Pekua/search

Monday, December 10, 2012

Nyerere Alipohutubia Bunge Kwa KiswahiliNyerere Ahutubia Bunge Kwa Kiswahili Kwa Mara Ya Kwanza

Leo (Desemba 10) Katika Historia yetu

Mwaka 1962, mara baada tu ya Tanganyika kuwa Jamhuri, Rais wa Kwanza wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere alihutubia Baraza la Taifa (National Assembly) Kwa kutumia lugha ya KISWAHILI. Awali lugha iliyotumika kwenye baraza hilo ilikuwa Kiingereza.

Nia na dhamira ya dhati ya kukienzi Kiswahili, si kwa sababu ya uzalendo tu bali pia kwamba ndiyo lugha inayoeleweka na watanzania wengi, iliwekwa bayana tangu mwanzo. Leo hii tunasuasua kukifanya Kishwahili kuwa lugha ya kufundishia licha ya tafiti mbali mbali kuthibitisha kwamba lugha ya kufundishia inapaswa kueleweka vizuri baina ya mwalimu na mwanafunzi.

Licha ya ushahidi wa kutosha kwamba hata sasa walimu wetu kutoka sekondari hadi chuo kikuu hawafundishi wakaeleweka pasipo kuchanganya KISWAHILI katika ufundishaji wa masomo yao, mfano:
“Slaves were obtained through many ways such as...waylaying yaani kuwavizia...”..Unaona ee mtu unajipitia ghafla unakamtwa sawa?”

Saturday, December 8, 2012

Leo ni Si ya Uhuru wa TanganyikaLeo (Desemba 9) ni Si ya Uhuru wa Tanganyika

Rejea ya Historia ya nchi yetu inaonyesha kuwa leo miaka 51 iliyopita ndipo Tanganyika ilipata uhuru wake. Siku kama ya leo hapo mwaka 1961 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokea Hati za Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Prince Phillip, Mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza. Mwalimu Nyerere ndiye Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika.

Ni siku ya kutafakari. Ni siku ya kupambanua.
Tukifanya hivyo hebu tuimbe pamoja wimbo huu:


Na huu pia..


TAZAMA RAMANI

Tazama ramani utaona nchi nzuri
Yenye mito na mabonde mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa....

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

Chemchem ya furaha amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako nikiburudika,
Nakupenda sana hata nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha Tanzania.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

Nchi yenye azimio lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga wa Watanzania,
Ninakuthamini hadharani na moyoni,
Unilinde nami nikulinde hata kufa.

Majira yetu haya, yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi, Nyerere
ameukomesha X2

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP