NAFASI ZA MASOMO YA KOZI ZA UALIMU- Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira Tawi la Mbeya
CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA - TAWI LA MBEYA
S
L P 3040, MBEYA
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO YA KOZI ZA UALIMU
Chuo Kikuu
cha Tumaini Makumira Tawi la Mbeya ambacho awali kilijulikana kama Mbeya Lutheran Teachers’ College kinatangaza nafasi za masomo ya kozi ya Ualimu Ngazi ya Cheti,Stashahada na Shahada katika mwaka wa
masomo 2013/2014.
1.
Sifa za Mwombaji
a)
Ngazi ya Cheti
i.
Mwombaji
awe amefaulu mtihani wa kidato cha Nne kwa kiwango kisichopungua daraja la nne
alama ishirini na saba (27) katika mkao mmoja.
ii.
Awe
amehitimu Elimu ya Sekondari siyo zaidi
ya miaka mitano iliyopita.
b)
Stashahada
i.
Mwombaji
awe na ufaulu wa principle moja na Subsidiary moja katika masomo
yanayofundishwa Shule za Sekondari. AU
Awe na Cheti cha daraja la
tatu A chenye ufaulu wa wastani wa B
au “Credit na Distinction”. AU
Awe na cheti cha daraja la
Tatu A na uzoefu usiopungua miaka mitano kazini.
Angalizo:Waombaji wote wanaotumia
cheti cha Ualimu Daraja la Tatu A wanatakiwa kuwa na
ufaulu
usiopungua “D” Tano katika mtihani
wa kidato cha Nne.
c)
Kwa muombaji wa Shahada
(Degree) tembelea tovuti ya TCU na chagua TUMA-MBEYA yenye code number MKM01 AU
MKM02.
2.
Namna ya kutuma maombi.
(a) Fomu za maombi zinapatikana
katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira
tawi la Mbeya kilichopo Uyole. Au tembelea katika tovuti yetu www.shuco.ac.tz.
(b) Mwombaji anatakiwa alipie Tshs. 30,000/= kama gharama za maombi katika
akaunti namba:
ELCT-MLTC
Computer Building Project (CRDB): 0152421083000
(c) Barua iambatanishwe na Vivuli vya Vyeti vya kuhitimu Elimu ya
Sekondari na Chuo.
(d) Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wawasilishe Vyeti vya Baraza la
Mitihani la Tanzania ili
vipatiwe utambulisho (kupasishwa).
(e) Hati halisi ya malipo (Pay in Slip) iambatanishwe kwenye barua
ya maombi.
3.
Muda wa mafunzo
Kozi ya Cheti na stashahada
zitatolewa kwa muda wa miaka miwili na kwa kozi za shahada ni miaka mitatu.
KWA
NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA MASOMO YATAANZA RASMI TAREHE 08/07/2013
4.
Maombi yote yatumwe kwa
Mratibishaji wa masuala ya
Taaluma
Chuo Kikuu Tumaini Makumira
- Kituo cha Mbeya
S.L.P. 3040
MBEYA.
Simu
no: + 255 25 2510450
+255 0655 858 527/+255 753 817 274
Nukushi:
+ 255 25 2510094
Tovuti:
www.shuco.ac.tz
Barua
pepe: tumashuco2012@gmail.com