Pekua/search

Sunday, August 25, 2013

Lengo la Kagame na Museveni ni moja kwa Tanzania

Lengo la Kagame na Museveni ni moja kwa Tanzania

 Imeandikwa na Kaa la ChumaWatanzania wenzagu, mabibi na mabwana asalaam alaikum, Bwana Mungu asifiwe.

Paul Kagame na Yowel Museveni ni watutsi (Hamitics) wanaoamini kuwa wao ndio bora mbele za Mungu na wao ni super race (kizazi bora) tuliosalia wabantu kuonekana machoni pao inferior race (kizazi cha ovyo). Hivyo basi ni imani yao kuwa si jambo jema kwa kizazi cha ovyo kuendelea kuneemeka na neema tulizopewa na Mwenyezi Mungu, Ardhi nzuri, milima ya kuvutia, madini ya kila aina, malisho ya mifugo bora, mito maziwa na bahari. Lengo lao linakuwa kuhakikisha kwa njia yoyote ile iwe kumwaga damu yaani vita au vinginevyo wanatutawala na kutanua himaya ya wahima (HIMA EMPIRE).

Ninamjua vizuri Mseveni Yowel Kaguta, kipindi cha vita ya Kagera alikuwa upande wetu tukipambana dhidi ya Idi Amini Dada. Vitani alitumia nick name ya MUYOKA yaani JOKA kifupi cha Museven Yowel Kaguta na wakati mwingine alijibadirisha nick names kulingana na sehemu ya mapambano. Ilifikia wakati nikiwa na wanajeshi wenzangu wa Tanzania tume- take control uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebe na ushindi wa kumuondoa Idi Amini umekaribia, makamanda tulianza kujadili ni nani anafaa kuwa rais wa Uganda na ni akina nani wanafaa kuwa wasaidizi wake. Makamanda watiifu kwa kikundi cha Mseveni walimpigia debe lakini sisi watz na jumuiya ya kimataifa tukamuona bado ni cha mtoto kuwa TOP MANYOTA tukamshauri atachukua nafasi fulani nyeti tena ya juu akagoma.

Alichukizwa na hali hiyo akatugeuka na kuanza kutushambulia wanajeshi wa Tanzania na kuangamiza walio wengi sana. Viongozi wetu wa kijeshi ngazi za juu komandi ya mwisho wakatuamuru makomando wote kuwa Museveni amekuwa adui na akionekana popote apatikane akiwa hai au mfu. Huyu jamaa kweli nyoka tulikuwa tunafanya Commando Mission tunaona gari aina ya Land Rover 109 anayoitumia inakatiza eneo la vita akiwemo tunaimwagia risasi nyingi na kuilipua anatoweka katika mazingira ya kutatanisha. Tulimaliza Vita tukarejea Tanzania akiwa amejificha misitu ya KONGO na akitembelea kwa baba yake na Paul Kagame Mzee Rukwavu Kagame ( rukwavu kinyarwanda maana yake sungura) huko Rwanda.

Mikakati yao ni aina moja, wanapandikiza watutsi ukabila wa nchi fulani fulani na kujiita wagoma, wakivu, wasukuma, waha, wahaya, wachaga na kujiita wazanaki lengo kuu ikiwa kujificha Unyarwanda wao (ututsi) ili kutawala sekta nyeti nchi za jirani ili mwisho wa siku mapinduzi yafanyike kiulaini. Hebu jiulize Tanzania usalama wetu uko wapi? Mkoani Kagera watutsi wanyarwanda wanajiita wahaya,wanyambo, wahangaza. Mkoani Singida wamejipachika makabila ya huko wakati huo huo Dar na Kigoma wanajiita waha. Iko siku wanatugeuka! Take care.

Siwezi kutoa siri ya jeshi hata siku moja ila wanasiasa nawatahadharisheni rushwa imekuwa ndiyo mbinu ya kuingia madarakani na ninyi ndio mmekuwa mkiamua mambo ya nchi hivyo kesho na kesho kutwa kikinuka mnatuamuru tuingie vitani. Halmashauri za Kagera wilaya zote ngazi nyeti wameshika watutsi kwa rushwa wanafedha kutoka kwa Kagame na Mseveni kuandaa mpango maalum. Hali kadhalika kwa mikoa ya Kigoma,Tabora, Mara na Katavi ni watutsi ndio madiwani, wabunge, madaktari mahospitalini, wenyeviti wa Halmashauri nk mpango maalum wa Rwanda na Uganda.Si ngazi hizo tu mpaka mawaziri ni watutsi, iko siku kitanuka kisa wanyarwanda waliojipachika utanzania mkawaruhusu kuongoza wamefanya mipango kuruhusu majeshi na siraha za Rwanda na Uganda kuingia nchini na kuteka maeneo muhimu raia a Tz wakazuiliwa kutoka au kuingia eneo lililotekwa wakatumika kama (HUMAN SHIELD) ngao ya binadamu itakuwa ngumu kuwanasua na kulikomboa eneo husika.

USHAURI: Wanasiasa acheni longolongo, vita si lelemama (sio kwamba naogopa wakianzisha tupo fiti na mziki watauona) ila acheni ufisadi unaoangusha uchumi wa nchi ili vita ikitokea uchumi ukiwa juu inakuwa rahisi kuliko uchumi ukiwa kama hivi ulivyo sasa na oparesheni maalum ya uraia halisi ifanyike bila kuangalia sura taaluma au utajiri wa mtu.
Imeandikwa na Kaa la Chuma (jamii Forum http://www.jamiiforums.com/jamii-intelligence/510788-lengo-la-kagame-na-mseveni-ni-moja-kwa-tanzania.html#post7160298) 

Mchangiaji mmoja amesema: 
Watanzania inabidi muwe macho na hawa wahutu wenye uchu wa damu za watusi,wanataka kuwaingiza katika matatizo makubwa yani janga! ili waweze kuingia madarakani,mwenye macho haambiwi tazamo,naamini yeyeyote yule anaye fikiria kupeleka vita kigali atakua mgojwa wa hakili kwani hatafaulu,na badala yake nikuwatia watanzania katika maisha ya ukimbizi ambayo hawakuyazoea,please epukaneni na hizo siasa za wahutu kama huyu mtoa maada. 

Adam:
Langu mimi ni kwamba, chuki ya kikabila baina ya Wahutu na Watutsi isiposhughulikiwa, itaisambaratisha Afrika Mashariki na Kati! Hapa kinachotawala ni CHUKI na TAMAA.


Friday, August 16, 2013

Kikwete Muunge Mkono Mwakyembe vita ya Mihadarati!Kikwete Muunge Mkono Mwakyembe vita ya Mihadarati!

 Mhakikishie ulinzi
Rais Kikwete. Chanzo- IPPMedia
Moja ya jambo lililomletea sifa Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ni kuzinduka usingizini na kupanga safu yake ya watendaji iliyobora zaidi.Miongoni mwa mawaziri wanaotajwa kuwa madhubuti na makini katika utendaji wao ni Sospeter Muhongo, William Mgimwa na Harrison Mwakyembe, na Naibu waziri January Makamba. Hawa wameungana na mawaziri wengine waliokuwepo tangu mwanzo kama vile John Pombe Magufuli.Uteuzi mzuri ni hatua muhimu japo haijitoshelezi kukamilisha utendaji uliotukuka. Usimamizi na miongozo isiyo na chengachenga ni muhimu zaidi kuhakikisha Mawaziri wanatekeleza wajibu wao vizuri. Ndiyo maana katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa, mawaziri husika wanakula kiapo (mkataba) wa kujifunga kuwajibika.Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Uchukuzi, hivi karibuni amejitokeza na kuweka msukumo mkubwa zaidi katika kukabiliana na aibu iliyolifika taifa letu. Janga la miharadati.Jambo hili linagusa wizara yake moja kwa moja na hivyo anao uhalali wa kisheria kujitoa kwa dhati ya moyo wake kukabiliana na jambo hili maana imethibitika kuwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere ni njia kuu ya kusafirishia madawa hayo huku kukiwa na madai kuwa Bandari ya Dar es Salaam, ndiyo lango kuu la kuingizwa nchini madawa hayo.Kujitokeza kwa Mwakyembe kumepeleka salamu nzito kwa Vigogo wa Unga nchini na duniani. Rekodi ya Mwakyembe iko wazi kwamba akilisimamia jambo huwa hafanyi makida makida wala kuigiza, anamaanisha. Ndivyo wanaomfahamu wasemavyo. Janga hili la aibu kwa taifa kuwa genge la wauza unga, kama ni kipele kimepata mkunaji. Ahsante Rais Kikwete kwa kuipatia Tanzania mtu huyu kusimamia wizara hii. 
Dkt. Mwakyembe. Chanzo- Swahili Times

Hata hivyo jambo hili ni la hatari kubwa kama inavyojulikana duniani kuwa biashara hii inafanywa na mijitu isiyokuwa na haya wala soni, mijitu isiyokuwa na utu bali iliyojaa damu mikononi mwao. Ubabe wa wauza unga unaelezwa kuwa chanzo cha mamlaka mbali mbali kunyamazishwa, ikiwemo mamlaka iliyokuu kabisa ya utumishi wa nchi.Kujitokeza kwa Dkt. Mwakyembe ni kujitoa mhanga maisha yake. Ni mfano wa uzalendo unaohitajika sana miongoni mwa viongozi wetu. Hatua hii ya Mwakyembe inayaweka majukumu mazito mikononi mwa Rais Kikwete. Na kusema ukweli ni hatua inayompa mtihani mkubwa Rais wetu, maana ni lazima afanye kitendo kumuunga mkono mteule wake.Moja ya jambo analoweza kufanya Rais Kikwete ni kutangaza hadharani kabisa tena mapema sana kuwa anaunga mkono jitihada za Wizara ya Uchukuzi chini ya jemedari Dkt Mwakyembe. Hii itaongeza uzito wa salamu aliyotuma Mwakyembe kwa vigogo wa unga.Sambamba na kutangaza hadharani kabisa kuunga jitihada za wizara ya uchukuzi, Rais pia hana budi kumhakikishia waziri wake ulinzi. Usalama wa Mwakyembe ni suala nyeti la usalama wa taifa. Ni ishara ya mwanzo wa ushindi wa taifa tukufu la Tanzania dhidi ya miharadati. Kwa hesabu za kawaida, mashetani ya biashara ya unga, yatatamani sana kumuangamiza Mwakyembe ili kuzidi kueneza hofu miongoni wa binadamu wa kipindi hiki.Pia unyeti wa kumlinda waziri Mwakyembe unatokana na historia ya maisha yake ambapo muda si mrefu alinusurika kifo baada ya kudaiwa kulishwa sumu. Jambo hili ni nyeti zaidi sasa, maana kudhulika kwake kokote hivi sasa kunaweza kuwa mwanzo wa kusambaratika kwa taifa. Watanzania wanyonge na wapole hawa wanaoumizwa na dawa za kulevya na madhila mengine wanaweza kuamua kuililia damu ya kiongozi wao na tangu hapo hamkani haitokuwa shwari tena!Nimefanya utafiti mdogo juzi na jana kwenye mitandao ya kijamii, unaona wazi kabisa kuwa wasafirisha unga (punda),  vigogo wa unga pamoja na makuwadi na walamba viatu wao, wamekazana kumkejeli na kumkatisha tama Mwakyembe. Unakutana maneno kama vile “hana ubavu huyo, ni mpenda sifa tu, hana lolote, anatafuta urais huyo”.Kutoka thehabari.com
Kama ni kutafuta sifa, basi Mwakyembe amechagua fungu lililojema, maana analikabili suala ambalo likiachwa liendelee litaizamisha nchi! Kama ni upenda sifa, basi natamani kila waziri akiwa mpenda sifa kwa namna hii na taifa litaanza kung’aa tena badala ya kuzidi kufifia na kufubaa.Aidha Rais Kikwete anayosababu zaidi ya kutangaza kumuunga mkono waziri Mwakyembe. Habari zinahusisha kusuasua kwake katika vita dhidi ya miharadati na kuhusika kwa familia yake katika biashara hii. Taarifa zinabainisha kuwa mwanawe Rais Kikwete, ni miongoni mwa vigogo wa unga nchini.Taarifa za Ridhiwani Kikwete kuhusishwa na dawa za kulevya si ngeni nchini. Zimeenea si haba. Na hata hivi karibu ametajwa kwenye kinachoitwa kuwa barua kutoka kwa wafungwa wa kitanzania huko Hong Kong! Haya yanaweza kuwa ni maneno tu ya waswahili sisi. Na maneno hata kwenye khanga yapo.Lakini kule kumhusisha Ridhiwani, mtoto wa mtumishi mkuu wa umma, si jambo la kufumbia macho.Rais wetu anapaswa aoneshe kwa vitendo kuwa hahusiki yeye wala familia yake. Moja ya njia za kuthibitisha hilo ni kutangaza kumuunga mkono Dkt. Mwakyembe pamoja na wote wanaojitoa mhanga katika kukabiliana na janga hili. Zaidi mhe. Rais awahimize mawaziri wengine wanaohusika kwa namna yoyote kama vile mambo ya ndani, maliasili na utalii waungane katika harakati hizi maana kidole kimoja kinavunja chawa kwa shida sana!Shime Rais wetu. Bado tumesaliwa na kaimani kidogo nawe.
Ridhiwani Kikwete ktkt ya Rais wa China na Mkewe. kutoka blog ya Darmetropolitan

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP