Pekua/search

Monday, May 26, 2014

Dedication to my Heroes- Bishop Amon Dick Mwakisunga

KUTABARUKIA Mashujaa Wangu
Askofu Amon Dick Mwakisunga- Aliyeitwa Kwa Rehema Zake Mungu Kurejea kwake, Mnamo Mwezi kama huu wa Mei 2003 (tarehe 5), Rehema zake Mungu Ziwe Juu Yake.

Katika mengi niliyoweza kujifunza kwa Mpakwa Mafuta huyu wa Bwana ni KUFANYA MAAMUZI. Aliweza kufanya MAAMUZI akapongezwa au Kulaumiwa, lakini Aliamua. Mfano, aliamua kuhamisha Makao Makuu ya KKKT Dayosisi ya Konde kutoka Manow na kuyaleta Tukuyu Mjini. Pale Manow alianzisha shule ya Seminari, ambayo kwa wakati ilianza kuchanua chini ya uongozi wake Baba Mchungaji Mwasamwaja...kabla mchwa haujaingia. Shikamoo mchwa.

Katika ulinganifu mzee wa 'shashaaa' - akimaanisha sasa aliweka mizania kati ya kukuza dayosisi kiroho na kimwili.


Amon Dick Mwakisunga alianza maisha yake akiwa Mwalimu waHisabati, Historia, Jografia na Kiswahili pale Shule ya Misheni ya Kiluteri pale Mwakaleli mnamo Mwaka 1953. Hii ilikuwa ni baada ya kuhitimu elimu yake ya Msingi Manow mwaka 1948, Sekondari pale Bulongwa mwaka 1951 na elimu ya ualimu Rungwe Alliance TTC mwaka 1954.

Kwa upande wa safari yake ya utumishi, alijipatia Stashahada ya Theolojia huko Ujerumani, chuo kikuu cha Hamburg mwaka 1964 na kisha Shahada Takatifu ya Umahiri (Uzamili) chuo kikuu hicho hicho cha Hamburg mnamo mwaka 1967.

Alitumikia katika nafasi mbali mbali ikiwemo kuwa Mkurugenzi wa Vijana wa sinodi ya Kusini ya KKKT, Mhadhiri chuo cha Theolojia Makumira ambapo pia alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo, Katibu wa Afrika huko Geneva katika Fungamano/Shirikisho la Makanisa ya Kilutheri (LWF). Na kati ya Mwaka 1989 hadi 2001 alipostaafu, alikuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Dayosisi ya Konde. Ndio wakati huu nilipomfahamu mimi.

Pumzika kwa Amani Baba yetu. Wengine sisi hatutakusahau daima.

Sunday, May 11, 2014

The Wings of Kilimanjaro vs Wings of THE Kilimanjaro....?The Wings of Kilimanjaro na Wings of THE Kilimanjaro....ni sawa?
NAULISA...

1. Wings of THE Kilimanjaro
2.THE wings of Kilimanjaro.
Bango la Air Tanzania- maandishi hayo yako kwenye moja ya ndege

  Nimeeona tungo hizo kwenye kila moja kati ya ndege mbili za Air Tanzania. Hizo article ZE zinabadili maana? Au basi kwanini zimeandikwa sehemu tofauti ya tungo?

Au ni kwa kuwa Kiingilishi chenyewe kililetwa kwa MELI ama Ndege?

Mliobobea katika Lugha ya Kimombo saidieni.

Napenda kujifunza tu. Nisije ulizwa ugenini nikawatieni aibu.
Ndege yenye Wings of the Kilimanjaro


Thursday, May 1, 2014

Tanzania: Yuko Wapi Kiongozi wa Ukweli mtu wa watu?Benjamini Mkapa- Uwazi na Ukweli?

Yuko Wapi?

Yuko wapi Kiongozi jabari na mweledi?

Yu wapi kiongozi Mahiri? Yuko wapi shupavu?

Yu wapi Kiongozi mwenye nia thabiti ya kuchochea maendeleo ya taifa hili?
Yuko wapi kiongozi wa ukweli

Yuko wapi aliye madhubuti na hodari kiuongozi akemee Zanzibar kujitungia katiba yenye kuchepusha muungano? Yuko wapi?

Yuko wapi kiongozi kati ya hawa wa kwetu katika chama tawala na kwenye vyama vya ushindani, mwenye kuupenda muungano? Yu wapi?

Nani kati yao hawa wetu viongozi mwenye kuenzi fikra na matendo ya Mwalimu Nyerere kwa kumaanisha? Yuko wapi?

Yuko wapi kiongozi anayeamini kuwa siasa si mchezo mchafu wa ghiriba, hila na ‘usanii’? mmemwona wapi?

Jakaya Kikwete- za kuambiwa ongeza za??
Yu wapi kiongozi hapa nchini anayeamini kabisa kabisa kuwa mamlaka ya nchi yanatokana na watu wana wananchi? Yuko wapi?

Yuko wapi kiongozi anayeupenda Muungano kwa dhati ya moyo wake? Yuko wapi? Tanzania inamtaka na atamke sasa kwamba Muungano wa serikali mbili ziiiiiiiiiii!!!!

Na aseme sasa kwamba muungano wa serikali tatu ziiiiiiii bali twende kwa serikali moja muungano kamili?

Tuamini YUPO. Tuafiki WAPO.
Lakini wako wapi? Kwanini wanajificha? Kwanini midomo yao inakuwa mizito na matendo kwao ni muhali kufanyika?

Yuko Wapi Kiongozi wa Ukweli mtu wa watu? Yuko wapi kiongozi mwenye dhamira ya dhati?
Alhaji Ali Hassan Mwinyi- Ruksaaa- na li kul-li ajalin kitaab.

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP