Kinjekitile Ngware wa Majimaji atiwa nguvuni na wajerumani.
Kinjekitile Ngware wa Majimaji
atiwa nguvuni na wajerumani.
Ni leo (Agosti 24)
katika Historia yetu
|
Mwaka
1905, Wajerumani walimkamata mtanzania aliyekuwa chimbuko la ujasiri wa wana wan
chi katika kuukabili uvamizi wa wageni toka ujerumani huko kusini mwa Tanzania enzi
hizo. Huyu si mwingine bali Kinjekitile Ngware. Hatimaye madhalimu haya
yalimnyonga shujaa na mwanafalsafa wa kitanzania Kinjekitile Ngware, tena
yalimnyonga hadharani huko muhoro, Rufiji.
Jikumbushe
baadhi ya matukio muhimu kuhusu vita vya maji maji:
Agosti
mosi, 1905 vita ya maji maji dhidi ya Wajerumani iliyokuwa imeanza mwaka huo
ilienea na kuyahusisha maeneo ya Songea, Masasi, mtwara, Lindi, Rufiji na
maeneo mengine ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi nchini.
Baadhi ya mashujaa wa maji maji wakiwa wametekwa na madhalimu ya kijerumani |
Agosti
5 1905 wapiganaji wa maji maji walishambulia misheni ya kanisa katoliki
Nachingwea na kumwua Askofu Cassian Speiss. Huyu alikuwa askofu wa kwanza wa
kanisa katoliki jijini Dar es salaam. Kifo kilimfika askoofu huyo akiwa
safarini kueneza dini huku Mukukunumbu, Nachingwea.
Agosti
14, vita kali na vilivyoua watu wengi vilipiganwa huko Liwale, Nachingwea kati
ya wapiganaji wa maji maji na majeshi ya wajerumani. Vita hiyo ilipiganwa kufuatia
kushambuliwa kwa boma ya wajerumani ya Liwale.
Septemba
mosi, kitete kiliwapanda wajerumani maana mashambulizi ya wazalendo yalikuwa
makli san asana sana, hivyo wajerumani walipiga simu nyumbani kwao ujerumani
wakiomba majeshi ya ziada ili kuzatiti mapambano yaliyokuwa yakiendelea.
Chanzo kikuu:
Mwanahistoria J. E. Makaidi.
0 comments:
Post a Comment