Pekua/search

Friday, July 27, 2012

J.A. Mwamsiku the Great Inspirator dies


A J Mwamsiku the Great Inspirator dies

Ni leo (Julai 27) katika Historia yangu
R.I.P Jubeck A. Mwamsiku

Hapo mwaka 2009 aliondoka duniani kurejea kwa muumba, baba yetu baada ya kupambana vikali na kansa. Alfajiri ile tulipopata habari ilikuwa ngumu na chungu. Ila mwisho wa yote tunamshukuru Mungu kwanza kwamba alitupa baba ambaye alikuwa rafiki, kiongozi madhubuti na aliyetupenda na kuwapenda binadamu wenzake sana.

Wiki moja kabla ya kifo chake mimi na Peter tulikuwa naye akitupa tumaini! Akitabasamu kutupa moyo! Na tulipoagana kurudi Arusha nakumbuka alisema, “Nendeni tutaonana Mungu akipenda. Nimefurahi sana kuwaona.” Naam alimaanisha tutaona siku moja tusioijua lakini iliyodhahiri katika ulimwengu wa imani.

Swali moja tu sikukuuliza ewe kiongozi wangu! Nilitamaani kukuuliza wiki ile ya mwisho lakini ulikuwa mgonjwa zaidi. Nikaahirisha. Ni swali hilo tu ulilopona . Hata hivyo namshukuru Mungu kwamba alikujaalia hekima kuu maana ulistahimili  mvua ya maswali tangu utoto wangu. Nashukuru kwamba ulinijibu kwa uaminifu. Ulinipa misingi ya kuishi katika maisha haya.
Wajukuu zako wanaendelea kupenda kujifunza 

Nilimuuliza mama swali lile, naye alinijibu. Limenifungua macho ila ninamiss ungekuwepo ningekuuliza mwenyewe. Wajukuu zako wakikua nami nikiishi sana, I will ask them what they think about this qn.

Kilimo:
Kati ya mambo mawili, ulisisitiza kilimo. Mechanizing agriculture japo ulipinga pawatila. Naam tumeanza. Kaka Edom na Afyusisye wanaendelea. Wale vidume sasa wamekuwa maksai, japo mmoja kawadhaifu tumembadilisha. Kubwa zaidi natamani ungekuwepo japo nikusimulie mwanzo mzuri wa Gwankaja Creations Agriculture scheme.
Elimu:
Wajukuu zako wanaendelea kusoma. Naam watasoma vizuri kwa msaada wake Mungu. Msisitizo wako katika elimu tunauendeleza na tutaendelea kusisitiza watu kujifunza.
Mama yetu (Mkeo), Tummenye, anaendelea kujitegemea

Rafiki yako P, the senior anasema anamiss ulivyokuwa unamsomea.Thursday, July 26, 2012

Bunge la lakataa Muswada wa Mafao kwa Mawaziri, RC na DC


Bunge la lakataa Muswada wa Mafao kwa Mawaziri, RC na DC

Ni leo (Juni 26) katika Historia yetu
 Mwaka 1968 Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania lilitumia mamlaka yake na kuukataa muswada wa serikali wa kutaka kuwalipa kiinua mgongo Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na wale wa Wilaya.
Hata hivyo muswada huo ulirudishwa tena Bungeni na kupitishwa kuwa Sheria kufuatia matamshi (vitisho) ya Rais Julius Nyerere kwamba, endapo wabunge wangeendelea kuupinga muswada huo, basi ingebidi warudi kwa wananchi (Kulivunja Bunge).

Najiuliza kwa sauti je Wabunge wa leo hii wangethubutu hii kitu?

Jikumbushe Baadhi ya Maspika wa Bunge tangu Uhuru
  • Mhe. Abdulkarim Y. A. Karimjee - Januari 1, 1959 - hadi Desemba 26,1962
  • Mhe.Adam Sapi Mkwawa - Novemba 27,1963 hadi Novemba 19,1972 na Novemba 6,1975 – Aprili 25,1994
  • Mhe. A. M. Erasto Mang’enya Novemba 20, 1973 – Novemba 5, 1975
  • Mhe. Pius Msekwa Spika Pius Msekwa ndio Spika wa Bunge la kwanza la Vyama vingi la 1995 kwa kuwa yeye alikalia kiti cha Uspika kuanzia Aprili 28, 1994 hadi Desemba 28, 2005
  • Mhe.Samuel John Sitta Desemba 28, 2005- Novemba 10, 2010. Aliongoza kwa kauli mbiu
    ya Kasi na Viwango.
  • Mhe. Anne Semamba Makinda Oktoba 30, 2010- Spika wa kwanza mwanamke. 


Wednesday, July 25, 2012

Wanajeshi Shupavu wa Tanzania warejea kutoka Uganda


Wanajeshi Shupavu wa Tanzania warejea  kutoka Uganda

Ni leo (Julai 25) katika Historia Yetu

Hapo mwaka 1979 - Wanajeshi wa Tanzania waliopigana vita ya uchokozi wa Idd Amin aliyekuwa rais nchini Uganda, waliwasili katika ardhi ya Tanzania huko Kagera na kulakiwa kwa furaha kuu na wananchi. Kufuatia tukio hili hivi sasa Watanzania tunaadhimisha siku hii kuwa siku ya MASHUJAA, badala ya Septemba mosi ya awali.

Jikumbushe baadhi ya Matukio makuu ya kuhusu vita hivyo:
Oktoba 30, 1978 Majeshi ya Idd Amini aka nduli wa Uganda yalishambulia Kagera na kusababisha vifo vya watu na uharibifu wa mali nyingi (uchokozi)

Novemba 2, 1978 Amiri Jeshi wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitangaza vita dhidi ya uvamizi wa Idd Amini. Baadhi ya maneno aliyotumia ni maarufu hadi sasa nayo ni, “ Sabababu tunayo..Nia tunayo ..na Uwezo wa kumpiga tunao..”

Machi 16, 1979 huko Lukaya nchini Uganda majeshi ya wananchi (ya ukombozi) wa Uganda yakihimiliwa na vijana shupavu wa majeshi ya Tanzania yalipigana vita vikali zaidi dhidi ya yale ya nduli Idd Amini. Inaelezwa kwamba askari wengi sana wa majeshi ya Idd Amini waliangamizwa.

Juni 16, 1979 Rais Nyerere alitangaza kumalizika kwa vita ya uchokozi ya Idd Amini

Julai 12, 1979 Wapiganaji wa majeshi ya Tanzania walianza kuondoka Uganda kurudi nyumbani.


Monday, July 23, 2012

Tumefanikiwa kuwakinyamazisha walimu matokeo tumeyaona...Tunajaribu Madaktari


Tumefanikiwa kuwakinyamazisha walimu matokeo  tumeyaona...Tunajaribu  Madaktari

  • Walimu wakinyazishwa matokeo yake wanafunzi hawafundishwi wala kusaidiwa kujifunza. Tumefanikiwa katika hili. 
  • Sasa Serikali inajaribu kuwanyamazisha madaktari....Kwanini hatujifunzi?  
Mwl.Makini angependa wanafunzi wake wajisaidie kwenye choo bora zaidi ya hiki

Nimesoma post ya Rafiki yangu wa mtandao wa Facebook, Mh Ahmaed Lukinga akihoji iwapo Walimu mkoa wa Singida wako kwenye mgomo, “SINGIDA WALIMU WAMEGOMA?” Anauliza, na kuendelea kuifafanua hoja yake kwa kutupa mfano wa mojawapo ya shule zilizofanya vizuri katika mtihani wa mock kidato cha nne mwaka huu.

Anatupasha kuwa shule hii iitwayo Ntonge imekuwa ya 20 kati ya shule 124 za mkoa mzima wa Singida na anatanabahisha kuwa shule hiyo imekuwa na matokeo kama ifuatavyo:  
Daraja la I=0
Daraja la II=3
Daraja la III=6
Daraja la IV=17
Waliofeli kabisa=2
Zaidi Rafiki yangu huyu aliyejitambulisha kuwa ni mwalimu anahoji, “KAMA MKOA MZIMA UPO HIVO UNATEGEMEA VIWANGO GANI VYA UFAULU KATIKA MITIHANI YA TAIFA KIDATO IV MWAKA HUU?” na kuongeza, “Hii ndiyo hali halisi, Watanzania wenzangu. Mwl. Ahmed Lukinga.”

Mwl. aliyenyamazishwa hajali kufundisha ktk darasa kama hili

Nikiwa nawaza kwa sauti najikuta kupata hamasa ya kujua zaidi...naishia kujiuliza tu.. hivi kama shule hiyo yenye wanafunzi wasiozidi 30 inafanya hivyo je shule zenye wanafunzi 100 hali ikoje? Lakini zaidi ikiwa Ntonge ni shule ya 20 kati ya 124 je shule ya 100 imekuwa na matokeo gani?

Narudi kwenye swali la msingi la Rafiki yangu Lukinga, nadhani si kwamba walimu wamegoma.. kunao ushahidi wa kutosha kubainisha kwamba walimu WAMENYAMAZISHWA. Waliposema hali yao ni mbaya kiasi kwamba haiwavutii kuendelea na kazi, tuliwapuuza na kibaya zaidi tuliwatishia maisha.. mkulu wan chi alisema wakigoma watakong’oliwa ‘waende kwenye meza ya mazungumzo wakiwa na bandeji na ngeu.’

Baada ya kufanikiwa kwenye kuwanyamazisha walimu sasa serikali iko makini kweli kweli kuwanyamazisha madaktari. Wasiseme, wasihoji achilia mbali kudai chochote...inawalekeza kuwa meza ya majadiliano ndio mwarobaini lkn katika hali ya kawaida wakiidai hiyo meza wanatishwa na kutishiwa maisha. Madaktari wanapaswa kuwa wazalendo...wanasiasa uzalendo wanaweka pembeni. Naami

Naam, Walimu wamefuata ushauri wa rais, wamekuwa mbayuwayu...hawajagoma wala kuandamana..na kweli wamepona, hawayajawakuta ya Dkt Ulimboka...ila hali ya elimu imekuwaje? Hata hivyo tumepata nafasi walau hii ya kuhoji na kujihoji. Lakini tunapojaribu kuwanyamazisha madaktari.........NATUENDELEE KUISHANGILIA SERIKALI.
Mwalimu asiyenyamazishwa huwa na ari na ubunifu unaotakiwa kutengeneza na kufaragua zana za kufundishia na kujifunzia


SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP