Tumefanikiwa kuwakinyamazisha walimu matokeo tumeyaona...Tunajaribu Madaktari
Tumefanikiwa kuwakinyamazisha
walimu matokeo tumeyaona...Tunajaribu Madaktari
- Walimu wakinyazishwa matokeo yake wanafunzi hawafundishwi wala kusaidiwa kujifunza. Tumefanikiwa katika hili.
- Sasa Serikali inajaribu kuwanyamazisha madaktari....Kwanini hatujifunzi?
Mwl.Makini angependa wanafunzi wake wajisaidie kwenye choo bora zaidi ya hiki |
Nimesoma
post ya Rafiki yangu wa mtandao wa Facebook, Mh Ahmaed Lukinga akihoji iwapo
Walimu mkoa wa Singida wako kwenye mgomo, “SINGIDA WALIMU WAMEGOMA?” Anauliza,
na kuendelea kuifafanua hoja yake kwa kutupa mfano wa mojawapo ya shule
zilizofanya vizuri katika mtihani wa mock kidato cha nne mwaka huu.
Anatupasha
kuwa shule hii iitwayo Ntonge imekuwa ya 20 kati ya shule 124 za mkoa mzima wa
Singida na anatanabahisha kuwa shule hiyo imekuwa na matokeo kama ifuatavyo:
Daraja
la I=0
Daraja
la II=3
Daraja
la III=6
Daraja
la IV=17
Waliofeli
kabisa=2
Zaidi
Rafiki yangu huyu aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu anahoji, “KAMA MKOA MZIMA
UPO HIVO UNATEGEMEA VIWANGO GANI VYA UFAULU KATIKA MITIHANI YA TAIFA KIDATO IV
MWAKA HUU?” na kuongeza, “Hii ndiyo hali halisi, Watanzania wenzangu. Mwl.
Ahmed Lukinga.”
Mwl. aliyenyamazishwa hajali kufundisha ktk darasa kama hili |
Nikiwa
nawaza kwa sauti najikuta kupata hamasa ya kujua zaidi...naishia kujiuliza tu..
hivi kama shule hiyo yenye wanafunzi wasiozidi 30 inafanya hivyo je shule zenye
wanafunzi 100 hali ikoje? Lakini zaidi ikiwa Ntonge ni shule ya 20 kati ya 124
je shule ya 100 imekuwa na matokeo gani?
Narudi
kwenye swali la msingi la Rafiki yangu Lukinga, nadhani si kwamba walimu
wamegoma.. kunao ushahidi wa kutosha kubainisha kwamba walimu WAMENYAMAZISHWA.
Waliposema hali yao ni mbaya kiasi kwamba haiwavutii kuendelea na kazi,
tuliwapuuza na kibaya zaidi tuliwatishia maisha.. mkulu wan chi alisema
wakigoma watakong’oliwa ‘waende kwenye meza ya mazungumzo wakiwa na bandeji na
ngeu.’
Baada
ya kufanikiwa kwenye kuwanyamazisha walimu sasa serikali iko makini kweli kweli
kuwanyamazisha madaktari. Wasiseme, wasihoji achilia mbali kudai
chochote...inawalekeza kuwa meza ya majadiliano ndio mwarobaini lkn katika hali
ya kawaida wakiidai hiyo meza wanatishwa na kutishiwa maisha. Madaktari
wanapaswa kuwa wazalendo...wanasiasa uzalendo wanaweka pembeni. Naami
Naam,
Walimu wamefuata ushauri wa rais, wamekuwa mbayuwayu...hawajagoma wala
kuandamana..na kweli wamepona, hawayajawakuta ya Dkt Ulimboka...ila hali ya
elimu imekuwaje? Hata hivyo tumepata nafasi walau hii ya kuhoji na kujihoji.
Lakini tunapojaribu kuwanyamazisha madaktari.........NATUENDELEE KUISHANGILIA
SERIKALI.
Mwalimu asiyenyamazishwa huwa na ari na ubunifu unaotakiwa kutengeneza na kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia |
0 comments:
Post a Comment