Pekua/search

Sunday, March 13, 2011

WOMEN'S DAY: IS IT MEANINGFUL TO YOU? HAVE YOU DONE MUCH TO CAUSE CHANGE?


Siku ya wanawake duniani bibi huyu katikati ya jiji la mbeya akitokea mlima loleza kuokota kuni. Ilibandikwa kwenye ukuta wa Facebook wa Joseph Mwaisango. Picha zimeondoshwa.
Top of Form
March 8, 2011
Rehema Simba Mwee mwee! Ndaga bibi wa watu ! hata hajui km leo ndo cku yetu ya kujidai. Lol !
Leah Mafwenga mhhh bibi mjasiriamli kweli huyu, nimekubali wanawake tunawezaq toka zamani umeri wa bibi huyo ukimkuta mumewe hatoki hata ndani
Peter Edson pole sana mama, ipo siku mungu atafuta machozi
Judith Kyejo Maskn bibi wa watu
Rehema Simba Bibi ikolonda ehela tu hn ckuku wala nini. Lol !
Adam Gwankaja Umeadhimisha vema cku hii@Joseph! Ahsante na pongezi sana!
Joseph Mwaisango asante nashukuru
Yohana K Mwakisole Jamani sioni sababu ya watu kufurahia hii hali ya bibi hapa huku tukifurahia fikra za wakoloni eti siku ya wamama, ni aibu tena iliyokithiri @rehema think at it tena na tena, then come up with other comment.
Max Mushi Wakina mama wetu wana hali ngumu,hii inaonesha bibi akiwa na mzigo mzito pembeni yake anapita binti(sista duu ) bila kumsaidia bibi mzigo .Ndio maadili ya Tanzania yetu kwa leo .Zamani zile bibi alikuwa wa jamii nzima ilhali mtoto pia .bibi alihitaji kusaidiwa mzigo
Geoffrey George Annaniah Duh mie nilipishana nae NMB pale alafu yupo strong anakaa jakaranda pale
Manka Raymond Mmwee bibi yetu hakuna anaekuonea huruma jipe moyo
Damian Lupogo enzi za mwl huyo dada nyuma yake ndo angekua amebeba mzigo lakin vijana wa siku iz wiziiiii mtupuuuuuuuuuu!!!
Bau Chizza safi huyo anadumisha nini maana kuwa mama
Hamza Kiliwasha its my home village
‎@Katika fikra zake kabeba mawazo mazito ya kujua nini anakula leo na hajui kesho atakula nini,kichwani amebeba mzigo huo wa kuni ambao hajui hata huyo mtejha atampataje na akimpata atanunua hizo kuni au atakopa hadi auze pombe ya kienyeji ...atakayouza ambayo pia wanunuzi wanakuja kunywa wakilewa wanaondoka bila kulipa!pia bibi huyu huenda ana mzigo mwingine nyumbani wa vijukuu ambavyo wazazi wao aidha wamevitelekeza hapo kwa bibi na wao wakihaha mitaani au wameshatangulia mbele ya haki kutokana na balaa lililoikumba dunia la ugonjwa wa UKIMWI ambao asilimia kubwa huua watu maskini.

Inawezsekana bibi huyu umri wake c wa kuitwa bibi bali kutokana na shida zilizomwandama amefikia hatua ya kuwa hivi alivyo, iwapo mwanamke huyu angetengenezewa maisha wakati wa ujana wake ikiwa ni pamoja na kupata elimu bora na kupata huduma muhimu zinazostahiki hata kwa kupata fursa ya kuwasomesha wanawe asingweza kubaki na vijukuu na watoto kuhaha mijini kujiuza au wengine kuingia katika kazi za sulubu na hata baadhi yao kuamua kujiingiza katika kazi za sulubu...JOSE bibi huyu ni mmoja kati ya bibi zetu wengi tuliowaacha huko vjjn ambao tunasahau hata kuwapelekea mfuko wa sukari,kubazi la kutembelea, shuka ya kujifunika wakati wa baridi.

Akina bibi hawa ndio hao hao wanaodanganywa na wanasiasa kuwa wataishi maisha bora na kupewa vijikanga na vijitenge ili watoe kura kwa watu wazandiki wasiojali maisha ya watu wa aina hii hapa nchini....INAUMIZA sana cjui bibi yangu yukoje hali yake huko NANGURUKURU!!!See More
Hebu mwangalieni huyu bibi kwa makini!!! inawezekana akabisa hivyo vitenge na khanga alizojitanda ndio mashuka yake ya kujifunika na pia inawezekana kabisa mgongoni kabeba mboga aliyochuma njiani anavyotoka huko maporini ili akifika tu nyum...bani awacheshie wajukuu chukuchuku wale wanywe maji walale hadi kesho asubuhi waanze kusaka tonge kwa mbinu nyingine..@Jose ...next tyme akina mama kama hawa ni muhimu kujua hata wanaishi vp...kwa kweli ukirejesha kumbukumbu kidogo tu nyuma kujua akina mama wanaokuhusu wanaishi vp unaweza kububujikwa na machozi@Leah huyu mama wala si mjasiriamali dhiki ndo inamtuma kufanya hivi hebu jaribu wewe kuwa mjasiriliamali kama huyu bibi!!!!@ Max...huyu unayemwita Cster du hebu mwangalie vzr usoni unaweza kusoma hisia zake hata bila kuambiwa!!! anataharuki na ndani ya moyo wake anaumia anashindwa afanye nini akijiangalia alivyo yeye huenda naye kawaacha wajukuu kwa mama yake anayefanana na huyu na ameamua kuhaha mitaani kutafuta chochote!!! hapo inamuuma lkn hawezi kufanya lolote.

@Annaniah... unajua hadi anapoishi huyu bimkubwa umefanya jitihada gani kuokoa jahazi hata kwa kujua anaishi ktk mazingira gani na kwa nini anafanya kazi hizi za sulubu?
@Chiza...wala hadumishi hicho unachoita kuwa mama, mama hatakiwi kuwa hivi angekuwa na mtoto kama wewe cdhani kama ungekubali mama yako aishi hivi uso wako ungeuweka wapi hapa duniani kumuacha mama yako akihaha hivi na wewe ungali unavuta hewa ya mwenyezi mungu bila hata kujua bili yake ikoje!See More
Hubert Mtui Huyu sii wa kijijini ni wa mjini wa kijijini ni zaidi
Veronika Kihongo Kijiji ndio usiseme ndugu yangu, wanaishi kiubishi
Elias Loidiso afadhali hata huyo ana mahali pa kuokota kuni. sehemu nyingine akina bibi kama hao wanalala njaa kwa sababu hawana mahali pa kuokota kuni kwa mapori yamechukuliwa na mafisadi au ni ya serikali na watu wamepigwa marufuku kuokota kuni na hakuna nishati mbadala
Adam Gwankaja umeweka angalizo muhimu sana kijana@Elias. imenikumbusha kiongozi aliyelalamikia watu wake kukosa viatu, kumbe hata miguu hawana!!!
Last Wenger Lingson ‎...DEAR GWANKAJA! I've been passing through posts of different fb users, but YOURS ARE some of the few EXCEPTIONAL.....you try the BEST to post something touching, and concerning our affairs!! I officially congratulate you for that bruh!! carry with that race. UMEKUWA MSOMI MWANAHARAKATI wa UKWELI!! little SHITS much SMASH HITS!!
Adam Gwankaja Ahsante kwa kompulimenti@Last! Pamoja kabisa! U too are a great head n mind! Keep it up!
Rashid Mkwinda ‎@Last wenger... umenena kwa lugha mpya! hapa ndo umezungumza lugha gani Kiebrania,Kichina ,Kifaransa au Kibunge bunge!! maana wabunge wetu wana desturi kweli ya kuchanganya lugha hata mahala pasipo stahili kufanya hivyo!!!
Last Wenger Lingson ‎........hahahaaaaa!!! ni ukuwadi wa mambo ya kigeni kaka!! Tunajifanya haiendi bila msisitizo ya kuchanganya lugha!! Lakini mpaka hapo umenipeleka shule kaka......... wakati ujao nitakuwa wa kueleweka zaidi. Asante. @Rashid
Rashid Mkwinda ‎@Last Wenger....Tehe tehe tehe tehe tehe tehe...ucjali kamanda...shukrani!!!!
Adam Gwankaja ‎@Last n Rashid, hamna haja kujisumbua ati! msikodolee macho kidole mkioneshwa mwezi! Utazameni mwezi!!! Ujumbe ulishafika tena kamili!
Raphael Mwakapalila inasikitisha sana sijui nani alaumiwe kwa hali hii kwani haya ni mateso
Adam Gwankaja ‎@Raphael, naam inasikitisha lkn umeambiwa wengine hata pa kuokota hizo kuni hapapo! Lakn pia sijui kama lawame peke yake zitasaidia! Labda tuanze kwa kujiuliza tufanye nini? Labda kila mmoja atimize wajibu wake! Je twawatupia jicho mama na bibi zetu? Baba na babu zetu? Maana twaweza kuwa ndiyo hifadhi yao kijamii kwa kichache tulicho nacho! Halafu tuwaze kuhusu wale wasio na watoto ama wajukuu! Hatua ifuatayo tutimize wajibu wetu kwenye kazi tulizojaaliwa kuzifanya!
Siku ya wanawake ina maana gani kwako?Top of Form
Ambwene Mwasongwe Mwasongwe Kumpa nafasi mwanamke ya kuonyesha uwezo wake na majukumu aliyopewa na Mungu kuyatimiza duniani.
Rosemery Paul Mushi mimi kama mwanamke natakiwa kufuata mjukumu yangu .wanawake 2naweza
Rosemery Paul Mushi ndio mungu aliona adamu hawezi kuwa peke yake ndio akamuumba hawa
Adam Gwankaja ‎@Ambwene na @Rosie, ni naam na amina mlonena!
Ambwene Mwasongwe Mwasongwe Rose mkiamua mnaweza msisubiri kuwezeshwa.
Rosemery Paul Mushi ni kweli hatusubiri kuwezeshwa
Steve Mwambapa Kwa hali ya kawaida mwanaume ni m2 muhm sn,katik kuonyesha hilo Mungu alimkabidh Adam bustan ya eden,lakin akampa msaidiz,ambaye badae kamletea matatiz mengi,na adam alijuta kupewa msaidiz,Mungu akatoa speech,akasema kuanzia leo Hawa/mwanamke utatawaliwa na mwanaume,huyu ni Mung alisema!so inamana wanawake wanapo taka nusu kwa nusu itawezekana??
Adam Gwankaja ‎@Steve, ahsante kwa mchango wako amba ni nukuu sahihi kabisa toka bibliani! lkn kumbuka Mungu haundi baraza la mawaziri yeye mwenyewe moja kwa moja!hachagui spika na Hachagui wabunge moja kwa moja kwa mfano!hizi ni taratibu walizovuviwa wanadamu kuziweka zisimamie ustawi wao kwa utukufu wake mungu! Kwa hiyo naona ni sahihi kabisa wanawake wnapodai nusu kwa nusu alimuradi wanao ule uwezo unaotakiwa kudeliver! Wasipewa au kunyimwa nafasi vile tu wao ni wanawake!
Yohana K Mwakisole I have learnt that, woman came out from man's rib, not from the feet to be sepped on, not from the head to be superior, but from his side to be equal under the arm to be protected and at th heart's side to be loved.
Sikujua kama ni siku ya wanawake ila nimejikuta at the end nimemnunulia wifey zawadi aliyoipenda.
Nadhani siku ya wanawake ni njema kwao sana tu ila wasizidishe sukari kwenye mboga maana seems wanataka uhuru zaidi ya uhuru. Wakumbuke kwamba... man hatobeba ujauzito heheheheSee More
Oswald Bankobeza BRO;NADHANI TULIOOA ITUKUMBUSHE KUWAPA FURSA YA KUONYESHA KWELI USAIDIZI WAO KWETU.KITU KINACHONIFURAHISHA NI KWAMBA MOST OF THEM ARE FIRM IN DECISION,FOCUSED,BEST ADVISORS AND SO MUCH MORE-GIVE THEM OPPORTUNITY
Bottom of Form
Bottom of Form

WORKING WITH AND FOR THE PEOPLE: HAVE THE ACTIVISTS DONE ENOUGH?


Maalum kwa wanaharakati (special to activists):
Nimepewa mfano jana, eti mwanaharakati mmoja wa masuala ya sanitation nchi jirani, akawaonea huruma mabinti kwenye shule za sekondari, akajitolea kuwanunulia sanitary towels aka always; alipoanza kuzisambaza na kuwaelekeza namna ya kuzitumia, akastaajabu walipomwambia hawana chupi! wajifunza nini?
Top of Form
Paul Celestine namna tofauti za fikra tofauti kwa watu tofauti katika miktadha tofauti kuhusu mada tofauti na kwa malengo tofauti!
Saimon Kajiba this is the silias case
Magdalena Sylister hahaaaa ! yako mengi sana ya kujifunza - kwamba hao wanafunzi walidhani huyo mfadhili ni Mungu wao kwamba awape kila kitu badala ya wao kushukuru kwa walichopata then kufanya bidii binafsi kutafuta kufuli.
Adam Gwankaja ha ha ha haaaa, Maggie, ngoma ikawa wanazitumiaje? na 'madenti' wafanye juhudi gani binafsi kwa mfano? ukitaka kumsaidia mtu unaanzia wapi?
Saimon Kajiba lakini c jukumu la serikali kuwanunulia nguo za ndani ni wao na walezi wao.....sasa serikali ishughulike na mambo ya msingi tu na sisi jamii tukijitolea kuwahudumia hawa wenzetu wenye mahitaji
Adam Gwankaja ‎@Saimon, hapo serikali iweke tu pembeni kabisaaaa. Mtathimini huyo mfadhili, mabinti na jamii yao.
Negwako Mwakibinga ni huruma!!!!!!!!!!
Saimon Kajiba ebu nijuze nchi gani hiyo? labda ndo utamaduni wao kutokuwa na nguo hizo kama wenzetu wa kaskazini
Saimon Kajiba JAMANI EBUU TUSHEE WOTE NENO HILI: VIGEZI MAANA YAKE NN KWA KISWAHILI?
niwie radhi mwanaharakati adam kuwa nitajaribu kuchangia mfano wako kwa kutoa picha pana zaidi na halisi.mfano huo unaweza kutusaidia kujifunza na kujitambua kwenye yale tuyafanyayo leo.Jana serikali 'imemwaga bajaji za kisasa'kwa ajili ya ...kubebea wake zetu wanapokuwa wajawazito.Hivi bajaji hizo zitapita njia gani kule loliondo,maneromango,nkasi,kishapu,na sehemu nyingine ambako njia zitumiwazo hata ng'ombe anapita kwa shida?ndiyo yaleyale ya kugawa always kwa mabinti ambao maskini ya mungu hawana chupi za kushikiza.Siye watanzania tunagawiwa sana 'always' lakini serikali inajifanya haijui kuwa hatuna chupi.tulizonazo ni kama zile za enzi zile za kukatika katikati zikapanda kiunoni.

Nimesomeka eee!
Elias Loidiso Hapa Emmanuel na Adam lakujifunza ni kuwa jambo lolote tunalohitaji kuisadia jamii ni vyema tukaishirikisha jamii husika. Hawa mabinti wangeulizwa pengine wangesema uhitaji mkubwa walionao ni chupi kuliko sanitary towels.hata serikali mara nyingi inanunua ped kumbe watu hawana chupi!
Emmanuel Lema hata pale bei za vitu zinapopanda hovyo lakini kiongozi anatuambia tena kwa kujigamba eti tatizo siyo sera mbovu ni mtikisiko wa kidunia.Kwanza kumbe anajua fika sera ni mbovu.Asichotaka tuamini ni kuwa hatuna mfumo wa kutupatia chupi za uhakika matokeo yake tunadanganywa kwa pedi tena mbaya sana pedi zenyewe tunapewa wakati ule tukiwa katika hali ile tena kwa nia ya kutuhadaa.
Erasto Golyama Kilowoko hahhahaa aaaa, wewe Adam, bado hujapona tu
‎@Emmanuel na Elias, mmelidadavua vilivyo hili suala. ni kweli, hata katika ulimwengu wa harakati, unashangaa tunaendesha kampeni za ushawishi na utete kwa kundi fulani, only to find, wao wanapenda hali ilivyo. wahusika wanajua mahitaji yao.... Habari hizi ndizo zinazofanya interventions nyingi kama za malaria kwa kugawa net, tunaishia kutumia net hizo kuvulia samaki au kuhifadhia kuku/vifaranga dhidi ya mwewe!!! aibu kwa taifa kama letu!

@Erasto, kumbe kweli bado hujapona, maana usingesahau kuwa mie sikuwa kwenye kundi moja nawe, ila tulikupeleka tu wewe!! enewei, its promising, unaelekea kupona!See More
Beatrice Machaga ‎@ inaonesha jinsi gani wanaharakati wanavyokupukia kutatua tatizo bila kuangalia visababishi vya tatizo. lakini adamu hujatulia mifani gani hiyo?
Adam Gwankaja Haswaaaaaa@Beatrice! Hiyo ndiyo mifano yenyewe! Niseme na ile mingine inayokuhusu wewe moja kwa moja!!
Beatrice Machaga chonde chonde kaka usiseme hiyo!
Benedict Kayombo Haaaaa!!! kumbe usiri ni kila mahali?
Adam Gwankaja Habari ndiyo hiyo @Benedict! Istoshe sio usiri, ni kuchuja tu habari! Usikonde Betty, mi thithemi maana hayapo! Tehe teheeeee!
Benedict Kayombo Ndio maana tunapenda kusikia ya wenzetu na siyo ya kwetu kusikika na wenzetu. Inanikumbusha mbali kwa binti "ADELLA" wa Mrisho Mpoto.
Adam Gwankaja Benedict, na hapo ndipo neno umbea lilipoanzia. Hebu sema yako hapa kaka kiongozi!!!! tehe teheeeee umekomaliiiiiiia ya Betty (wala hayapo!!!) tehe teheeeeeeeeee
Benedict Kayombo Teh!! Tehhhhh!! Rudia posti yangu ya mwisho kabla ya hii, kuna maneno hapo!
Adam Gwankaja haswaaaaa nshaikamata ndiyo nikaandika haya. kama tungependa yetu yasikike neno umbea lingekuwa msamiati adimu, ama vipi?
Benedict Kayombo Haswaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!
Mjadala kwenye kuta za FACEBOOK.
Bottom of Form

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP