Pekua/search

Sunday, October 9, 2011

KULIKONI KIMYA CHA MAMLAKA ZA NCHI DHIDI YA VIONGOZI KUZISHIWA KIFO?


 Je nalo ni tunda la miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika?


PAMOJA SANA: Prof. Lipumba alipomtembelea Prof. Mwandosya Hospitalini
Tabia ya watu mbalimbali hususan viongozi kuzushiwa kifo inazidi kuota mizizi miongoni mwa watanzania:

Ndani ya miezi mitatu, Waziri wa Maji Prof Mark Mwandosya kazushiwa kifo mara mbili. Hii ni pamoja na majuzi ambapo taarifa kwamba amefariki zilienea karibu kila pembe ya nchi!

 
Sheikh Yahya Hussein alizuliwa kifo mara kadhaa kabla ya kufariki!

Mufti Sheikh Shaaban Simba naye vivyo alitangazwa kukumbwa na umauti akiwa kwenye matibabu nchini India.
Orodha ya waliozushiwa kifo yaweza kuwa ndefu.

Kinachosikitisha, kutia shaka na hofu zaidi ni ukimya wa mamlaka za nchi dhidi ya tabia hii mbaya na isiyo ya kistaarabu. Sikumbuki kusikia tabia hii ikikemewa vikali na serikali, madhehebu ya dini ama  asasi nyingine za kiraia!

Kuna madai kuwa kutangaziwa kifo kwa Prof Mwandosya kunahusiana na hofu na minyukano ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu 2015. Kama hivyo ndivyo, Je tutakuwa tumekosea tukiamini kuwa kimya cha mamlaka za nchi kinalenga kubariki siasa za kimafia ambazo mwisho wa siku zitaifanya Tanzania isitawalike kirahisi?

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP