Pekua/search

Monday, January 31, 2011

MJADALA WA MALIPO YA DOWANS KAMA MOTO WA NYIKA

Suala la watanzania kutakiwa na mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kibiashara (ICC) kuilipa kampuni tata ya ufuaji umeme nchini DOWANS karibu sh bilioni 100, limemgusa kila mtanzania kwa namna tofauti. Yafuatayo ni majadiliano ya wadau mbali kwe nye mtandao wa internet kama yalivyoanzishwa na Mimi Mwanakijiji. Uhariri mdogo umefanyika ambapo ni picha tu zilizoondolewa, mawazo ya wachangiaji yamebaki kama yalivyo. Soma, shiriki mjidala hii ya kitaifa.



Mtu mmoja anifafanulie utimamu wa watawala wetu: Majenereta ya Dowans kama tungeyanunua sisi wenyewe moja kwa moja yangetugharimu kama dola milioni 60 tu, yakawa ya kwetu wenyewe (tanesco). Hakuna cha capacity charges wala upuuzi mwingine. Lakini sasa kesi hii ikiisha kabisa tutakuwa tumelipia karibu dola milioni 170!!.. talk about the classical def of insanity!
Top of Form
Thomas David Maqway tz shamba la bibi...wewe vuna utakavyo...
January 27 at 11:58pm · LikeUnlike · http://static.ak.fbcdn.net/rsrc.php/yF/r/tddUIK01p63.png1 personLoading...
Steve Mushi dah!haya ya dowans yamekuwa dowaz!ila serikal ingeruhu ushindani wa mashirika katika swala ili la umeme!nadhani hata haya mambo ya ufisadi yacngekuwa mengi hv!tatizo shrika ni moja na kila mmoja anataka kula hapo hapo!
January 27 at 11:59pm · LikeUnlike
sasa wangekula wapi?.. 10% ya kutoa tenda,posho za kikao cha kufungua tenda,posho ya kikao cha kuteua mzabuni,posho na vitafunwa vya tafrija ya kusaini mkataba na mzabuni aliyeshinda(richmond),dili za kuipamba dowans kwenye vyombo vya habar...i(salva na washkaji zake),posho za mjadala mrefu bungeni,milioni 400 za kamati ya mwkyembe,ada ya za ushauri wa kitaalam SANA kutoka kw mtaalam mwelekezi na mjuzi wa sheria za mikataba ya kimataifa,rex attonneys(kabla na baada ya kuvunja mkataba),malipo ya wanasheria walioiwakilisha serikali/tanesco huko icc pamoja na nauli zao,malazi,makazi na matumizi yao mengine ya kawaida,cheap popularity(uvccm)!... na mengine mengi yajayo!..See More
Malare Murilo  Zitto Z.Kabwe aliona kitu hapo mwanzo na kuishauri serikali kununua tu hiyo mitambo,reason was "KWA MASLAHI YA TAIFA" lakini pia kwa upande mwingine sheria ya manunuzi hairuhusu kununua mitambo ambayo tayari ni mitumba/iliyokwisha tumika..Sasa kwa kiongozi timamu na mwenye busara katika hili ni bora mara mia sheria ikapindishwa kwa maslahi ya taifa
Friday at 2:20am · LikeUnlike · http://static.ak.fbcdn.net/rsrc.php/yF/r/tddUIK01p63.png3 peopleLoading...
There is collective amnesia among us. The same people waliokataa kununuliwa kwa mitambo, wakataka mkataba uvunjwe ndio leo hii wanapiga kelele kwamba Dowans wasilipwe! I'm talking about Sitta, Mwakyembe et al. Hi kwanini hakuna anayewakumbu...sha msimamo wao huu leo hii? Walimvuruga sana Zitto on this one, pamoja na Kamati yake ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma. Leo hii eti they are the heroes? Tuache unafiki Watanzania. @Malare - Waiver ingeweza kupatikana ili kuepuka hiyo sheria ya manunuzi ya mitambo mitumba, lakini hiyo haikuamliwa, badala yake wakina Sitta walipinga wakidai ununuzi huo utanufaisha mafisadi. Ujinga mtupu, halafu watanzania bado tunashabikia tu, mxiiiSee More
Nate, nadhani unasahau kwanini (mimi nikiwa mmojawapo) tulikataa mitambo isinunuliwe toka kwa Dowans; siyo isinunuliwe kabisa. Option iliyokuwapo ilikuwa ni ya kutaifisha mitambo ile - nilishalizungumzia hili mwenyewe kwa kirefu huko nyuma.... Now, tungeitaifisha kwa sababu za kisheria ambazo zilikuwepo wakati ule siyo Dowans wala nani ambao wangeweza kulalamikia.

Sidhani kama Mwakyembe au Sitta walikataa mitambo isinunuliwe toka kwa watengenezaji lakini of course hata leo hii bado wengine tunapinga siyo tu kulipwa Dowans lakini kununua mitambo hii hii. Now, ni wazi kuwa kama watendaji wetu wangejua kunegotiate vizuri baada ya kuvunja mkataba tungewaambia tutanunua at a fair market value lakini na nyinyi mnapoteza haki ya kutudai mahakamani. So, Dowans wanakubali tuvunje mkataba lakini tukanunua toka kwao kwa bilioni 60 whichi is thefair market price.

Lakini, siyo Taneso wala serikali waliyotaka ku a. renegotiate terms za contract toka mwanzo - mkataba wa Richmond ulirithiwa na Dowans bila ya modification yoyote licha ya kuwa mazingira yaliyosababisha kuingiwa mkataba ule in the first place yalikuwa tayari yamebadilika. Dowans wakarithi mkataba ukiwa na masharti yale yale ya ajabu!

b. Na Tanesco walipokuwa wanapanga mpango wa kuvunja mkataba hakukuwa na jaribio lolote la kurenegotiate terms za kununua majenereta yale au vinginevyo. Sisi tulivunja tu. Lakini hivi sasa ukiniuliza mimi the only option ambayo inawezekana ni hiyo ya kujaribu kila pande ifanikiwe kwamba Dowans waanapewa uchaguzi mmoja tu. Ondoka na majenereta yako ukauze kwingine lakini hatukulipia hata senti moja ya ziada, tutanunua majenereta mapya.

Did you notice kwamba hilo "tuzo" ambalo leo tunatakiwa kulipa ni dola milioni 61 hivi (market price ya majenereta hayo) lakini tukiwalipa bado wao wanakuwa na majenereta hayo na wanaenda kuuza kwingine (San Antonio) kwa dola milioni 60 nyingine?

Kweli kuna makosa yamefanyika huko nyuma lakini hatuwezi kuendelea kufanya makosa au kuzawadia makosa mengine kwa sababu hiyo. Somebody need to show some leadership na bahati JK inaonekana hana nia au uwezo huo kwa wakati huu.See More
What we are dealing with is not just bad judgement on part of certain leaders, particularly political leaders, but also we are graping with good governance and rule of law issues. Kutaifisha sio good governance, na implication yake katika m...azingira ya dunia ya leo sio sawa na enzi zile za Nyerere. Kwahiyo sikubaliani na kutaifisha, kwa vile athari zake ni kubwa zaidi. Rule of law ndio hiyo ambayo inatulazimu kwamba tukubali maamuzi ya arbitration. Leo hii, mashabiki wa rule of law and good governance are advocating for utaifishaji na kugoma kulipa pale tunaposhindwa kesi kwa makosa yetu wenyewe! Quite interesting indeed. At any rate, nakubaliana na wewe kwamba mkataba wa Richmond unngekuwa renegotiated hata kabla ya Dowans kuwa kwenye picha. Hilo lilikuwa kosa la pili, la kwanza likiwa kosa la kuipa tenda kampuni ya Richmond ambayo haikuwa na track record yoyote. Pili, nani aliyeshinikiza mkataba uvunjwe tu bila ku-renegotiate? Naamini wahusika ni Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini (Shelukindo, Mwakyembe) wakiungana na Spika Sitta. Wao ndio walibeza ushauri wa Kamati ya Mahesabu ya Mashirika ya Umma (Zitto), na wakajenga hoja mbele ya wananchi, wakisaidiwa na wanaharakati kama kina Mwanakijiji, kwamba tutashinda kesi ikiwa tukivunja mkataba bila ya ku-renegotiate kwa vile eti ule mkataba na Richmond ulikuwa kinyume na kanuni za procurement. Mkataba ulipo-huishwa Dowans, hiyo ilikuwa kati ya makampuni binafsi, kwahiyo huwezi kuuliza kwanini haukuwa re-negotiated (serikali haihusiki katika business to business deals). Mwisho, kweli tunahitaji na negotiated settlement to this that makes Dowans "whole", as perhaps finding them a new buyer who will pay them what we have to pay. Something along that line. Lakini tafadhali usiniletee haya mambo ya kuwasafisha kina Sitta na Mwakyembe katika hili. Wao wanahusika sana katika kuwavuruga TANESCO na Wizara na kuwafanya wafanye maamuzi mabovu kwa Taifa.See More
Stephen Seyayi It seems to me that this whole mess is due to consistent political meddling. Politicians have too much power and influence in this country. Political influence was used to get into the richmond deal, then to transfer the contract to dowans. When the technocrats at Tanesco tried to salvage the situation, politics interfered, i.e kukataa mitambo isi nunuliwe. Hawa wanasiasa na mfumo mbovu kabisa wa siasa ndo unao tukwamisha. We will never progress, under the current political system.
Nate, kutaifisha ni sehemu ya sheria yetu; unapozungumzia "rule of law" sipendekezi kitu chochote nje ya sheria yetu. Tunapozungumzia kutaifisha nazungumzia "seize" them siyo "nationalize" kwa maana ya Arusha Declaration of whicho some peop...le find a little bit offensive. Seizing a product is not out of the ordinary; its part of the legal process even here in the US (a classic example is the Mardoff case). So, claiming is "not good governance" is not true; I'll argue in fact it is indeed part of "good governance". Corruption can not be tolerated and able leaders must not be afraid to take proper action when it is warranted.

Mimi ni miongoni mwa watu wachache ambao sikuamini tunaweza kushinda kesi mahakamani kwa sababu the arguments presented from the beginning were not purely legal but more political. Lakini, ni kweli kabisa sikuamini wakati ule kama vile nisivyoamini sasa kwamba tulishindwa kuikamata mitambo ile baada ya ushahidi toka awali wa improper process toka mwanzo.

Kinyume na unavyosema ripoti ya Mwakyembe mapema kabisa (kama umechukua muda kuisoma) utaona kuwa ilikuja mapema 2008. Ilifanya kazi yake na kuuliza maswali yote muhimu na ilifinua the process of meddling toka mwanzo wa tenda ya Richmond. Kuwalaumu kina Mwakyemba na Sitta kwa mkataba wa Richmond na Dowans ni kujaribu kukwepesha lawama wka wahusika wenyewe yaani lowassa, Karamagi, Kikwete, Rostam Aziz na watendaji wa sehemu hizo ambao toka mwanzo walitaka Richmond ipewe mkataba na toka mwanzo waliipanga Dowans kuchukua mkataba huo no matter what.

Mkataba wa Richmond ulipelekwa kwa Dowans S.A kinyume cha vifungu vya mkataba huo kabla ya tume ya mwakyembe haijaundwa! Walioingia mkataba huo na kuandika ni serikali ya Kikwete na watendaji wake na siyo kina Mwakyembe; walioweka masharti mabovu ya mkataba huo ni kina Mwanyika na mawakili wa wizara ya Madini na Nishati siyo kina Mwakyembe!

Baada ya ripoti ya Mwakyembe kutolewa tulitegemea wahusika wangechukua mapendekezo yake mara moja na kuyafanyia kazi lakiini hawakufanya hiviyo. Sasa hadi mkataba unavunjwa baadaye na kamati ya Zitto na ya Shelukindo zilipogongana ni kwa sababu waliotakiwa kuchukua hatua hawakuchukua na tunajaribu kuwaexcuse na kubebesha lawama kwa watu walioibua udhaifu mkubwa wa serikali ya Kikwete!

Haya yatakuwa ni maajabu ya mwisho. Yaani, tufumbe macho uzembe wa JK na watendaji wake halafu tuwabebeshe zigo kina Mwakyembe na Sitta kwa sababu walipinda ununuzi wa bidhaa ambayo wao wenyewe walihoji toka mwanzo! I don't buy that.See More
MwanaKJJ, wala sijamaanisha kwamba tufumbe macho uzembe wa JK au wa Ngeleja au Karamagi et al katika hili. Nilichosema ni kwamba the attempt kuwasafisha Sitta, Mwakyembe na Kamati ya Shelukindo is not right EITHER. These guys were motivated... more by their political enmity within CCM factions than anything else, ndio maana hata suggestion ya kununua mitambo wakai-frame along political lines instead of expert opinion iliyoshauri mitambo inunuliwe. Makosa yaliyofanywa awali na Lowassa, Karamagi, Ngeleja et al yakawa doubled-down na makosa ya kina Sitta na Mwakyembe kwa ushabiki wao wa kisiasa. Lakini leo hii kina Sitta na Mwakyembe wana behave as if they did nothing wrong, kwamba wao wapo pure katika hili, na hawaoni they bear any responsibility. Thats nonsense. The guy who was right (Zitto) maskini he is still being demonized - that time by Sitta and Mwakyembe's gang, now by the entire Chadema apparatus! Read this: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=9467See More
But on your first argument you didn't even mention the people who are in fact more responsible in the whole mess. But, at least these people Mwakyembe and Sitta have the courage of trying to correct their mistakes (as u suggest them) while ...the true culprits of this of this remains silent!

The Zitto case is purely politics and for me I don't see it a big deal at all. I disagreed with Zitto on that point and I said to him and I came to his defense publicly (I wrote an article in his support) when everybody was against him.To me it was merely a matter of political differences. I would not describe differing with some body's politics kuwa ni "demonization" otherwise wengi wetu tuko demonized mara nyingi kwa sababu tunatofautina na watu wengine.

Zitto is a politician and he must be willing to pay the price of his political position and so is Mwakyembe and Sitta as well as Kikwete and the rest of them.

But still you are putting a whole lot responsibility on Mwakyembe and Sitta but not on Kikwete, and the people who put us in this mess in the first place, I think thats not fair. We wouldn't be here if JK, AG, Karamagi, RA, etc wangetimiza wajibu wao kwa weledi unaotakiwa. Wao ndio wanastahili kubeba lawama hii.

Whatever Mwakyembe and Sitta did pale in comparison to what JK and the group did. Unless of course you don't think Mwakyembe and Sitta bare more responsiblity than the government itself.See More
Biwi Wa Malima ‎@Wananchi hii yote uhuni tuu kuna watu wamekatana cha juu sasa wameamua bora liwe zogo na ugomvi wa tembo ziumiazo ni nyasi
Friday at 6:16am · LikeUnlike
‎@MwanaKJJ, Tofauti ni kwamba Sitta na Mwakyembe are populist, they are making public statements showing outrage without admitting their part in the mess, conveniently. That is not courage, its populism tu, there is no other word for it. On... the other hand, yes the Govt is for the most part silent (which is not helpful), but internally they are admitting the mistakes. Unfortunately we are not seeing anybody being made accountable, which is sad. But really the Govt is at the same time grappling with means of resolving this mess according to rule of law (not politically), to the utter frustration of the citizenry! The political ruse that Sitta's gang has thrown in the air is so thick, the Govt will have to succumb to it sooner or later. The people now want the Govt to find a political solution, not a legal one. What makes you believe that what today Sitta and Mwakyembe are advocating (not to pay Dowans) will not just cause us even more money in terms of fines and legal fees down the road? Your idea that "seizure" is not "nationalization" is just semantics to for the business environment (in America, the word "nationalization" is never used, so its really the same thing in principle).See More
Nate, politics is an art of populism and manipulation.. You are saying "On... the other hand, yes the Govt is for the most part silent (which is not helpful), but internally they are admitting the mistakes. " I'm more than disappointed if ...that is the case. Why is the government silent? By this you mean JK, and the others or some junior members of the gvt?

Nate, in America of course they don't say "nationalization" when they seize private propert.. but is the same thing.. at least we had the courage to give it the proper name. Seizing private property for the benefit of the state is nothing but nationalization..

Saying that "Unfortunately we are not seeing anybody being made accountable, which is sad."

But who is supposed to make people accountable in the government? Why can't they do it? Why didn't they make these people accountable in the first place. To me Mwakyembe and Sitta and the rest of those courageous MP did was to hold people accountable.

And we are still looking for more responsibility and accountability in this issue.See More
Dunia Dy no, MM. this is not insanity. the correct English word for it is 'CORRUPTION
‎@ Nathan, nashawishika kuamini kuwa "There is collective amnesia among us," see what? ndiyo maana tunaliziro suala zima kwenye Dowans na malipo, na Sitta na mwakyembe kwa kushinikiza kulipa, na wala sio Richmond na mikataba yake ya kilagha...i ama kushindwa kwake kudeliver sawa na mkataba (kwa wakati). Je kina Shelukindo, walianzisha hoja ya Richmond kutoka kwenye ombwe?

Ombwe kwenye utendaji wa serikali na apparatus zake nadhani ndiyo chanzo cha yote haya. Who signed the richmond stuff? what was the interest behind kuukata mfumo rasmi wa negotiations na manunuzi? Nani alivunja mkataba wa dowans pasipo legal prudence.

On the whole issue of whether there is or no political interest of Sitta na Mwakyembe ni propaganda zile zile zinazoturudisha square ziro! How powerful were they to influence/force the government do what it did? Why didn't the same, not work to force Hosea, Mwanyika and Mwakapugi out? WE ARE OVERLY SIMPLIFYING THINGS, NADHANI.
Did Sitta and Mwakyembe, force the government pick and trumpet for the law firm it picked?See More
According to my vision, 2cpoweka balance kati ya siasa na taaluma mambo hya ytaendlea klitafna taifa le2 cku zote. Na hii yote tkana na maamuzi ya kisiasa kuwa na nguvu zaid kliko yale ya kitaalam, hvyo bac ktokana na dili la kisiasa kuwa n...a nguvu kma mgodi wa dhahabu, wataalam we2 pia wmejkuta wakvutwa na kma cyo kuwa waoga bac kutmbukia kwenye mchezo mchafu wa kuwatengnezea dili watawala we2. Kwa kusema hyo cna mana ya kuikata siasa, kwa kuwa nachoweza sema hpo ni kwamba "political is every thing" kwa vile wanasiasa ndo wanaokaa mjengni na kpanga mstahakabal wa taifa ila 2 ninkubaliana na ile political system ambyo haiinglii masuala ya kitaalam kwa kuacha masuala ya kitaalam kuchkua nafac yake. Na mwisho uwepo wa mwanasheria mkuu wa gvt pale mjengni uonyeshe tofauti na cyo 2 kuungana kugonga zile meza hta kwa masuala yacyo na tija kwa taifa. See More
Nathan Chiume Sitta na Mwakyembe wana uchungu na wapinzani wao ndani ya CCM kwa vile wanaamini (fact or not) watapata chapuo kutokana na malipo kwa Dowans. Tuseme ukweli jamani. Ndio maana hata walipinga ununuzi wa mitambo, kwa sababu hiyo hiyo. Wote wanasiasa wetu, wa pande zote ndani ya CCM, na wapinzani kwa ushabiki wao wametufikisha hapa. Hii ya kujaribu kuweka lawama zaidi kwa watendaji wa Serikalini kwa makosa yao bila ya kuangalia makosa ya wanasiasa baadaye sio sahihi hata kidogo. My 2 cents.
Hatusemi lawama kwa watendaji tu tunasema lawama kwa Rais Kikwete, Waziri wake wa Nishati, Mwanasheria Mkuu n.k. Tuwataje hawa kwa majina kama tunavyowataja hawa kina Mwakyembe na Sitta kwa ukali huo huo. Tukikubaliana kuwa wote wanawajibik...a tutakuwa sawasawa, tusiwaite wengine kwa majina yao na wengine kuwapa euphemism ya kuwaita tu "watendaji". Kila mmoja kwa kiwango chake of course kaboronga mahali fulani lakini kuna walioboronga zaidi ni watendaji.

Kama inavyosema hapa the bucks stops with the president.See More
Nathan Chiume Na wewe inaonekana hupendelei Sitta na Mwakyembe wakitajwa. Jibu swali fupi tu - nani alaumiwe kama sio Sitta na Mwakyembe kwa kushinikiza TANESCO isinunue mitambo? (rejea mada yako uliyoanzisha mwenyewe).
Nikisema walaumiwe nitakuwa ninassume msimamo wao haukuwa sahihi. Kwa hiyo, jibu langu ni kuwa wanaotakiwa kulaumiwa ni walioliingiza Tanesco kwenye mkataba huo wa Richmond/Dowans. Katika mazingira yale mitambo ile isingepaswa kununuliwa na... Tanesco ingekuwa ni kuzawadia uzembe na kutuza ufisadi.

Labda na wewe ujibu: Nani allaumiwe kwa kuiingiza Tanesco katika mikataba hii mibovu na kushindwa kuwawajibisha wahusika?See More
Exaud Mshana Nathan, kama rais wetu angekuwa makini na kutekeleza wajibu wake kwa weledi tusingekuwa na mjadala huu. Tukubali ukweli, tuache propaganda zisizo na maana. Tuseme bila kuuma maneno, Kikwete anahusika 100%. Wanaotaka kugeuza kibao kwa Sitta na Mwakyembe, watu ambao walifanya kazi yao kwa usahihi haingii akilini. Tuangalie tulipojikwaa si tulipoangukia.
Nathan Chiume ‎@MwanaKJJ, Exaud - Mimi nalaumu wote, kuanzia Karamagi, Ngeleja, Sitta, Mwakyembe, Kamati ya Nishati na Madini mpaka Rais mwenyewe. Wote wametuvuruga-vuruga tu. Nyie endeleeni kulaumu upande mmoja, mimi narudia tena kwamba nalaumu pande zote - mpaka Upinzani. Viongozi wote wametuangusha jamani.
Mimi Mwanakijiji I like your stand Nate. Tunatofautiana kwenye hilo jingine. Thanks for a good discussion sir.
hakuna anayewajibishwa...chiligati..."tumejifunza kwa kweli,..ni somo tosha..,hatutarudia tena"..."nonsense"...wamekuwa mahakama,....wao ndio wao,...wafanye makosa (wizi,ufisadi,rushwa)...hizo ndizo kauli zinazotamalaki....tunashindwa kuami...ni kama baba yetu....hayuko kwenye hili (10%) kama siyo 100%...coconut country...

tumekosa maadili kupita upeo...hata dhamira zetu zimekuwa mfu mithili ya ganzi....wana wa nchi nao wametekwa....hakuna aliye msafi katika hili....as long as walikuwa madarakani,...na laiti kungelikuwa na maadili ya kitaifa...kila aliyehusika (waliotuhumiwa na waliotuhumu,wanaotuhumu, wanaotuhumiwa,na pia wahanga wa huu ushenzi wote) alikuwa na nafasi pekee (kura turufu) ya kukataa hata mawe yakanena asilani.

sita anafanya nini serikalini....ajiuzulu...wote waliokwepo madarakani wakaruhusu ushenzi huu....waondoke....wawaachie wanaosimamiwa huu ushenzi(ili wapate msamaha wa walipa kodi na watubu kweli kweli)....wakibaki ndani ya nyumba hata kama wakitubu hatutawasamehe mpaka mwisho wa dahari, kwani wao ni moja...See More
Bunge haliwezi kubeba lawama yote kwa maoni yangu. Halikuingia mkataba wa kilaghai na richmond. Halikuvunja mkataba na dowans. Kama lingekuwa na uwezo huo wa kushinikiza hata dkt Hosea wa takukuru asingekuwa kazini. Bunge lilitimiza kazi ya...ke ya kuishauri serikali na serikali ikachagua uamuzi iliyochagua na kwa namna walivyofanya kipuuzi! Lakini tuambiane ukweli hapa, mkataba wa Richmond haukuwa na mushkeli!? Bunge lingefanya nini zaidi ya kubainisha kasoro zile? Na je uhaulishaji toka Richmond 'fake' kwenda Dowans,ulikuwa shwari? Na kesi ya dowans dhidi ya tanesco ilipewa wasimamizi sahihi? Rais wetu mwanasiasa ndiye kiongozi wa maamuzi yote ya kiutendaji ya serikali! See More
Nathan Chiume Tazama Kubenea alivyomshambulia Dr Rashid, Lipumba na Zitto kuhusu kununua mitambo 03/25/09: http://www.mwanahalisi.co.tz/ngeleja_sasa_amwacha_zitto_ulingoni
dhamira zao zinawasuta...sura zao zinaonesha...kilichoko mioyoni mwao tofauti na kinachotoka vinywani mwao...hawa si watu tena...utu wao una mashaka...wameshindwa kutetea maslahi ya nchi yetu...hatuna budi kuwafukuza kazi...from the highest... office of the land to the bottom...maadili hakuna...na hii kansa inazidi kuenea hata kwa watoto wetu...kizazi kijacho kinapata urithi angamizi...ni anguko la taifa...tukinyamaza...tutahukumiwa...na hatutaweza kujitetea kamwe.

ni vema kila mtu kwa nafasi aliyo nayo, kwa namna anavyoweza, kwa jinsi anavyofikiri inafaa kwa upana wake must redress our national moral standing...if you cannot do it no one will...elimisha umma, kwani hawajui, wako gizani na watawala wanafanya wawezalo wabakie huko kwenye kiza tororo wasifahamu kinachotendeka kwa sababu ndiyo salama yao

kama tutanyamaza...basi mawe yatanena...na mimi na wewe hatutakuwa na tofauti na wao...letu litakuwa moja na hukumu yetu itakuwa moja!!See More
Nathan Chiume ‎@Adam - Bunge linaweza kubeba lawama kwavile lilishinikiza TANESCO kutofanya maamuzi ya kitaalamu. Si unakumbuka mpaka Dr Rashid akatahamaki kuingiliwa? Leo hii tumlaumu Dr Rashid?
Thomas David Maqway ‎@adam...bunge ndilo linalopaswa kulaumiwa...bunge(wananchi) ndio msingi wa maadili ya taifa kuporomoka...kwa uwingi wao wamekaa kimya...kwa woga wao...ya richmond wameogopa kutaja kikwete...mwakyembe alificha ukweli na sasa haya ndio matokeo yake....ushenzi huu unaendelea na bunge lipo...hakuna hatua zinazochukuliwa...wale ni wawakilishi wa wananchi, ni watetezi wa wananchi...si waajiriwa wa serikali...wanatetea serikali katika maamuzi mabovu...
Rama S Msangi umetumia neno zuri sana hapo juu kwenye hoja yako. "WATAWALA"...so hukuwa hata na haja ya kuhoji utimamu wao kiakili, kifikra au kivyovyote vile, maana sifa moja ya WATAWALA ni kwamba, ni watu wasiokuwa na ufikiri. wangekuwa VIONGOZI ingekuwa sahihi zaidi kuhoji na kujadili hili
Churchill Shakim naamini wanatumia utimamu wao ili kutuibia...
kwa misingi mingine wako radhi kubomoa nyuma wanayoishi
‎@Nata@Mkjj rejea hoja ya @nata hapo juu nanukuu alivyozungumza "Mimi nalaumu wote, kuanzia Karamagi, Ngeleja, Sitta, Mwakyembe, Kamati ya Nishati na Madini mpaka Rais mwenyewe. Wote wametuvuruga-vuruga tu"

mimi ningewapanga hivi nawapanga k...wa ubora
1)Zito na kamati ya mahesabu
2)Sitta, Mwakyembe,Kebenea na gazeti lake
3)Karamagi, Ngeleja,Kamati ya Nishati na Madini mpaka Rais mwenyewe.

Kwanza nampongeza Zito kwa kukubali lawama na mashambulizi toka pande zote na kusimamia usemi wake wa kununua mitambo ya Dowans.vyombo vya habari ,ndani ya Chama chake,na hata wananchi wengi hawakumwelewa lakini sasa HOJA YAKE NDIYO INAONEKANA BORA.

Sitta, Mwakyembe na kubeneana gazeti lake wanakuwa wa pili kwa kukosa point ya kutokumwelewa Zito na kamati yake lakini tunakubali mchango yao bungeni kwa kufunua waziwazi mikataba mibovu ya Richmond na Dowans ,tujiulize pasipo ushupavu wa mwakyembe na kamati yake na ushupavu wa spika sita leo hii tusingekuwa na nguvu ya hoja ya kuhoji ,hivyo tusiwalaumu hawa tuangalie tufanye nini kujinasua na deni la Dowans maana walilaumu hoja ya kununua wakifikiri watawanufaisha zaidi waasisi wa Dowans hivyo makosa madogo yapo na yamefanyika lakini lengo lilikuwa moja kuiondoa serikali toka kwenye mdomo wa Dowans na Richmd

namba tatu na wamwisho wanajulikana na makosa yao ndiyo yaliyotuletea yote haya.

hivyo tuache kuwalaumu sana Sitta, Mwakyembe na zito tujipange upya kisheria namna ya kujinasua maana Dowans wana roho ngumu hiyo hela wanaitaka kwa nguvu zao zote na sasa hivi wameshawasilisha kesi mahakama kuu na pia wamefungua kesi uingereza,Narudia TUJIPANGE KISHERIA UPYA KUKABILIANA NAO TENA MAANA DOWANS NA WATU WACHACHE WANATAKA HAYO MABILIONI KINGUVU BILA AIBU.See More
Bamdogo Kiki Na kwanini sikuzote hizo mpaka leo hawanunua mengine mapya? wanasubiri wawekezaji?
Egbert Mhada Tusingekuwa na matatizo ya umeme kama haya majenereta yangekuwa yanatumika. Tunaviongozi wasiojali masilahi ya wananchi nchi hii. Unajua Procurement procedures hazijaandikwa kwenye katiba. Nasema mimi ningekuwa Rais wa nchi hii haya majenereta yange kuwa yanafanya kazi na kama wananchi wangeniadhibu kwa hilo basi ingekuwa msalaba. Mhando watch out in this country they always start with a small fish when the going get tough.
Naona baadhi wanapotosha hoja hapa. Matatizo ya nchi yetu yanatokana na serikali kuwa re-active ktk masuala nyeti, kama umeme, badala ya kuwa pro-active. Ufahamu wangu na utashi wa dhamira yangu hautamtupia lawama hata chembe Dr. Mwakyembe ...na Sitta kwa kusimamia uwekaji hadharani hoja ya Richmond.

Hao waliopeleka utetezi wa Tanesco ICC walikuwa na ajenda ya siri. Nachelea kuamini kuwa walipewa maelekezo ili tushindwe kesi, pesa ilipwe na hatimaye Jk + Lowasa na kundi lake wajisafishe na kashfa hii. Pasingekuwa na njia nyingine kwa wao kujisafisha bila kuwachafua kina Mwakyembe. Ktk propaganda hizo za uchafu, wanasahau kuwa yale yalikuwa maamuzi ya kamati teule ya bunge la Tanzania na si suala binafsi la kina Sitta.

Lazima tufahamu kuwa mafisadi wanaandaa mazingira ya kuendelea kushika dola. Mambo haya ni mkakati wa uchaguzi ujao. Wananchi lazima tuhoji, kuna mikataba mingi ya hovyo wahusika lazima wawajibishwe. Ccm haina uwezo wa kuwatetea wananchi, jk hana moral authority ya kuilinda katiba ya nchi hii. Wanaoeneza propaganda zisizo na mashiko wajiandae kulia kwani zita backfire, hali ya maisha ya mtanzania inakuwa ngumu kila uchao. NGUVU YA UMMA PEKEE NDO YA KUISAIDIA NCHI HII.See More
Frank Uhwello Tatizo ni kuwa wanasisa wamekuwa na nguvu kuliko wataalam/watendaji, mbaya zaid wamekuwa wabinafsi wenye tamaa ya kujilimbikizia mali. Inasemekana wataalamu toka TANESCO walishauri tusiingie mkataba na RICHMOND lakin walipuuzwa. Matokeo yake ndiyo haya sasa, nchi inaangamizwa na wachache......
‎@ Mimi Mwanakijiji,kwa kweli uongozi uliopo madarakani ndio uliotufikisha hapa tulipo,ukifuatilia kwa makini,walikuwa na uwezo wa kutuepusha na janga hili la malipo ya kitapeli tunayodaiwa sasa,lakini kwa sababu wanazozijua wao hawakuwajib...ika ipasavyo kwa Taifa.

Nafikiri ni muda muafaka sasa kutaka uwajibikaji toka kwao kwenye suala hili kuanzia Raisi wa nchi na Mawaziri wake waliohusika katika kadhia hii.Kuwajibika kisiasa haitoshi nafikiri kuna haja ya kwenda mbali zaidi na kudai wafikishwe mahakamani na washitakiwe.

Kuhusu Dowans na malipo hewa wanayodai,nayaita hewa kwa sababu tangu mwanzo hawakustaili kupewa mkataba wa uzalishaji umeme japo walitumia nguvu ya Ikulu kupata mkataba huo,malipo hayo yasitishwe na mitambo yao itaifishwe ili kulipia gharama ya fedha ambazo zimepatikana kiulaghai.

Sasa ni wakati muafaka kwa watanzania kuwa makini na viongozi tunaowapa madaraka ya kuiongoza nchi hii kama tunataka kweli kuendelea kiuchumi.See More
MM. The demand by some to know the names of the owners of dowans is it politically motivated? Many would like to hear names of EL, RA, Karamagi and JK mentioned. Why can u tell me? May be Tanzania will be Tunisianised or Egyptianised so th...ey hope. I hear they are meeting in bagamoyo to come up with a strategy to sensitize the public on dowans so that can make people rise against the goverment. Are u aware of that? They thought katiba could be their trump card but it has no impact. Soi? Use the currrent matatizo ya umeme kuwa dowans imesababisha. As u put it "politics is an art of populism and manipulation...." So be it. Right?See More
Exaud Mshana ‎@Majani, am afraid, it seems u ar putting a blind eye on the issue under discussion here. Propaganda cant derail our focus on these issues.
Proches Tairo ‎@ Mimi Mwanakijiji, yangetugharimu kama dola milioni 60 tulakini billl ya kuyaendesha na kuyamaintain ambayo tungeletewa ingeweza kuzidi hata hiyo dola milioni 170. Nafikiri issue hapa ni kwamba did we really need hiyo mitambo in the first place regardless of whether tungeinunua sisi wenyewe or tungecontract out to a thirdy party?
Friday at 1:30pm · LikeUnlike
Frederick Katulanda Kaka hili ni 'AIBU KWA TAIFA' hawatakawia kutueleza Bungeni kuwa 'Hatujadili Dowans..kwa vile ni Usalama wa Taifa' huku wengine wakiapa konokono.
Mimi Mwanakijiji Kapangala Majani, mkutano wa Chadema ni kikao cha kawaida cha Kamati Kuu; mbona Kamati Kuu ya CCM ilikutana siku chache zilizopita na watu hawakusema wamekutana ili kutafuta jinsi ya kuiokoa Dowans na kuilipa? Sasa watu wasifanye vikao halali kwa kuogopa kudhaniwa?
Martha Lema Blood boils in me when i imagine that 60 mil dollars from tax payers money will be awarded to a few greedy immoral politicians (Tzs) who yet have more than enough already (tena waTz wote tunahitaji kuwajua kwa majina) If it were not for Shelukindo/Mwakyembe's team tungeyajuaje haya regardless of their motive, they opened our eyes.
Hamisi Manyanya Only Zitto Kabwe got the right brain at that moment, 'wanaharakati' wakamuona mamluki n now ......? Long live Zitto, in u I now trust!
Hamisi Manyanya Only Zitto Kabwe got the right brain at that moment, 'wanaharakati' wakamuona mamluki n now ......? Long live Zitto, in u I now trust!
Baadhi ya wataalamu pale Nishati niliongea nao mwaka jana wanilieleza wazi kwamba, kwenye majenereta kuna dili,kuanzia mikataba yenyewe hadi mafuta ambayo ndiyo yanaitafuna nchi kwa sasa, na hapo ndipo wanasiasa wetu, tangu kuondoka madara...kani kwa Nyerere wamekuwa wakitumia kujikusanyia pesa chafu. Hii ni kuanzia mikataba ya IPTL.

Na katika mtiririko wa matukio yote hayo hadi Dowans huwezi muepusha JK, huo ndio ukweli.

Kama alivyobainisha Adam hapo juu, Bunge lilitekeleza wajibu wake, sasa niulize tunaolalamika hapa, kwa maana ya wananchi, tulitekeleza wajibu wetu wakati JK akipiga uswahili kwenye maazimio ya Bunge!!! jibu hapana.

Nimechangia mara nyingi na narudia, Watanzania tuache uswahili nasi tutimize wajibu wetu wa kuwawajibisha viongozi wabovu mwanya unapopatikana. Tunisia wameweza, sisi ni kulalama tukiwategemea wachache watufanyie kazi, TUBADILIKE.See More
Kepha Dickson IPO SIKU MBINGU ZITAFUNGUKA NA WATAKIMBIA NCHI KAMA TUNISIA SEREKALI ITAVUNJIKA KAMA MISRI ..!!..
Bottom of Form

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP