Pekua/search

Tuesday, May 24, 2011

KUELEKEA KUSINI MWA TANZANIA: HII NAYO NI BARABARA- Dkt Magufuli aendelee kutumia utu!

Hii pia ni barabara:kipande cha Marendego-Somanga katika barabara ya Dar - Lindi - Mtwara.Ni sehemu ya KM 60 za barabara ambazo ujenzi wake umesuasua kwa miaka sasa
Top of Form
May 16 · Like · Bottom of Form
Asifiwe Alinanuswe mbunge wetu tulimpitisha kwa kishindo,, rais wetu tukampa kula, diwani akajpitia kiulaini,, nitahakikisha watu wanasafiri kwa tax toka kusini kwenda kaskazini,,,,
May 16 at 1:07pm
 
Adam Gwankaja Eeee@Asifiwe si ndo kama hivi twasafiri kama hivyo!
May 16 at 1:40pm
Last Hisia Kali ‎....Halafu mkishatushibisha leteni kelele zenu kwa wingi ztubembeleze!!....huwa tunapata usingizi mzuuri kweli kweli wala hata hatuoni bughudha!!.....na kiitikio chetu kitakoleza na kupambiza vema kelele zenu za kubembeleza.....NAKUPENDA TANZANIA!!!
May 16 at 2:09pm ·
Asifiwe Alinanuswe haya ndugu,, by the way magari yamekuja late sana sisi ni watembeaji
May 16 at 8:10pm ·
Adam Gwankaja ukikumbuka HELCOPTER za CCM na CHADEMA zilivyokuwa zikipasua anga wakati wa kampeni, unaweza usiamini kwamba ni hapa hapa nchini ziliko barabara za aina hii! TUTAFIKA TANZANIA
May 16 at 9:38pm
Baraka Loya Mwambipile Ndio maana naipenda sana hii nchi yangu ya TANZANIA, maana tunaishi kwa zimamoto tuuu!!!. Itafika kipindi cha uchaguzi 2015 na tutaambiwa yaleyale tuliyoambiwa 2010 tutakubali na hawa wasanii wanasiasa. Tutakuwa tumesahau kama kuna kipindi barabara zetu ilikwa zina geuka kuwa mito kama hivyo kwa ajili ya kula yao. Tutafika tuu japo kwa kuchelewa sana wandugu.
May 16 at 10:49pm
Steven Mwakasitu jamani bro Adam, usinikumbushe siku ambayo nililala hapo Barabarani nikitokea Mtwara. kati ya siku nilizowahi ona tabu ni hiyo basi
May 17 at 9:12am
Maria Namusoke Jamani, is this a road or a pond,sijui nini sasa!!!
May 17 at 4:33pm ·
Asifiwe Alinanuswe had it been a pond we would go fish,,, its xxxxxxxxxxxxxx mmh @Baraka wanaacha ivo ili waje waombee 'kula' tena mwana,, Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote! nchi yangu jina lako ni Tamu saaaaaaaaaanaaaaaaaaaaaaaa
May 17 at 4:38pm
Baraka Loya Mwambipile ‎@Asifiwe, kuna umuhimu wa kuwa na kumbukumbu, wamezidi kududanganya na tabia za kuacha mambo mpaka wakati wa kampeni ukikaribia, inabidi kuwawajibisha mapema.
Kipindi hiki sina uwezo wa kuimba wimbo wote wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, nchi yangu Tanzania............., ninadhani niwengi hatuukumbuki wote. Swali ni je siku hizi hatuipendi Tanzania?
May 17 at 4:46pm
kwa kiwango cha elimu watoayo sidhani kama watu wanakumbuka,, @Baraka hawa jamaa achana nao,, uzuri wake ni kuwa hakuna awezae kukufundisha uzalendo, tazama hata wimbo wa uzalendo kama huo huukumbuki maana sekondari hukuimba, primary sijui,,, hata waliomba ndo hao tuliowapa jina zuri UFISADI,, hatutakumbuka kama walituahidi barabara maana watatujaza kanga, scarf, kofia na pombe kidogo then tunatia kwa moyo mmoja kwenye kapu la ccm na kama hatujatia wanachakachuaaaaaaaaa
May 17 at 5:02pm
Niliimba sana s/msingi na secondary, lakini huku mbele sijajengewa mazingira ya kuukumbuka. Nakumbuka zamani ikiwa sehemu inapandishwa ama kushushwa kwa bendera ya taifa lazima usimame, popote pale. lakini siku hizi ni kama zimebakia sehemu...See More
May 17 at 5:11pm
Ngojeni kwanza tuwaelimishe wananchi kuhusu hii dhana ya kujivua gamba. Maana wapinzani wanapotosha. Tukiona imeeleweka ndio tutageukia hili la maendeleo ya barabara. Kwa sasa tutaendelea kujibu mapigo ya hizo mnazoita tuhuma ya maendeleo duni mfano kwenye miundombinu kupitia vyombo vya habari na kupigana vita dhidi ya rushwa kupitia majukwaa, kama tulivyoelekezana kule dodoma hivi karibuni nadhani wote mnakumbuka maana kakipindi kakipita kidogo watanzani hawakawii kusahau. Yote katika yote, tumejitahidi sana kulinda tunu zetu walizotuachia waasisi wetu. Yaani AMANI, UPENDO NA MSHIKAMANO baina ya watanzania wote. Jamani hamuoni sisi tuko juu kuliko wenzetu?? Hatufanani na Somalia, Libya na sehemu nyingi tu za bara hili. Mkichezea tunu hizi yatawafika kama ya Libya na somalia!!
May 17 at 6:15pm ·
Ndugu wananchi mbona hamna msimamo? Kukiwa na ukame mnalia, ikinyesha mnalia, mabwawa yakiwa mbali na barabara mnalalamika eti hooo tunatembea umabli mrefu kufata maji sijui vp!! Jamani!!!, tukiweka hapohapo barabarani ndio mnapiga na picha na kuweka mpaka fesibuku kama hivi na komenti nyingi za ajabu ajabu!! Mnajua kabisa kwamba serikali yenu hii ni sikivu sasa isikie lipi na ifanyie kazi lipi. Pamoja na juhudi zoooote hizi za kumpunguza makali waziri wetu wa ujenzi na spidi yake ya kukausha mabwawa kama haya, lakini wapi!! Watz mfanyiwe jema lipi ndio mshukuru!!?
May 17 at 6:22pm · Unlike · 1 person

Tuesday, May 10, 2011

MITIKISIKO YA MUUNGANO - KUCHOMWA KWA MABANDA YA WABARA HUKO UNGUJA

Hii ya Wahuni huko Zanzibar kuchoma maduka ya 'Wa Bara' haina budi kulaaniwa na kuandamwa vikali lakini iwe ni salaam muhimu kwa watawala kwamba wanapaswa kuwa WASIKIVU zaidi.Ikiwafikia 'Wa Pemba' wa Kariakoo mbona itakuwa kazi kweli kweli!!! DHAMBI YA UBAGUZI NI ZAO LA DHAMBI YA SERIKALI KUKOSA USIKIVU.
Top of Form
Isaya James Mmh! Hili nalo neno!
Leah Mafwenga Mhhh sijui nani awaambie jamani
Adam Gwankaja salaam zitafika tu
Leah Mafwenga kwa njia gani we uadhani? ingawa nakubaliana na wewe zitafika tu ila sielewi zitafikaje
Adam Gwankaja hata zile mbaya na za kishenzi zaidi kama hiyo waliyotumia zenji. salaam zitafika tu
Leah Mafwenga poa nimekuelewa wangu
Arnold Samugabo Hawa jamaa hawatupendi sijui kwanini tunajipendekeza: watuambie mara ngapi tuwaelewe?
Leah Mafwenga mhhhhhhhhhhhhhhh!
Felix Mwakyembe ukweli hawatuhitaji japokuwa watu wenyewe njaa tupu
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka wale wote wanatuhumiwa kuhusika na kitendo iki cha kinyama ktk taifa letu...!
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka wale wote wanatuhumiwa kuhusika na kitendo iki cha kinyama ktk taifa letu...!
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka
David John Dhambi hii ni mbaya sana, tena Serikali iwachukulie hatua haraka wale wote wanatuhumiwa kuhusika na kitendo iki cha kinyama ktk taifa letu...!
Ninyi mnadhani hakukuwa na taarifa zozote za ki inteligencia? japo police ni ya muungano lakini police waliowengi ni wazanzibar. Wananchi wengi wa Zanzibar wanaona Muungano unawanufaisha wanasiasa na watu wenye pesa, lakini kwa walalahoi ha...See More
Umenena vema sana Baraka Loya Mwambipile. WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA? Hata hivyo nadhani hao 'wananchi wengi' wa zenji si kweli kwamba wanaona muungano hauna faida kwao, ila ni wanafiki may be. Je hawajui kuwa maduka ya KWA MPEMBA yako ...See More
Mimi ninayasema haya kaka nipo huku na nimeyaona yoote hayo na wapo wachache wanaoyatambua hayo. Narudia tena, wananchi wa kawaida wanaona wanaofaidi ni wenye pesa/matajiri na wanasiasa, mwananchi wa kawaida halioni hilo, wanaona ni sawa tu...See More
Gulila Nuru Tuwaanzishie wapemba walioko huku,kama hawawezi kuwavumilia wabara wetu kwanini sisi tuwavumilie? serikali inasemaje? wasijifanye wao watakatifu wakati wanachuma kwenye ardhi yetu na tunawaita ndugu wao wanatufanya kafiri,SIAFIKI MUUNGANO JAMANI!
uko sawa Baraka, lakini haingii akilini sana kwamba hawaoni faida. It is something they are made to believe hao maamuma, chanzo kiko mahali pengine kabisaaa, yaani nafsi za wanasiasa na wazandiki wengine. HIVI MWANANCHI WA KAWAIDA NI NANI huko Zenji? Hawa watumishi, wafanya biashara wadogo, wakati na wakubwa, hawa wanasiasa nk mbali mbali waliosambaa na kutapakaa huku bara, wametoka wapi? Wamedondoka kutoka mwezini? Hawana udugu na hao 'wananchi wa kawaida?' sio kaka, dada, shangazi, binamu, mjomba, baba na mama wa hao wananchi wa kawaida? Nani haupendi muungano? nani anadhani hafaidiki na muungano in real sense na kwa sababu gani? Lakini pia tujiulize kwanza, wazanzibar wanaoona hawanufaiki na muungano, WALITAKA WANUFAIKEJE? Wawe wakibebwa? Wakitawadhwa? NAAM, TUNAHITAJI KUJADILI HILI. TATIZO SERIKALI TULIYONAYO IMEPOTEZA UHALALI. INA HOFU. INA MASHAKA. HAIJIAMINI. NANI ATASIMAMIA MJADALA HUU?
Mimi nakuomba siku moja njoo kisiwa cha Pemba, halafu ufanye kama reseach fulani. Karibu kipindi ambacho ntakuwepo huku, maana sio wakati wote nakuwepo. Then yote hayo tunayoyaongea uta prove. Nasema hivi watu walioko bara hawatofautishwi na watu wa Zanzibar wowote ambao wako nchi za nje. Yaani bara ni sawa na nchi zingine tuu, kwamba unaweza hata kwenda kuomba msaada kama Tanzania inavyoomba misaada nchi zingine. Hivi unajua kuwa wewe hapo huwezi kumilki/kununua ardhi Zanzibar lakini wao wananunua tu bara mpaka nasikia wametengewa na eneo huko Bagamoyo kuwa kama la Zanzibar? Wanatambua kuwa ndugu zao wengi wako bara, lakini wakiwa nchi nyingine kama walivyo na ndugu hata uarabuni. Wanawafukuza wabara kama nasi kule kariakoo tunavyopambana na wachina kuuza ama kufanya umachinga wakati hata sisi waenyewe wa Tz tunaweza. Hapa ni kwamba kuna haja ya kuujadili kiupana muungano. And for sure kama kutakuwa na kupiga kura kwa wa Zenji kuwa muungano uwepo ama usiwepo, wangi wao watasema uvunjike kabisaa, wala hawautaki.
Felix Mwakyembe yote hayo yanayokana na kuwadekeza, niliwahi comment kuna siku kila Mzanzibari atakuwa kiongozi, Bara imewadekea sana tangu enzi za Mwalimu, hawa jamaa ni wale wenye chako changu lkn changu ni changu, ni wabaguzi wakubwa linapokuja sula la Tanganyika na Zanzibar
‎"hawa jamaa ni wale wenye chako changu lkn changu ni changu, ni wabaguzi wakubwa linapokuja sula la Tanganyika na Zanzibar" kaka Felix, tutazungumza mengi sana, lakini hawa jamaa hapo ndipo waliposimamia. Na hilo ndo kosa kubwa sana lililofanyika. Ndio maana wao wanazionesha waziwazi dalili za kuuvunja muungano lakini uongozi wa juu hautaki kulitazama hili jambo, wameweka pamba kwenye masikio na macho yao yana makengeza kiasi kwamba hawasikii wala hawaoni. Swali ninalojiuliza mimi ni je sisi wananchi wa kawaida tufanyeje? hapo ndo ninapokwama mimi binafsi
Felix Mwakyembe Baraka, nimekulia Zanzibar na kusoma huko tangu darasa la kwanza, nawaelewa sana so thinking yangu juu yao inatokana na experience ya tangu utoto, wabara tu wavumilivu saana, hata shuleni tulitengwa kiaina, kukitokea uharibifu wowote shuleni mnakusanywa watoto toka bara, etisisi ndo wakorofi, lkn uhuni wao wa hadi kulawiti vitoto vidogo hawausemi, kwangu Muungano hauna faida kweti heri uvunjwe
kwa kweli sina uzoefu sana zanzibar. Nimefanyakazi Unguja miezi minne tu, intennsively. Pemba sijafika bado.Siwezi kujisifu kujua hali halisi ya huko, lakini mambo flani flani ni dhahiri. Naamini pamoja na maelezo yenye hisia ya Baraka na Felix kwamba hapo Wabasiasa na viongozi wengine toke huko wana hatari zaidi kuliko 'wananchi' wa kawaida wa Baraka. Viongozi wanachochea hali hii.Ni viongozi wa vyama na serikali ndiyo waliopigania Wimbo wa taifa lao, ndiyo waliotaka bendera yao na ndiyo waliobadili katiba ya nchi yao. Hebu endelea kujiuliza hili swali dogo, Unguja ni kisiwa kidogo tu, ZILIKUWA WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA, hata ufedhri huo ukafanyika ? - watu wakakusanyana, wakala njama, wakajiandaa, hadi wakatekeleza azma yao? Kama ulivyosema felix kwenye wanabidii, hivi wabara ndiyo mafirauni zaidi hapa nchini? Baraka, kosa kubwa kubwa la viongozi wetu ni KUKOSA SIFA NA HIVYO KUPOTEZA KUJIAMINI. Kasoro kubwa ni kwamba Tanzania Bara haina mtetezi popote pale. Maana kwa mujibu wa katiba Rais wa Muungano ndiye msimamizi wa masuala ya bara yasiyo ya Muungano, he is two in one. Mwinyi alitutetea sana. Its time kabisa, we openly discuss haya masuala na kama vipi muungano na tuuwache, jamani. Baraka jiandae kurejea kaka. Hutakufa njaa, aseeee!
Kaka Adam kufanya kazi kwangu huku sio kwamba nimekosa sehemu ya kufanya kazi! hapana bali ilikuwa ni katika kuudumisha muungano na ukizingatia niko serikalini na kazi ninayofanya ni ya muungano, kwa hiyo kwa haya yanayotokea ndo nazidi kujifunza. Ila ninachoshukuru ni kwamba kazi yangu ni profesional so hakuna mtu anayenibughudhi kwa mimi kufanya kazi hii, japo huwa kunakuwa na vijineno vya hapa na pale vya nao wabara hao, kwani hizi kazi sisi hatuziwezi? lakini ningetaka kuhama ni kuomba tuu na kwa issue za kisiasa wala maboss hawawezi kunikatalia. Kwa hiyo uwepo wangu huku sio kwamba nanyanyasika , hapana, nipo naishi kama nyumbani ila by being carefull maana huwezi jua wanakufikiria nini.
Kwa namna wanavyofanya wazanzibar hata sioni haja ya kuwa na muungano na ingekuwa amri yangu ni kuuvunjilia mbali kabisa.
Sawa Baraka Loya Mwambipile, ni vizuri kujifunza kama ufanyavyo, hata hivyo si vema wapemba wakafika pahala wakadhani tunaenda huko kuganga njaa kama wanavyohemea misosi huku kwetu, na ndiyo msingi wa kukwambia jiandae kurejea kwetu, neema iko tele. Vijineno kwenye kazi ni kawaida, hata tulioko huku vipo. Lakini tukubaliane naposema hawa washkaji niwapuuzi; wanapodai kuwa hizo kazi mnazofanya huko wao wanaziweza, ilhali wakijua fika kuwa ndugu zao kibao wanafanya kazi upande huu wa Tz. Time is a good ticha, WE WAIT N SEE.
19 hours ago · Like · 1 person
Bottom of Form

Saturday, May 7, 2011

Literature and life:oh literature has made the today's me

Literature!oh literature has made the today's me. Ningeishije leo mimi!?. My gratitude be to all who have illuminated my way along this study kuanzia dada Tusweghe (RIP) who taught me kiswahili sayings, nahau na mithali, to Ms Dulle with her class readers and Tselestino Mwang'onda (Okonkwo), Kayuni (Ikemefuna), mr.Mvera to Koroga Korogoa Adamu, Njozi na Maselle wa Barra!  
By Adam GwankajaTop of Form

Mwasakafyuka Samson Ni vyema kutazama tulikotoka na kuwakumbuka wale waliotufikisha hapa. . . . . ! Bahati nami nimwanafunzi wa fasihi andishi ktk kiswahili, japo sikufika nayo mbali. .ila fasihi inajua kumfinyanga mtu. Nimekua imara kwakua niliandaliwa kuwa hivyo.
Adam Gwankaja ‎@Mwasak... We acha tu! I huenda ningesoma uhandisi ningepata A, ila akili yangu ingekuwa kama limashine fulani hivi aka liroboti!katika shule yangu ya kuungaunga kwa kamba, fasihi nilikuwa napata C tu, ila imeniumba! Jana @Asifiwe amenikumbusha, songs of lawino 'the last safari tu Pagak' mweeeeee! Mh!
Mwasakafyuka Samson Song of lawino, song Of Ocol, The river between, The Great pond, Is it possible , The African Child, things fall apart, Shida, Kuli, Harakati za ukombozi, kusadikika , Ngoswe. . . Etc. ! Nini unataka, ni kazi za wafinyanga ubongo, wametuumba.
Dear God,bless this boy Mwasa, anaongea maneno huyu. Ongeza Hawala ya Fedha, kumbuka big names kina Amandina Lihamba, sijui Penina Mlama, usisahau msingi wa Richard Mabala na Mabala ze fama na Hawa ze Basi duleva zilizotuandalia utangulizi wa kusoma vitabu vya fasihi; usiache Petals of Blood, the Trial of Dedan Kimaathi na ile ya braza Jero! A man of ze pipo hadi Enemy of ze pipo! I will marry when I want na God beats of wood, mine boy cha peter abrahams na women at point zero, watunzi kina Tsitsoi Dangarembaga na Eliehi Lema na Patched earth yake! Wee Ibrahm hussein na Majimaji! Usisahau the wreath of flowers na Rwanda magere! Eti the Gathering storm na Quo vadis Tanzania ya prince Kagwema! Ningekuwaje mimi bile haya na mengine mengi?
Hahaah, usisahau The blood petal by Ngugi wa Thiong'o, ktk yote Shafi Adam shafi mwishoni anakwambia, Yana mwisho haya, Ndyanao Balisidya yeye alikua na Kiwi cha Macho, Ni mambo magumu kufikiri, fasihi ni maisha. Fasihi ni roho, bado inaishi nasi, inatutia moyo kuwa Kina Clementina wanapungua, wanatambua thamani yao. . ! The Mine boy, moja ya riwaya kongwe na Murua, Mabala, alikua na Kingereza chake rahisi, utapenda kumsoma ! JE kalulu The Hare, hahaah, all goodthings they come to an end .
Bernard Elias Adam, ila this guy Dr. Maselle wa Balla is so special to we ex-literature people. He made life to be so possible.
Adam Gwankaja Kweli kabisa kaka. Nimeonana naye juzi nikampa mrejesho kuhusu jinsi DECONSTRUCTION THEORY inavyonibeba katika maisha haya, akacheeeeeka na kusema, "Nashukuru Adam, hii inanipa somo kwamba inabidi tufundishe VITU VINAVYOBEBEKA! mwaka huu nitautumia mrejesho huu"
Mwacheni Bara Masele aitwe Bara masele katika critical thinking in literature. Namkumbuka pia mwanazuoni huyu maana nilibahatika kupita katika mafundisho yake ya fasihi. hata hivyo, sijamsahau Dr.Lilian Osaki (African Literarature), Dr. Hamza Njozi (Modes of existence of the works of art),Dr. Korogoa wa Korogoto and Fuge Man (meaning and analysis in literature) na Mr. Majembe (professional intnl communication in english). they truly helped to pave our patterns of thinking.
Adam Gwankaja Patamu hapo. Hiyo timu ni nouma, nadhani ndiyo iliyoumiza vichwa na kuja na ile kitu iliitwa TANZANIAN LIT IN ENGLISH, tukashangaa kumbe kuna mijitabu kibaaaaao iliyoandikwa na waTz ilhali kweli mtaala wa shule tumejaza vya kenya na afrika maNgharibi!!!!
Bottom of Form

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP