Pekua/search

Wednesday, July 25, 2012

Wanajeshi Shupavu wa Tanzania warejea kutoka Uganda


Wanajeshi Shupavu wa Tanzania warejea  kutoka Uganda

Ni leo (Julai 25) katika Historia Yetu

Hapo mwaka 1979 - Wanajeshi wa Tanzania waliopigana vita ya uchokozi wa Idd Amin aliyekuwa rais nchini Uganda, waliwasili katika ardhi ya Tanzania huko Kagera na kulakiwa kwa furaha kuu na wananchi. Kufuatia tukio hili hivi sasa Watanzania tunaadhimisha siku hii kuwa siku ya MASHUJAA, badala ya Septemba mosi ya awali.

Jikumbushe baadhi ya Matukio makuu ya kuhusu vita hivyo:
Oktoba 30, 1978 Majeshi ya Idd Amini aka nduli wa Uganda yalishambulia Kagera na kusababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali nyingi (uchokozi)

Novemba 2, 1978 Amiri Jeshi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitangaza vita dhidi ya uvamizi wa Idd Amini. Baadhi ya maneno aliyotumia ni maarufu hadi sasa nayo ni, “ Sabababu tunayo..Nia tunayo ..na Uwezo wa kumpiga tunao..”

Machi 16, 1979 huko Lukaya nchini Uganda majeshi ya wananchi (ya ukombozi) wa Uganda yakihimiliwa na vijana shupavu wa majeshi ya Tanzania yalipigana vita vikali zaidi dhidi ya yale ya nduli Idd Amini. Inaelezwa kwamba askari wengi sana wa majeshi ya Idd Amini waliangamizwa.

Juni 16, 1979 Rais Nyerere alitangaza kumalizika kwa vita ya uchokozi ya Idd Amini

Julai 12, 1979 Wapiganaji wa majeshi ya Tanzania walianza kuondoka Uganda kurudi nyumbani.


0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP