Pekua/search

Sunday, January 17, 2010

he is an american - he must be loving tanzania; more than you?


MGENI ANAPOTUZIDI UZALENDO
Na Mch. Emmanuel Bwatta - University of the South, Tennessee, USA.

Mwenye hii gari ni Mmarekani na mwanafunzi wa uchungaji hapa ninaposoma. Alikuja Tanzania (Arusha) June mwaka jana. Nilivutiwa jinsi anavyoonyesha kuipenda Tanzania labda kuliko sisi wenyewe. Nadhani hiiyo picha ni kielelezo tosha.

Friday, January 8, 2010

TANZANIAN KIND OF POLITICS; ONLY THAT THEY ARE IMPOTENTNi kkatika halmashauri ya wilaya ya Arusha mkoani Arusha, Tanzania

Inakuwa vipi wasiokuwa wana CCM wakienda kujitafutia riziki hapo?
Je wakereka hawa, wamefungua tawi hili kwa vile wanakipenda CCM au walikuwa wanatekeleza usemi maarufu wa SUMAYE, F, waziri mkuu mstaafu, "Ukitaka mambo yako yaende sawa, weka bendera ya CCM" Msemo ambao ulishuhudia majambazi yakipita polisi pasipokusimamishwa kisa? wanapeperusha bendera ya CCM.

Sunday, January 3, 2010

old ways of celebrating christmas on extinction - are new ones any better?Mambo ya kusangula - a way to celebrate Christmas that is now on the edges of its extinction in Rungwe Tanzania marking the end of 'those golden old days!'

By Baraka Herbart - recently in Lwangwa Tukuyu - Tanzania


'Kusangula' ni moja kati ya matukio yenye mvuto wa aina yake ambayo mara nyingi hufanywa na vijana na watoto wa kwetu hasa nyakati za sikukuu za krismas na mwaka mpya!

Kundi la vijana na watoto wake kwa waume hupita nyumba kwa nyumba wakiimba na kuserebuka 'nyasima kapapike napile imbange...eeh hodi hodi..'! Wakifika kwako,unatakiwa kuwapa japo zawadi ndogo ndogo tu kama hindi,ndizi au hata vijisenti kidogo!Lakini si lazima sana kama huna!Wao huenda kugawana!Hawa hunogesha kijiji kizima kwa mirindimo ya shangwe,vifijo, nderemo n.k!Acha tu!

Leo hii hawapo tena!Utandawazi! Vijana wapo 'mageto' na 'vimwana' wao na watoto nao wamekaa masebuleni 'wakikodolea' Tv!Kijiji kimya,utadhani hapana sikukuu!Ukibahatika kuwaona ni kama hawa wachache wamekuja nyumbani kwangu,nawapa vijisenti kidogo!Mara nao wametokomea, hawapo!Kumbe ni wale wale 'wajasiriamali' ,ambao wanatafuta namna baada ya kuganga na kiu ya 'kalita'!!Hatimaye nawakuta wamejipumzisha 'Kipangamansi' ,moja ya vilabu vya pombe maarufu sana hapa Lwangwa!Nadhani ni baada ya mifuko kunona!Tamaduni hizi zaelekea kwisha!!!

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP