Pekua/search

Wednesday, September 9, 2009

RAIS WA WATU ALIPOZUNGUMZA NA WANANCHI

Naam tarehe 9.9.09 Rais kazungumza na wananchi kwa kujibu 'maswali yao'. Hakika Rais wetu alikuwa na bahati saana kuulizwa maswali kuhusu masuala ambayo Rais yeyote wa watu angepennda kuyazungumza kwenye hotuba yake, hata kama hakuulizwa na wananchi wake 'wanaompenda sana.'

Suala la kuziba midomo watu kwenye vikao vya chama chake, suala la mikoa iliyopembezoni, suala la ufisadi, suala la mtikisiko wa muungano, nyaraka za madhahebu ya dini nk ni masuala yanayosumbua nafsi za watu, na kwa kweli wauliza maswali walilenga!!!!!!

Yaliyonigusa:
Rais 'anaijua' tanzania kweli kweli maana ameweza kuzungumzia barabara zinazojengwa kwa urefu, kiasi cha pesa, mkandarasi, nk utadhani waziri wa ujenzi!!Rais amezungumzia takwimu za elimu mwaka kwa mwaka, mwaka hadi mwaka utadhani waziri mwenye dhamana ya elimu, au hata zaidi yake. Hakika mheshimiwa rais ALIJIANDAA. CONGS

Kwa kusikiliza na kutafakari majibu ya rais kuhusu nyaraka na miongozo ya madhehebu ya dini nashindana na nafsi yangu kuamini kuwa 'Waislam', na askofu Kakobe walipangwa au walitumwa kuyazungumzia kwa mtindo wa Yohana mbatizaji. Hajaeleza kwa kina mathalan, ni vipi waraka wa katoliki unakuwa issue ya kuhatarisha amani, maana hauelekezi dini ya mtu wa kuchaguliwa. hajaeleza kwa kina hofu inatoka wapi?

Rais walau ametueleza kwa kina kuhusu kikao cha CC na NEC ya CCM na kutuahidi kuwa kwa nafasi yake ya uenyekiti wa chama hicho HATARUHUSU WATU WAZIBWE MIDOMO, na kwa mtazamo huo ataendelea kusimamia wajibu wa wabunge wa chama hicho kwa wananchi zaidi si matakwa ya chama chao pekee.

Hata hivyo mwenyekiti huyo wa CCM hakuzungumzia ni Mshindani wa Spika wa sasa kwenye kinyang'anyiro cha nafasi hiyo, yaani Msekwa awe mmoja wa wazee wa kutafuta ufumbuzi wa mkanganyiko ndani ya chama, Je CCM imeishiwa wazee?

Kuhusu ufisadi, pamoja na kuwa amejitahidi kuzungumzia kuandaliwa kwa mfumo wa kisheria wa kuwabana mafisadi, hajaeleza mathalan kuhusu tuhuma za mapambano ndani ya chama hicho, ambapo baadhi ya vigogo wanatuhumiwa kutumia mijihela kuwakandamiza wenzao.

5 comments:

Anonymous September 11, 2009 at 12:22 AM  

niliona swali ukweli wa kuongozwa lakini nilishangazwa na suala la muungano na mafuta ambapo ajibu .... kupunguza masuala ya muungano sio tatizo, tatizo kidogo litakuwa kuvunja muungao..
Maoni yangu nikuwa ni jibu la kisiasa zaidi, hivi ukiamua kupunguza au kutoa mambo ya muungano yaliyopo hadi ikafikia kuwa na 12, (hapo hakuna tatizo) then ukaendelea hadi 1 then utaoa moja toka ktk moja (siotatizo) utakuwa na muungano? wanamahesabu wataniambia upo ambao ni empty set, au 0 hayo ni majibu ya Rais kimaana.
Chapili suala la muungano ni suala wa watanzania Leo watanzania wakitaka kuvunja waruhusuni ni wao. kama nyerere alivyo sema uvunjeni tu ila kubalini athari zake.
mulionaje wenzangu?

HAULLE, Evaristo
chanzo: wanazuoni yahoogroups

Anonymous September 11, 2009 at 12:23 AM  

Japo wazo la kuulizwa maswali moja kwa moja ni zuri, lakini mimi naona Rais alichokifanya ni kurudia taarifa zinazojulikana (repeating known facts). Pili Rais alishindwa kuonyesha ni wapi yeye ana maono ya kupeleka nchi (Strategic Vision of the Country).
Tatu, Rais kama mkuu wa kaya anasema kwamba mpaka Waziri Mkuu na Makamu wa Rais warudi toka safari ndio atakaa na viongozi wa dini kujadili swala la nyaraka/ilani. Je bila wasaidizi wake yeye anashindwa nini kuendelea na haya mzungumzo?

Adam Jackson Foya
wanazuoni yahoogroups

chams September 11, 2009 at 2:34 AM  

majibu ya rais yalikuwa ya kisiasa zaidi.Nimesikitika sana Rais kutoshughulikia swala la walimu kwani hakusema ni lini walimu watalipwa malimbikizo yao. Rais anaungana na Waziri wake kuwadanganya walimu.In short hakukuwa na jipya katika maeleza yake zaidi ya kutoa ahadi zaidi.Mbona hakuzungumzia tatizo la umeme Songea na ahadi aliyoihadi ka wakazi wa mkoa ambayo imempa wakati mgumu Christine Ishengoma asijue nani wa kumbana.NIONAVAVYO MIMI KIKWETE AKIKUWA ANAFANYA UPIMAJI NA TATHIMINI

Adam September 11, 2009 at 5:02 AM  

Shukrani kwa mchango wako Chams. Nimefurahia kuusoma kutoka kwako tena. Hakika Tanzania tuna kazi. Labda wananchi tuamke, tujazibike na kukasirika. Umeona watu wanavyomfagilia mhe. rais? Kaazi kweli kweli. Tumheshimu Rais wetu, sawa, lakini tusiwe rahisi kukubali tunapofanywa mazuzu, nadhani.

Anonymous September 11, 2009 at 5:17 AM  

Kaka Adam Foya

hata kama hoja lazima wote watatu wawepo sawa Je kwani ishu yenyewe imetokea leo? nafikiri ni zaidi ya miezi miwili sdasa. je mkuu wa kaya anataka kusema wasaidizi wake hawapo nchini kwa muda wote huo? labda usanii unazidi, amesahau hata kama kuna uchaguzi oktoba hii.
any nation without vision will perish
nakubaliana na mzee Adam Foye yeye kajibu kama mwana kijiji tu kimsingi hakukuwa na jipya tulimfikiria yeye kuzungumzia vitu vya kisera zaidi, ishu mkukuta hata kama hatuupendi anafikiria mkakati gani wa muda mrefu? mkukuta waisha mwakani
any way tutafika tu tukiwa tumechoka,taabani, mahututi au maiti
Haulle
WANAZUONI YAHOO GROUPS

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP