Pekua/search

Saturday, January 28, 2012

'CHADEMA WAMESABABISHA MGOMO WA MADAKTARI'

"Taarifa za kiintelijensia zimebaini kuwa Chadema ndio wamesababisha
mgomo wa madaktari, mgomo ambao umeendelea kwa siku kadhaa sasa na
umehatarisha maisha ya wagonjwa wengi na umesababisha hata madaktari
kuvuana uwanachama kwenye chama chao cha madaktari. Chadema ndio hao
hao wamekuwa wanaratibu migomo mingi kwenye vyuo vikuu, ndio haohao
wameratibu mgomo wa madereva wa maroli kule mbeya lakini pia ni
Chadema walio hakikisha na naibu waziri wa Afya anagoma kwenda kuonana
na madaktari pale kwenye ule ukumbi walio andaa wao maana protokali na
usalama wake ulikuwa hatarini.

Hawa Chadema hawafai maana wanataka nchi isitawalike, Wanafanya haya
wakijua kuwa raisi JK yuko kwenye mkutano wa uchumi duniani na kule
anakutana na kuongea ikiwa ni pamoja na kupiga picha na Bill Gates na
matajiri wengine wa dunia ili watusaidie kujikwamua kutoka kwenye
mkwamo wa njaa na uchumi mbovu. Chadema ndio hawahawa wamesababisha
sasa hivi shilingi yetu imeshuka thamani maana muda mwingi wanautimia
kuwasumbua watu waliokuwa wanajua matumizi ya shilingi na sasa
wamekasirika na matokeo yake shilingi imeshuka thamani.

Chadema ni watu wabaya sana maana baada ya mgomo huu wa madaktari
wataandaa mgomo mwingine waliouahirisha na walimu mwaka jana,
wanachowaza Chadema ni Migomo tu ili serikali idorore na nchi
isitawalike, Chadema ni chama cha fujo na maandamano, wamewezesha
mgomo mpaka ndani ya ccm na kusababisha wale makada wenye magamba
kugoma kuvua magamba yao! Hiki chama ni kibaya sana ndio maana
kimemtuliza hata yule Aminiel Mahimbo aliepokwa my wife wake na jamaa
anae walaza macho magamba.

Watanzania mtambue kuwa chadema ni chama kibaya sana maana ndio
kimesababisha minong'ong'o eti Dr Mwakyembe amewekewa SUMU! Nani
amuuwe Mwaki?! Mwaki hana tatizo kubwa anaugua tu mafua na hata ripoti
yake ni chadema haohao ndio wameizua maana wanajua kuwa ikiwekwa
hadharani ataleata tena mambo yake yenye harufu ya ki richmond,
chadema watu wabaya sana maana wamesababisha maisha magumu kwa kila
mtanzania, chadema wamesabibisha mpaka umeme unagoma mara kwa mara.
Tusiwaamini watu hawa maana wanataka kuiondoa serikali iliyoko
madarakani kwa maandamano.

Hii ni siri yako! Hata yale mafuriko yaliyosababishwa ndugu zetu
kuhamia kwenye majumba ya nguvu kule ma bwe pande ni jamaa hawahawa
wakiongozwa na makamanda wao. Hawa jamaa ni nuksi."

Mohamed Mtoi kutoka jukwaa la Wanabidii


KUSOMA MJADALA JUU YA MADA HII KWENYE FACEBOOK Bofya HAPA

Saturday, January 14, 2012

ECONOMIC CRISIS ISN'T A MUST TO TANZANIA.

"...a minister travels from Dar es Salaam to Washington DC, the government pays up to $20,000 for his/her first class ticket while an assistant’s business class ticket costs around $10,000. Shockingly, economy class costs roughly $2,000. So we pay $30,000 for two persons to fly to Washington instead of $4,000. If the Swedish ambassador can fly economy class, why can’t our officials do the same?" Mobhare Matinyi.

To read the full article on Citizen click HERE

Monday, January 9, 2012

Leo (Januari 9) katika Historia yetu - ISIKE MKASIWA ALIJIUA

Leo (Januari 9) katika Historia yetu:
Mwaka 1893 - Shujaa wa Kinyamwezi Isike Mkasiwa, alijiua kukwepa fedheha ya kusalimu amri kwa Wajerumani katika vita ya kukataa kutawaliwa na wageni.
Kufuatilia na kuchangia mjadala kwenye fesibuku tekenya HAPA

Saturday, January 7, 2012

LEO (January 7) KATIKA HISTORIA YETU (our history)

Leo (Januari 7) katika Historia yetu:

Mwaka 1938- Wilaya ya Pangani mkoani Tanga ilizinduliwa

Mwaka 1958 - John Williamson, Mkanada 'aliyegundua' almasi huko Mwadui Shinyanga alifariki dunia na kuzikwa huko huko Mwadui.

KUSOMA Kweny facebook bonyeza HAPA
Au kiunganishi http://www.facebook.com/photo.php?fbid=3052852440994&set=a.1455905638322.64825.1253767086&type=1&theater

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP