchangia mfano wako kwa kutoa picha pana zaidi na halisi.mfano huo unaweza kutusaidia kujifunza na kujitambua kwenye yale tuyafanyayo leo.Jana serikali 'imemwaga bajaji za kisasa'kwa ajili ya ...kubebea wake zetu wanapokuwa wajawazito.Hivi bajaji hizo zitapita njia gani kule loliondo,maneromango,nkasi,kishapu,na sehemu nyingine ambako njia zitumiwazo hata ng'ombe anapita kwa shida?ndiyo yaleyale ya kugawa always kwa mabinti ambao maskini ya mungu hawana chupi za kushikiza.Siye watanzania tunagawiwa sana 'always' lakini serikali inajifanya haijui kuwa hatuna chupi.tulizonazo ni kama zile za enzi zile za kukatika katikati zikapanda kiunoni.

Nimesomeka eee!
Elias Loidiso Hapa Emmanuel na Adam lakujifunza ni kuwa jambo lolote tunalohitaji kuisadia jamii ni vyema tukaishirikisha jamii husika. Hawa mabinti wangeulizwa pengine wangesema uhitaji mkubwa walionao ni chupi kuliko sanitary towels.hata serikali mara nyingi inanunua ped kumbe watu hawana chupi!
Emmanuel Lema hata pale bei za vitu zinapopanda hovyo lakini kiongozi anatuambia tena kwa kujigamba eti tatizo siyo sera mbovu ni mtikisiko wa kidunia.Kwanza kumbe anajua fika sera ni mbovu.Asichotaka tuamini ni kuwa hatuna mfumo wa kutupatia chupi za uhakika matokeo yake tunadanganywa kwa pedi tena mbaya sana pedi zenyewe tunapewa wakati ule tukiwa katika hali ile tena kwa nia ya kutuhadaa.
Erasto Golyama Kilowoko hahhahaa aaaa, wewe Adam, bado hujapona tu
‎@Emmanuel na Elias, mmelidadavua vilivyo hili suala. ni kweli, hata katika ulimwengu wa harakati, unashangaa tunaendesha kampeni za ushawishi na utete kwa kundi fulani, only to find, wao wanapenda hali ilivyo. wahusika wanajua mahitaji yao.... Habari hizi ndizo zinazofanya interventions nyingi kama za malaria kwa kugawa net, tunaishia kutumia net hizo kuvulia samaki au kuhifadhia kuku/vifaranga dhidi ya mwewe!!! aibu kwa taifa kama letu!

@Erasto, kumbe kweli bado hujapona, maana usingesahau kuwa mie sikuwa kwenye kundi moja nawe, ila tulikupeleka tu wewe!! enewei, its promising, unaelekea kupona!See More
Beatrice Machaga ‎@ inaonesha jinsi gani wanaharakati wanavyokupukia kutatua tatizo bila kuangalia visababishi vya tatizo. lakini adamu hujatulia mifani gani hiyo?
Adam Gwankaja Haswaaaaaa@Beatrice! Hiyo ndiyo mifano yenyewe! Niseme na ile mingine inayokuhusu wewe moja kwa moja!!
Beatrice Machaga chonde chonde kaka usiseme hiyo!
Benedict Kayombo Haaaaa!!! kumbe usiri ni kila mahali?
Adam Gwankaja Habari ndiyo hiyo @Benedict! Istoshe sio usiri, ni kuchuja tu habari! Usikonde Betty, mi thithemi maana hayapo! Tehe teheeeee!
Benedict Kayombo Ndio maana tunapenda kusikia ya wenzetu na siyo ya kwetu kusikika na wenzetu. Inanikumbusha mbali kwa binti "ADELLA" wa Mrisho Mpoto.
Adam Gwankaja Benedict, na hapo ndipo neno umbea lilipoanzia. Hebu sema yako hapa kaka kiongozi!!!! tehe teheeeee umekomaliiiiiiia ya Betty (wala hayapo!!!) tehe teheeeeeeeeee
Benedict Kayombo Teh!! Tehhhhh!! Rudia posti yangu ya mwisho kabla ya hii, kuna maneno hapo!
Adam Gwankaja haswaaaaa nshaikamata ndiyo nikaandika haya. kama tungependa yetu yasikike neno umbea lingekuwa msamiati adimu, ama vipi?
Benedict Kayombo Haswaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!
Mjadala kwenye kuta za FACEBOOK.
Bottom of Form

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP