Pekua/search

Tuesday, October 23, 2012

Daudi Mwangosi: sasa ninakuanika- A tribute

 NAMBA ZAKO


Na Evaristo Haulle
Daudi jina mwangosi, sasa ninakuanika,
Kwa ugumu si wepesi, Jinalo linatukuka,
Kwa bomu tunaakisi, damuyo ilomwagika,
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Ya kwanza ni namba yako, Tanzania mwaka huu
Ya kwanza ni namba yako, miaka yote na huu
Ya mwandishi namba yako, kupata ushenzi huu
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Nne sita namba yako, jeshi kuua nchini
Tatu tisa namba yako, wa mwaka hu si mwakani
Mwandishi ni namba yako, kuuwa duniani
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Mbili saba namba yako, mwezi twataja julai,
Efu mbili namba yako, sita tunaijumui,
Siku hii namba yako, taufik wabilai,
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Myaka sita namba yako, twakuona luningani,
Sijachoka nambayako, ripoti chaneli teni,
Ni ya kwanza namba yako, Iringa kutubaini,
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Wakamia namba yako, wadhani unafaidi,
Saa nne, namba yako, kalamu isowazidi,
Watimiza namba yako, nyororo huko Mufindi,
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Thelathini namba yako, moja ndio januari,
Kuzaliwa namba yako, mia-kenda twakariri,
Saba-mbili namba yako, uhai ulikabiri,
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Mbona ndogo namba yako, miaka arobaini,
Washuruti namba yako, umri wako duniani,
Isitoshe namba yako, ukweli twaubaini,
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.


Na tatu ni namba yako, watoto ulowaacha
Mbili tisa namba yako, tarehe ulotuaga
Ishirini namba yako, kumi-mbili mwaka funga
Damu daudi mwangosi, Haito mwagika bure.

Chanzo: Blog ya ULIZA TU  

Monday, October 22, 2012

Mfumo DUME hauna UUME wala NDEVU



Mfumo DUME hauna UUME wala NDEVU

Mambo yalikuwa hivi mkutanoni. Mama Sofia Simba kwambali kama anatamani kuinuka vile. Picha toka ukuta wa fb wa gazeti mwananchi.

Ukiiangalia picha hii na ukifuatilia kwa karibu zogo lililozuka kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) huko Dodoma,unapata picha kwamba MFUMO DUME umetawala maisha yetu Watanzania na ni hatari zaidi maana kuuondoa hakuishii tu kuongeza idadi kubwa ya wanawake kwenye nafasi za maamuzi.

Ningetarajia kuuona MFUMO USAWA ama basi MFUMO JIKE katika uchaguzi ule. Lakini kilichotawala pale ni mfumo dume uliopindukia ule unaofanywa na wanaume. Kitendo cha kutaka baadhi ya watu tena wenye dhamani WASIHOJIWE na WASITOE MAELEZO kwa wajumbe, kitendo cha kutaka wajumbe WANYAMAE Ndiyo hasa MFUMO DUME wenye. Mfumo dume kwa sifa zake na rangi yake halisi sit u kule kupendelea wanaume katika kufanya maamuz na katika kupata na kutumia fursa, bali ni mfumo NYAMAZISHI, HODHI usiotaka HOJA bali AMRI.

Mjumbe kamuuliza mgombea amefanya nini ama juhudi gani kukiimarisha chama chao? Hilo linaletaje zogo? Badala ya kujibu hoja na kuwafahamisha wajumbe mgombea anarusha vijembe juu ya uchanga wa muuliza swali...’mgni huyu...hajui tulichofanya...JAMANI SI NDIO MAANA ANAULIZA? Kama kawaida yao wapambe wamekuwa mstari wa mbele kutaka kumnyofoa macho mjumbe aliye hoji..huu ndiyo mfumo dume hasa. Mfumo usiovumilia fikra tofauti na mawazo mbadala.

Mlioko kwenye harakati dhidi ya mfumo dume hamna budi kuutambua mfumo huu vizuri..hauna ndevu wala uume..ni mfumo unaowaumiza wanawake kwa wanaume sawia..hata baadhi ya wanawake wanautumia mfumo huu kuwaumiza na kuwakandamiza wanawake wengine.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP