Kabla ya Mwaka 1920 Hakukuweko na nchi ikiitwa Tanganyika
Kabla ya Mwaka 1920 Hakukuweko na nchi ikiitwa Tanganyika
"Kwa kuwa chini ya utawala wa Kijerumani Tanzania Bara iliitwa Deustche Ost- Africa,
ilikuwa lazima Waingereza kutafuta jina lingine mara baada ya kushika utawala.
Awali katika mwaka 1920, yalipendekezwa majina kadhaa, yakiwemo, “Smutsland”, “Ebumea”,
“New Maryland”, “Windsorland”, na “Victoria”, ambayo hata hivyo yalikataliwa yote
na Serikali ya Uingereza kutokana na sababu mbalimbali.
Baadaye serikali ya Uingereza ilielekeza yapendekezwe majina ya kienyeji, ndipo
yakajitokeza majina “Kilimanjaro” na “Tabora”, ambayo yalifikiriwa lakini hayakuchaguliwa.
Hatimaye jina “Tanganyika Protectorate” lilipendekezwa na msaidizi wa Makoloni na
likakubaliwa na Serikali. Inafahamika kwamba, kabla ya ujio wa wageni kutoka Ulaya,
wenyeji katika maeneo ya Magharibi mwa nchi waliliita ziwa kubwa lililopo eneo hilo
“Ziwa Tanganyika”. Inaelekea hiyo ndiyo sababu kubwa iliyofanya maofisa wa serikali
kulikubali jina la Tanganyika kwa sababu lilikidhi matakwa ya sera kwa kuwa lilitokana
na majina ya kienyeji.
Halimaye neno “Protectorate” liliondolewa kutoka jina rasmi la ‘Tanganyika Protectorate’,
na badala yake likawekwa neno “Territory”.
Kwa hiyo, kuanzia mwaka 1920 hadi uhuru nchi ikajulikana kama “Tanganyika Territory”."
Nimeibeba kutoka http://www.ijuetanzania.co.tz/ tovuti iliyosheheni mambo mengi muhimu kuhusu Tanzania na historia yake.
Heri ya siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania tunayojivunia kuwa wana wa nchi.
0 comments:
Post a Comment