Pekua/search

Monday, July 23, 2012

Tumefanikiwa kuwakinyamazisha walimu matokeo tumeyaona...Tunajaribu Madaktari


Tumefanikiwa kuwakinyamazisha walimu matokeo  tumeyaona...Tunajaribu  Madaktari

  • Walimu wakinyazishwa matokeo yake wanafunzi hawafundishwi wala kusaidiwa kujifunza. Tumefanikiwa katika hili. 
  • Sasa Serikali inajaribu kuwanyamazisha madaktari....Kwanini hatujifunzi?  
Mwl.Makini angependa wanafunzi wake wajisaidie kwenye choo bora zaidi ya hiki

Nimesoma post ya Rafiki yangu wa mtandao wa Facebook, Mh Ahmaed Lukinga akihoji iwapo Walimu mkoa wa Singida wako kwenye mgomo, “SINGIDA WALIMU WAMEGOMA?” Anauliza, na kuendelea kuifafanua hoja yake kwa kutupa mfano wa mojawapo ya shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa mock kidato cha nne mwaka huu.

Anatupasha kuwa shule hii iitwayo Ntonge imekuwa ya 20 kati ya shule 124 za mkoa mzima wa Singida na anatanabahisha kuwa shule hiyo imekuwa na matokeo kama ifuatavyo:  
Daraja la I=0
Daraja la II=3
Daraja la III=6
Daraja la IV=17
Waliofeli kabisa=2
Zaidi Rafiki yangu huyu aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu anahoji, “KAMA MKOA MZIMA UPO HIVO UNATEGEMEA VIWANGO GANI VYA UFAULU KATIKA MITIHANI YA TAIFA KIDATO IV MWAKA HUU?” na kuongeza, “Hii ndiyo hali halisi, Watanzania wenzangu. Mwl. Ahmed Lukinga.”

Mwl. aliyenyamazishwa hajali kufundisha ktk darasa kama hili

Nikiwa nawaza kwa sauti najikuta kupata hamasa ya kujua zaidi...naishia kujiuliza tu.. hivi kama shule hiyo yenye wanafunzi wasiozidi 30 inafanya hivyo je shule zenye wanafunzi 100 hali ikoje? Lakini zaidi ikiwa Ntonge ni shule ya 20 kati ya 124 je shule ya 100 imekuwa na matokeo gani?

Narudi kwenye swali la msingi la Rafiki yangu Lukinga, nadhani si kwamba walimu wamegoma.. kunao ushahidi wa kutosha kubainisha kwamba walimu WAMENYAMAZISHWA. Waliposema hali yao ni mbaya kiasi kwamba haiwavutii kuendelea na kazi, tuliwapuuza na kibaya zaidi tuliwatishia maisha.. mkulu wan chi alisema wakigoma watakong’oliwa ‘waende kwenye meza ya mazungumzo wakiwa na bandeji na ngeu.’

Baada ya kufanikiwa kwenye kuwanyamazisha walimu sasa serikali iko makini kweli kweli kuwanyamazisha madaktari. Wasiseme, wasihoji achilia mbali kudai chochote...inawalekeza kuwa meza ya majadiliano ndio mwarobaini lkn katika hali ya kawaida wakiidai hiyo meza wanatishwa na kutishiwa maisha. Madaktari wanapaswa kuwa wazalendo...wanasiasa uzalendo wanaweka pembeni. Naami

Naam, Walimu wamefuata ushauri wa rais, wamekuwa mbayuwayu...hawajagoma wala kuandamana..na kweli wamepona, hawayajawakuta ya Dkt Ulimboka...ila hali ya elimu imekuwaje? Hata hivyo tumepata nafasi walau hii ya kuhoji na kujihoji. Lakini tunapojaribu kuwanyamazisha madaktari.........NATUENDELEE KUISHANGILIA SERIKALI.
Mwalimu asiyenyamazishwa huwa na ari na ubunifu unaotakiwa kutengeneza na kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia


0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP