Dar na miji mingine ingekuwa Yatima leo hii- SENSA NJEMA
Utaratibu
wa Sensa usingebadilika- Dar na miji
mingine ingekuwa Yatima leo hii
“Siku
zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya
kwamba IANDIKWE ORODHA YA MAJINA YA WATU WOTE (SENSA) wa ulimwengu
(nchini mwake). Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa
liwali wa Shamu. Watu wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. Yusufu naye aliondoka Galilaya,
toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao
Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa ukoo na jamaa ya Daudi, ili aandikwe pamoja na
Mariamu mkewe, ambaye amemposa naye ana mimba, ikawa katika kukaa huko, siku
zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za
kitoto, akamlaza katika hori la kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi
katika nyumba ya wageni. “ Luka Mtakatifu – 2: 1- 7.
Haya wandugu HESABIWENI. Enzi za wenzetu ingebidi Dar es Salaam kwa
mfano ibaki na watu wachache tu.
Jikumbushe kuhusu sense nchini:
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho
zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002.
Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi
ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603.
Waziri Mkuu Pinda alipozindua uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi 2012 |
Matokeo ya Sensa ya Watu 1967-2002 na Makadirio kati ya mwaka
2003-2025 Mwaka
Idadi Mwaka Idadi
1967
12,313,469
1978
17,512,610
1988
23,095,885
2002
34,443,603
2003
34,859,582
2004
35,944,015
2006
38,250,927
2009
41,915,880
2010
43,187,823
2012
45,798,475
2015
49,861,768
2020
57,102,896
2005
37,083,346
0 comments:
Post a Comment