Pekua/search

Monday, August 27, 2012

The Great Inspirators - Tuwasifu wakiwa hai bado


Mzee Ambepwile Mwakapasa aka Mfugaji - Kijiji cha Isange, Tukuyu
They inspired me to love Community development
Ni katika kutafakari misimamo na mitazamo ya wazee hawa nikajiwa na falsafa ya ING'ENG'EESI, kimombo Bamboo bee! Hana sifa sana za kuweza kuruka, lakini anaruka sana tu.
Ndipo nilipopata picha kwamba kazi za kujiolea ni sawa na bomba la maji..haliyanywi maji hayo lakini hupoozwa nayo.

It is from them that i learnt to love Community development work. God bless these great men of Isange Village, Tukuyu, Mbeya, Tanzania. (Shukrani nyingi kwa Hezekia Mwalugaja wa HOCET kwa picha hizi) la sivyo nisingeweza kupata kuwashukuru wazee wangu hawa wangali hai.Pamoja na hawa katika kundi hili yuko John Mwalugaja, Mwasakujonga na Ben Mwakanyamale(hawako pichani)! Mungu awabariki.
Mzee Ahadi Lufingo Mwakibete (Tshirt nyeusi)- Isange, Tukuyu
Mzee Robert Mwakasendo aka Mwenyekiti (kushoto)- Isange
  

Saturday, August 25, 2012

Dar na miji mingine ingekuwa Yatima leo hii- SENSA NJEMA


Utaratibu wa Sensa usingebadilika-  Dar na miji mingine ingekuwa Yatima leo hii

“Siku zile amri  ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba IANDIKWE ORODHA YA MAJINA YA WATU WOTE (SENSA) wa ulimwengu (nchini mwake). Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu. Watu wakaenda kuandikwa, kila mtu  mjini kwao. Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa ukoo na jamaa ya Daudi, ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa naye ana mimba, ikawa katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori la kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni. “ Luka Mtakatifu – 2: 1- 7.

Haya wandugu HESABIWENI. Enzi za wenzetu ingebidi Dar es Salaam kwa mfano ibaki na watu wachache tu.
Jikumbushe kuhusu sense nchini:
Sensa ya kwanza Tanzania ilifanyika mwaka 1910. Sensa nne za Mwisho zilifanyika baada ya Uhuru, katika miaka ya 1967, 1978, 1988 na 2002.
Kulingana na sensa ya mwisho iliyofanyika mwezi Agosti 2002, idadi ya watu nchini Tanzania ilikuwa 34,443,603.
Waziri Mkuu Pinda alipozindua uhamasishaji wa Sensa ya Watu na Makazi 2012

Matokeo ya Sensa ya Watu 1967-2002 na Makadirio kati ya mwaka 2003-2025 Mwaka Idadi Mwaka Idadi
1967 12,313,469
1978 17,512,610
1988 23,095,885
2002 34,443,603
2003 34,859,582
2004 35,944,015
2006 38,250,927
2009 41,915,880
2010 43,187,823
2012 45,798,475
2015 49,861,768
2020 57,102,896
2005 37,083,346
2025 65,337,918
Rais kikwete alipohutubia taifa kuhamasisha ushiriki katika Sensa jana. Picha kutoka Twita ya Haki Ngowi.

Friday, August 24, 2012

Kinjekitile Ngware wa Majimaji atiwa nguvuni na wajerumani.


Kinjekitile Ngware wa Majimaji atiwa nguvuni na wajerumani.
Ni leo (Agosti 24) katika Historia yetu

Rais Kikwete lipozindua mnara wa kumbukumbu ya mashujaa wa Maji maji Agosti 2010 huko kilwa
Mwaka 1905, Wajerumani walimkamata mtanzania aliyekuwa chimbuko la ujasiri wa wana wan chi katika kuukabili uvamizi wa wageni toka ujerumani huko kusini mwa Tanzania enzi hizo. Huyu si mwingine bali Kinjekitile Ngware. Hatimaye madhalimu haya yalimnyonga shujaa na mwanafalsafa wa kitanzania Kinjekitile Ngware, tena yalimnyonga hadharani huko muhoro, Rufiji.

Jikumbushe baadhi ya matukio muhimu kuhusu vita vya maji maji:
Agosti mosi, 1905 vita ya maji maji dhidi ya Wajerumani iliyokuwa imeanza mwaka huo ilienea na kuyahusisha maeneo ya Songea, Masasi, mtwara, Lindi, Rufiji na maeneo mengine ya ukanda wa pwani ya bahari ya Hindi nchini.
Baadhi ya mashujaa wa maji maji wakiwa wametekwa na madhalimu ya kijerumani
 Agosti 5 1905 wapiganaji wa maji maji walishambulia misheni ya kanisa katoliki Nachingwea na kumwua Askofu Cassian Speiss. Huyu alikuwa askofu wa kwanza wa kanisa katoliki jijini Dar es salaam. Kifo kilimfika askoofu huyo akiwa safarini kueneza dini huku Mukukunumbu, Nachingwea.

Agosti 14, vita kali na vilivyoua watu wengi vilipiganwa huko Liwale, Nachingwea kati ya wapiganaji wa maji maji na majeshi ya wajerumani. Vita hiyo ilipiganwa kufuatia kushambuliwa kwa boma ya wajerumani ya Liwale.
Septemba mosi, kitete kiliwapanda wajerumani maana mashambulizi ya wazalendo yalikuwa makli san asana sana, hivyo wajerumani walipiga simu nyumbani kwao ujerumani wakiomba majeshi ya ziada ili kuzatiti mapambano yaliyokuwa yakiendelea.

Chanzo kikuu: Mwanahistoria J. E.  Makaidi.


SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP