Pekua/search

Tuesday, February 7, 2012

WANASIASA WANAWATUMIA WASANII KAMA KONDOMU - SINGLE USE ONLY

Mzee Sefu
Mzee Thabit Sefu wa mjini Mbeya amekuwa kwa muda mrefu akitumbuiza  kwenye hadhara mbali mbali mjini mbeya hususan za kisiasa. Ujumbe wa nyimbo zake katika ngoma yake yenye asili ya kingoni almaarufu kama DZOMBE umekuwa ukichoma moyo, kuamsha hisia na kufikirisha. Zaidi sana amekuwa nguvu kubwa ya kuwakusanya watu. Nilipofanya mahojiano naye mwaka 2007 alikuwa hakumbuki umri wake lakini kulingana na matukio anayokumbuka na kuhadithia alikadiriwa kuwa na miaka 80. Mzee Sefu amepitia mikasa mbali mbali ikiwemo kuchimbwa mkwara kwa kutumbuiza kwenye shughuli za VYAMA VYA SIASA VYA UPINZANI. Soma makala HAPA.

Hivi sasa hali ya mzee huyu inaelezwa kuwa mbaya sana (Bonyeza HAPA kufuatilia mjadala kwenye facebook). Si wanasiasa wa CCM ama wa Upinzani wanaomtupia jicho. Kama KONDOMU wamemtumia, wamefanikisha malengo yao, Washamaliza haja zao, WAMEMTUPILIA MBALI. Usanii ni laana nchini? kipaji ni balaa!!! Pole mzee SEFU.


Monday, February 6, 2012

KIWANDA CHA SARUJI WAZO CHAZINDULIWA (ni leo (Feb 6) katika Historia

Februari 6 Mwaka 1967 kiwanda cha kwanza cha kutengeneza saruji nchini kilizinduliwa huko Wazo jijini dar es Salaam. WENZETU WALITHUBUTU na kweli WAKAWEZA!! SISI JE?

Sunday, February 5, 2012

MABENKI YOTE YA KIGENI YATAIFISHWA (Ni siku ya leo - Feb 6 katika historia yetu)

Tarehe kama ya leo (Februari 6) hapo mwaka 1967, Mabenki yote ya kigeni nchini Tanzania yalitaifishwa na kuundwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara NBC. Wenzetu hawa hakika WALITHUBUTU, WALIWEZA, WAKAENDELEA MBELE VIZURI hadi mahali fulani michumia tumbo ilipoleta nongwa.

Friday, February 3, 2012

LEO (Februari 4) KATIKA HISTORIA: Mtanganyika wa kwanza kuwa Bwana Shauri wa Wilaya

Mwaka 1955 - Dunstan Omari aliteuliwa kuwa BWANA SHAURI (District Officer) wa kwanza Mwananchi nchini Tanganyika. Baadaye pia Omari akapata bahati ya kuwa Kamishna wa Wilaya (sasa Mkuu wa Wilaya aka D.C) wa kwanza. Huyu bwana alikuwa miongoni mwa Watanganyika/Watanzania wa kwanza kuhitimu elimu ya juu huko majuu. alisoma Aberystwyth University, Wales, ambapo alihitimu mwaka 1953.
kufuatilia kwenye Facebook bonyeza HAPA

Wednesday, February 1, 2012

TUMEPATIKANA: Madaktari wa Jeshi Muhibili nk - Je wao wanalipwaje?k

Hii nini? Ni simba akikosa MAJANI hula Nyama, au? Ikishindikana kuwatibu wagonjwa hospitali za JESHI hupelekwa Mhi2, leo madaktari wa huko geshini wamekuwa bingwa kuja mhi2 kututibu. eee Mungu tuhurumie. Iponye nchi hii, hata ikibidi WACHUKUE TU BAADHI YA VIONGOZI WETU WAHUNI.
 kusoma mjadala kwenye Facebook bonyeza HAPA

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP