Bunge la lakataa Muswada wa Mafao kwa Mawaziri, RC na DC
Bunge la lakataa Muswada wa Mafao kwa Mawaziri, RC
na DC
Ni leo (Juni 26)
katika Historia yetu
Mwaka 1968
Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania lilitumia mamlaka yake na kuukataa
muswada wa serikali wa kutaka kuwalipa kiinua mgongo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa
na wale wa Wilaya.
Hata hivyo muswada huo
ulirudishwa tena Bungeni na kupitishwa kuwa Sheria kufuatia matamshi (vitisho)
ya Rais Julius Nyerere kwamba, endapo wabunge wangeendelea kuupinga muswada
huo, basi ingebidi warudi kwa wananchi (Kulivunja Bunge).
Najiuliza kwa sauti je Wabunge wa leo hii wangethubutu hii kitu?
Jikumbushe Baadhi ya Maspika wa
Bunge tangu Uhuru
- Mhe. Abdulkarim Y. A. Karimjee - Januari 1, 1959 - hadi Desemba 26,1962
- Mhe.Adam Sapi Mkwawa - Novemba 27,1963 hadi Novemba 19,1972 na Novemba 6,1975 – Aprili 25,1994
- Mhe. A. M. Erasto Mang’enya Novemba 20, 1973 – Novemba 5, 1975
- Mhe. Pius Msekwa Spika Pius Msekwa ndio Spika wa Bunge la kwanza la Vyama vingi la 1995 kwa kuwa yeye alikalia kiti cha Uspika kuanzia Aprili 28, 1994 hadi Desemba 28, 2005
- Mhe.Samuel John Sitta Desemba 28, 2005- Novemba 10, 2010. Aliongoza kwa kauli mbiu
ya Kasi na Viwango. - Mhe. Anne Semamba Makinda Oktoba 30, 2010- Spika wa kwanza mwanamke.
0 comments:
Post a Comment