Pekua/search

Saturday, June 6, 2009

TUJADILI LUGHA YA KUFUNDISHIA TANZANIA

Tangazo la Hakielimu gonga hapa kuhusu lugha ya kufundishia, kila ninapolisikiliza, linasema mengi kwa muda mfupi sana.Binafsi nalikubali sana kwa uzoefu wangu kama mwanafunzi na kama mwalimu pia. Tunakaririshwa tunaenda kukaririsha. Na kwa mantiki, mchakato wa kujifunza na kufundisha hapa kwetu unahusu zaidi kufasiri kutoka Kiingereza kuwa kiswahili. Suala hilo linakwamisha sana kujengeka kwa uelewa unaoweza kuchochea na kurahisisha uhawilishaji wa maarifa yanayopatikana darasani kwenye muktadha mwingine. JE TUTAFIKA? TUENDELEE NA ZEE, SAMBADE GESHI,.. GLOBALI WOMING....???UNASEMAJE? TOA MAONI

4 comments:

Anonymous June 6, 2009 at 4:52 AM  

Hii haifai haifai haifai wala sijui nisisitize vipi. Kutumia lugha mbili ni kuchanganya mwanafunzi kabisa na kupunguza kasi ya kuelewa somo. Inabidi kusoma na kutafakari kwa KiSwahili kwanza ndipo kutafsiri kwa lugha ya Kiingereza tena neno baada ya neno. Nadhani elimu ya Tanzania ibadilike na wanafunzi waanze kufundishwa kwa lugha ya Kiingereza (au lugha yoyote iliyo mali katika ulimwengu wa sasa). Itawezekana ikiwa Waalimu watapigwa msasa wa lugha ya Kiingereza na kutakiwa kuitumia lugha hiyo. Kwa sasa hatuwezi kujidai eti mbona WaChina, Wafaransa, WaJapani nk wanatumia lugha zao wakati tunajua fika kuwa lugha ya Kiingereza haipo katika mitaala yao, ukiitaka inabidi kwenda kwenye shule za lugha hiyo. Sisi tunakumbatia Kiingereza na tumeiweka lugha rasmi ya kiofisi lakini hatuitumii ipasavyo. Tusitupe KiSwahili lakini tutilie mkazo Kiingereza hadi hapo baadaye.

Haulle June 6, 2009 at 6:44 AM  

mambo magumu sana hapa bongo, tunajifunza lugha ya kabila letu kikerewe, kikisi, kimakonde,kipare, nk kabla ya kuanza shule, then twajifunza kiswahili hadi la saba then kiingereza, ukiangalia kwa makini, mengi ya O-level yanakuwa ni kufasili kiswahili kwenda kiingereza (yaani yale ya shule ya msingi) kutoka hapo ni kukariri mtindo mmoja, nafikiri unafiki ndio unao tuweka hapo, Je wakumbuka Sumaye waziri mkuu ana sema Ningependa Kiswahili kiwe lugha ya kufundishia, huku waziri wake asema kiingereza kiwe hadi primary (Mungai)halafu ni waziri wa utamaduni pia. sumaye ndo mtendaji anonekana hana maamuzi, nani ataamua? achana na kufikiria tume ya Makweta mapema miaka ya 80, unafiki mwingi mmno bongo.... Tutafika?????? haulle

Chambi June 7, 2009 at 12:12 AM  

Dada Subi kuna tofauti kati ya kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia na kutumia Kiingereza kama lugha ya mawasiliano. Tunatakiwa kuzingatia hilo la pili kwa kufundisha Kiingereza kama lugha ya pili kama hizo nchi zingine zinavyofanya ilhali zinatumia lugha zao kufundishia. Hali ilivyo sasa Tanzania tunakosa yote kwa sababu tunafundishia lugha ambayo hata hatuijui vizuri kuitumia kuwasiliana. Kama anavyosisitiza Dakta Qorro, tufundishe vizuri Kiingereza kama lugha na tutumie Kiswahili kama lugha ya kufundishia.

Adam June 11, 2009 at 10:09 AM  

Mjadala unapamba moto, usipitwe. soma mjadala ufuatao kama unavyoendelea kwenye wanazuoni yahoogrou.SOMA. CHANGIA.

FUATILIA HAPA:

Idd hicho kisingizio tumekitumia kwa muda mrefu wakati hali inazidi kuwa mbaya. Kama Rais mwenyewe anahutubia Taifa kwa Kiswanglishi na kama Walimu wenyewe wanafundishia kwa Kiswanglishi kwa nini tunajidanganya kuwa lugha tunayofundishia ni Kiingereza na kuwa ni gharama sana kufundishia kwa Kiswahili? Hoja inayotolewa na watafiti wa hili suala sio ya kukitupa pembeni Kiingereza na kutumia Kiswahili 100%. Hoja yao ambayo nakubaliana nayo kwa 100% ni kuwa tutumie lugha inayoeleweka na inayotumiwa zaidi mitaani na majumbani kufundishia wanafunzi ili waelewe vizuri kile wanachofundishwa. Na wakati tunafanya hivyo ili kupata elimu, ujuzi na maarifa basi pia tufundishe lugha ya Kiingereza vizuri ili watu waweze kuitumia kama inavyotakiwa. Hali ilivyo sasa inatisha. Ukipata muda pitia ripoti na insha zinazoandikwa na wahitimu wetu na hata walimu na wahadhiri wetu uone jinsi ambavyo tupo katikakati - Kiingereza hatukijui vizuri na Kiswahili tunakijua kidogo. Saa huu unusunusu/undumilakuwili unamsaidia nani?


Subject: Re: [wanazuoni] TUJADILI LUGHA YA KUFUNDISHIA TANZANIA


Nadhani wengi tunazunguka mbuyu, swala la muhimu ni mmoja tuu. Jee tunao wataalamu wa kutosha kwenye kila sector ambao watasaidia hiyo transformation? Jee tunazo tools za kutosha?

Kwenye maswala ya science ndiko ambako kazi ipo, jee tunazo nyenzo za kutosha kufundishia masomo kama fizikia, kemia na biologia? Kama wakufunzi wenyewe wamesoma kingereza mpaka mwisho, jee wataweza kuwa effective kwenye kutransform?

Na mwisho? Jee ni benefit gani as a society tutapata kwa kuapply kiswahili 100%


fuata kiunganishi kifuatacho kwa michanzo zaidi
http://groups.yahoo.com/group/wanazuoni/message/3776

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP