Wanajeshi Shupavu wa Tanzania warejea kutoka Uganda
Wanajeshi Shupavu wa Tanzania warejea kutoka Uganda
Ni leo (Julai 25) katika Historia
Yetu
Hapo mwaka 1979 - Wanajeshi
wa Tanzania waliopigana vita ya uchokozi wa Idd Amin aliyekuwa rais nchini
Uganda, waliwasili katika ardhi ya Tanzania huko Kagera na kulakiwa kwa furaha
kuu na wananchi. Kufuatia tukio hili hivi sasa Watanzania tunaadhimisha siku
hii kuwa siku ya MASHUJAA, badala ya Septemba mosi ya awali.
Jikumbushe baadhi ya Matukio makuu
ya kuhusu vita hivyo:
Oktoba 30, 1978
Majeshi ya Idd Amini aka nduli wa Uganda yalishambulia Kagera na kusababisha
vifo vya watu na uharibifu wa mali nyingi (uchokozi)
Novemba 2, 1978
Amiri Jeshi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais wa Tanzania Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere alitangaza vita dhidi ya uvamizi wa Idd Amini. Baadhi ya maneno
aliyotumia ni maarufu hadi sasa nayo ni, “ Sabababu
tunayo..Nia tunayo ..na Uwezo wa kumpiga tunao..”
Machi 16, 1979
huko Lukaya nchini Uganda majeshi ya wananchi (ya ukombozi) wa Uganda
yakihimiliwa na vijana shupavu wa majeshi ya Tanzania yalipigana vita vikali
zaidi dhidi ya yale ya nduli Idd Amini. Inaelezwa kwamba askari wengi sana wa
majeshi ya Idd Amini waliangamizwa.
Juni 16, 1979
Rais Nyerere alitangaza kumalizika kwa vita ya uchokozi ya Idd Amini
Julai 12, 1979
Wapiganaji wa majeshi ya Tanzania walianza kuondoka Uganda kurudi nyumbani.
0 comments:
Post a Comment