KUMBE KINGUNGE NGOMBALE-MWIRU ANA UMRI WA MIAKA 40 TU!!
Jamani eeee
Eti Kingunge Ngombare-Mwiru (pichani kushoto) alizaliwa mwaka 1969!!!!
Kwa sababu ndogo ndogo tu limenijia wazo kujua umri wa Kingunge, pengine ili kutaka kumtendea haki (kkatika mjdala unaoendelea kuhusu waraka wa kanisa katoliki).
Mahali pa kuanzia nimeenda website ya Bunge, nikiamini ni chanzo cha kuaminika cha taarifa.
Niliyoyakuta huko, mh ndo hayo, eti date of birth ya Kingunge, mbunge wa kuteuliwa na rais ni 31 Dec. 1969!!! soma hapa au fuata kiunganishi hiki: http://www.parliament.go.tz/bunge/mpcv.php?vpkey=201#. Zaidi ya hapo kila kiashiria cha umri wa Kingunge kimeachwa wazi, mfano, zimeorodheshwa nyadhifa zake, lakini alianza lini hadi lini, ama alisoma au kuhudhuria mafunzo lini hadi lini, hakuna kinachooneshwa wala kuelezwa. Jambo hilo linafuta akilini mwangu kwamba kuandikwa mwaka 1969 kuwa ndipo alipozaliwa mhe. Kingunge, si bahati mbaya. Utani huu, unalenga kumnufaisha na????? Na kama ni kukosekana kwa umakini kwa watendaji kadhaa wanaohusika na ukurasa huo wa Bunge, TANZANIA ITAISHIA WAPI???kwanini umri wa Kingunge ni issue, hata ufichwe au ufanyiwe usanii???
Nawasilisha
3 comments:
Kwanza nikupongeze kwa udadisi wako uliokufanya ukagundua kuwa Mzee Kingunge ambaye kila Mtanzania anamfahamu kama mzee aliyeshiba miaka ana miaka 40.Hiyo nafikiri siyo issue ndogo. kwanza kwa sababu ya heshima ya mzee Kingunge mwenyewe, pili kwa sababu ya heshima ya tovuti ya Bunge. Mimi naamini kuwa tovuti ya bunge ni tovuti yenye heshima kubwa na kila kitu kinachowekwa humo ni lazima kiwe kimechujwa kikamilifu na kiwe cha kuaminika.Kama taarifu za tovuti ya Bunge zitakuwa zinapingana na hali halisi huoni kuwa inaleta picha mbaya kwa bunge lenyewe kwa ujumla wake? Hata mtoto mdogo akiona picha ya Mzee Kingunge atakuambia Kingunge anakaribia miaka 100.Iweje leo awe na miaka 40? Je, wale wanaoshughulikia maswala ya bunge na kuamua tu kuweka habari ambazo siyo za kweli kwa sababu wanazozijuwa wenyewe kwenye tovuti hiyo inayowakilisha sura ya taifa letu tuwaweke kwenye kundi gani? Hii inatisha, nchi yetu imekosa umakini katika kila nyanja. Hapa sasa tunaelekea pabaya. Na kama watasema umri wa Kingunge ulikosewa, vipi taarifa zake nyingine ambazo hazionyeshi miaka hata moja nayo ni bahati mbaya? Hili linafanywa kwa maslahi ya nani? Tutaaminije kuwa taarifa nyingine nyeti zilizoko kwenye mtandao huyo kuwa ni za kweli? Kwa mtizamo wangu hii ni kashifa kubwa kwa Kingunge mwenyewe, bunge letu na nchi nzima kwa ujumla. Nafikiri sote tunapaswa kuwajibika. Sote tunapaswa kujiuzulu kuanzia Rais hadi yule asiye na ajira. Najua unaweza kuniuliza kuwa yule asiye na ajira atajiuzulu nini. Lakini jibu ni rahisi tu kuwa huyu asiye na ajira ndiye aliwaajiri hawa wanaofanya mchezo na ofisi nyeti.Ulipomchagua Rais ndipo ulipomteua Kingunge kuwa mbunge wa kuteuliwa na hivyo ulichangia kuweka taarifa zake zisizo za kweli kwenye tovuti yetu sote. Rais alipomteua katibu wa bunge au yule nayemteua katibu wa Bunge na wewe ulihusika. Ulipomchagua mbunge wako ndipo ulipochangia kutumi vibaya tovuti ya bunge. Kwa hiyo sote tunawajibika hivyo tunapaswa kuachia ngazi.(Tafadhali soma katikati ya mistari).Sasa Kingunge anaposimama bungeni na kushambulia waraka ulioandaliwa na kanisa Katoliki kwa ajili ya kuwaehelimisha wananchi ili waweze kuwajibika katika kuchagua viongozi wanaowajibika hayoni kuwa yeye andiye wakulamiwa pamoja na wenzake wasiwajibisha kutengeneza jamii ya Watanzania waadilifu? Kingunge anapowashangaa maasikofu kwa kumwita fisadi(Tanzania Daima ya Alhamisi 23, 2009 uk.1 toleo Na.1693) hayoni kuwa yeye ni fisadi wa kuficha umri wake wa kweli? Je, huko siyo kugushi? Kama ameweza kuwa fisadi wa kudanganya umri hawezi kuwa fisadi wa mambo mengine? Napendekeza kuwa wembe uliomnyoa Kiiyo aliyewahi kuwa mbunge wa Temeke umnyoe na Kingunge pia.
Naomba kuchangia!
Elias Loidiso
Uchunguzi zaidi Uonaonesha kuwa waheshimiwa wabunge waliozaliwa tarehe moja (Desemba 31, 1969)kwani pamoja na Kingunge, waheshimiwa Rostam Aziz, Yusuf Makamba,Rostam Aziz,na John Cheyo!!! Haingii akilini kwamba waheshimiwa hawa wooote wana umri wa miaka 40 leo hii. Na kama ni utani basi umekiuka mpaka, kama ni uzembe basi ni ule uliotopea!!
Kwa mikogo na mbwembwe Tumezindua mkongo wa mawasiliano wa chini ya bahari hivi majuzi, je tutafaidi lolote???? Kama hatupati vitu vya uhakika kwenye tovuti ya bunge, kwanini watu walaumiwe kwa kutembelea ze utamuz mara nyingi zaidi kutokana na kuwa ya kisasa kila kukicha inakuwa na vitu vipya??
Tazama, kwa mfano mbali ya mheshimiwa cheyo kuelezwa kuwa na umri huo 'uliokosewa', bado hakuna taarifa zake zozote kuhusu elimu ama ajira!! je amekataa kutoa taarifa zake? Je kama public figure, anayo hiari hiyo?
Mungu tunusuru!!!
Kwa watanzania tulio wengi ,umri huwa ni siri .Wengi wetu hatupendi umri wetu ujulikane kwa watu.Hivyo basi inawezekana mhusika anafahamu kuwa taarifa zake zimekosewa lakini akaamua kukaa kimya.Mi nafikiri babu KNGUNGE kuwa kijana kiasi hicho ni masihara.Kuna watu ambao wanaweza wakadanganya au hata kukadilia umri wao na jamii ikaamini lakini sio babu yangu Kingunge.
Nafikiri inapendeza unapokuwa kiongozi au mtu maarufu ukawa muwazi ili linapotokea tatizo watu wakuhukumu kulingana na umri wako kwani wakati mwingine unaweza ukafanya jambo watu wakaona umekosea kumbe jambo hilo katika umri huo hi kitu cha kawaida.
Tumezindua mkongo wa mawasiliano kwa ajili ya kutuma na kupokea habari,sasa kama habari tunazopokea na kutuma si sahihi tunapelekana wapi?Kuna haja gani ya kusoma habari ambazo zimepotoshwa?kwanini zipotoshwe?kwa faida ya nani?
Post a Comment