Dr. Slaa 23:

1 Kisha Dr. Slaa akauambia umati wa Watanzania pamoja na wafuasi wake wa CHADEMA pale Jangwani,

2 "CCM na Mafisadi wana mamlaka ya kufafanua Sheria za Watawala na Ilani zao za Uchaguzi na kutoa Ahadi kem kem.

3 Kwa hiyo wasikilizeni na kupima chochote watakachowaambieni. Lakini msiwape kura zenu wala msiyaige matendo yao, maana hawatekelezi yale wanayoyawahutubia.

4 Hufunga mizigo mizito na kuwatwika Watanzania mabegani, lakini wao wenyewe hawataki kunyosha hata kidole wapate kuibeba.

5 Wao hufanya matendo yao yote ili watu wawaone. Huvaa nguo nzuri za gharama, kutembea na magari mazuri ya gharama na kuishi katika nyumba nzuri za gharama zenye hati za majina yao, au watoto wao au ndugu zao.
6 Hupenda nafasi za heshima bungeni na katika karamu au hafla mbalimbali hupenda viti vya meza kuu ili waonekane.

7 Hupenda kusalimiwa kwa heshima bungeni, maofisini au hata barabarani, sokoni, kwenye sherehe au misibani na kupendelea kuitwa na watu: Mheshimiwa.

8 Lakini ninyi msikubali kuitwa kamwe Mheshimiwa maana Nchi yenu ni mmoja tu na wala haijawagawa wa kuheshimiwa sana wala kidogo, nanyi nyote ni Watanzania mlio na haki sawa za Kibinadamu.

9 Wala msimwite Fisadi yeyote hapa duniani Mheshimiwa au Mtukufu, maana Mtukufu ni mmoja tu Mungu aliye mbinguni.

10 Wala msiitane Mheshimiwa bali Wapiganaji maana kiongozi wenu ni mmoja tu, ndiye Dr. Slaa.

11 Aliye mkubwa miongoni mwenu ni lazima awe mtumishi wenu.

12 Anayejikweza atashushwa, na anayejishusha atakwezwa.

13 "Ole wenu walimu wa Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnaufunga mlango wa Maendeleo ya Kweli mbele ya macho ya Watanzania. Ninyi wenyewe hamwendelei kwa amani, wala hamwaruhusu Watanzania wanaotaka kuendelea wafanye hivyo.

14 Ole wenu CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnawanyonya Watanzania na kujisingizia kuwa watu wema kwa kuwapa misaada ya danganya toto. Kwa sababu hiyo mtapata adhabu kali na kunyimwa Kura.

15 "Ole wenu CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnasafiri Angani, baharini na nchi kavu ili kumpata mtu mmoja afuate Ilani Yenu ya Uchaguzi na Kuwapa Kura. Mnapompata, mnamfanya astahili maradufu kwenda katika Mateso makali wakati ninyi wenyewe mkiponda raha kama mko peponi.

16 "Ole wenu viongozi vipofu wa CCM! Ninyi mwasema ati mtu akiapa kuwa Raia kama Bashe ama Ulimwengu, kiapo hicho si kitu; lakini akiapa kwa kutoa fedha na dhahabu na kukubali kuwa Fisadi, kiapo hicho kinamshika.

17 Enyi vipofu wapumbavu wa CCM! Kipi kilicho cha maana zaidi: dhahabu, pesa au Kuwatumikia Watanzania kitakachofanya hiyo fedha na dhahabu kuwa ya Maana?

18 Tena mwasema ati hata akiwa na Dhahabu lakini Viongozi wake hamjampenda basi si kitu hata kama hana matatizo na hata kama Wananchi walimpitisha katika Kura za Maoni; lakini akiapa kuwa mnyenyekevu, kuwalamba miguu na kuwatumikia matakwa yenu, basi huyo mtu huonekana wa Maana hata kama si Raia kama ilivyokuwa kwa Mustafa Mkulo.

19 Enyi vipofu wa CCM! Ni kipi kilicho cha maana zaidi: ile zawadi, fedha au Uongozi wenu kwa Umma ambao hufanya hizo, zawadi na fedha kuwa za maaana?

20 Anayeapa kuwa Kiongozi wa Umma ameapa kuwa Mtumishi, na Kuwatumikia watu huku akipiga vita Ufisadi wote kwa Uadilifu wa juu.

21 Na anayeapa kwa Chama cha Mafisadi ameapa kwa hilo Mafisadi na pia kwa kulinda maslahi ya Mafisadi Wakuu.

22 Na anayeapa kwa Watanzania na kwa Mungu kuwa muadilifu huyo astahili kupewa Kura.

23 Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnatoza watu kodi mbalimbali, hata juu kwa masikini lakini punde mkikusanya pesa mnaacha mambo muhimu ya yaliyo katika Ilani zenuya Kuleta maendeleo ya Kweli na kuwanyima watue haki, huruma na imani. Haya ndiyo hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.

24 Viongozi vipofu wa CCM! Mnatoa inzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!

25 "Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnasafisha kikombe na bakuli kwa nje, lakini ndani mnaacha kumejaa vitu mlivyopata kwa unyang'anyi na uchoyo wa Watanzania Masikini.

26 Wana CCM na Mafisadi Vipofu! Kisafishe kikombe ndani kwanza na nje kutakuwa safi pia.

27 "Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mko kama makaburi yaliyopakwa chokaa ambayo kwa nje yanaonekana kuwa mazuri, lakini ndani yamejaa mifupa ya maiti na kila namna ya uchafu.

28 Hali kadhalika ninyi mnaonekana na watu kwa nje kuwa wema, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na uovu.

29 "Ole wenu Wana CCM na Mafisadi, wanafiki! Mnajenga makaburi ya Viongizi Waadilifu na kuyapamba makaburi ya watu wema.

30 Mwasema: Kidumu Chama Cha Mapinduzi! CCM Nambari Wani! JK Apewe Kura Za Ndiyo!

31 Hivyo mnathibitisha ninyi wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa watu waliowaua Viongozi Waadilifu kama: Nyerere, Karume, Sokoine, Kolimba, Malima, Kombe, Mwaikambo na wengineo

32 Haya, kamilisheni ile kazi wazee wenu wanafiki waliyoianza!

33 Enyi CCM na mafisadi kizazi cha nyoka wenye sumu! Mnawezaje kuiepa hukumu ya moto wa Jehanamu?

34 Ndiyo maana mimi mmeletewa Mshindani Dr. Slaa na Wapoiganaji wa CHADEMA, watu wenye hekima na Viongozi Makini; lakini mnawapaka matope na kuwachafua baadhi yao, na wengine mnawakatia Rufaa Tume ya Uchaguzi yenu na kuwasakama katika kila mji kwa kila aina ya uzandiki mkiacha kuelezea Sera zenu na kujibu Tuhuma zinazowakabili.

35 Hivyo lawama yote itawapateni kwa ajili ya damu yote ya watu wema iliyomwagwa juu ya ardhi na matope mnayowapaka Wapiganaji wa CHADEMA. Naam, tangu kuuawa kwa Sokoine ambaye hakuwa na hatia, mpaka kuuawa kwa Horice, mwana wa Kolimba, ambaye mlimuua Katika Vikao Vyenu mbele ya wajumbe.
36 Nawaambieni kweli CCM na Mafisadi, kizazi hiki chenu kitapata adhabu na kunyimwa Kura kwa sababu ya mambo haya.

37 "CCM, Ee CCM! Unawaua Viongozi Waadilifu na Kuwachafua Viongozi Wazalendo wenye Uchungu na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako kama Seleli, Mpendazoe na wengine. Mara ngapi nimejaribu kuwakusanya Viongozi Wazuri na Watanzania kwangu, kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka.

38 Haya basi, nyumba yako Dodoma na Lumumba itaachwa magofu!

39 Nakwambia kweli, hutaniona tena mpaka wakati Nitakapoingia Ikulu pale Magogoni