RAIS WA WATU KUZUNGUMZA NA WANANCHI
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120 ,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kesho, Jumatano, Septemba 9, 2009, atazungumza moja kwa moja na wananchi kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na vyombo vingine vya utangazaji nchini kuanzia saa mbili na nusu usiku. Mbali na TBC, televisheni nyingine za ITV, TVZ, Mlimani TV, Tumaini TV na Channel Ten zinatarajia kuonyesha mazungumzo hayo.
Rais atatumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali yao , kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa nchi yetu, Serikali yetu na maendeleo yetu.
Aidha, Rais atasikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.
Mazungumzo hayo yatakayochukua muda wa dakika 90 kuanzia saa mbili unusu usiku (saa 2:30 usiku) hadi saa nne kamili usiku.
Aidha mazungumzo hayo yatatangazwa kwenye redio za TBC-Taifa, Sauti ya Tanzania, Zanzibar, Radio Mlimani, Radio Clouds, Radio Tumaini, na Radio Uhuru.
Maswali, maoni, hoja, ushauri utapokelewa moja kwa moja na TBC kupitia simu nambari +255-22-2772448, +255-22-2772452 na +255-22-2772454.
Aidha, maswali, maoni, hoja ama ushauri unaweza kutumwa moja kwa moja TBC kupitia ujumbe mfupi wa SMS kwenye nambari 0788-500019, 0714-591589 na 0764-807683 ama kupitia kwenye barua pepe swalikwarais@yahoo.com kuanzia leo.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais inawashauri wananchi kutumia kikamilifu nafasi hiyo ya kuwasiliana moja kwa moja na Rais wao.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
08 Septemba, 2009
CHANZO:
www.wanabidii.net
3 comments:
Afadhali amejitokeza hadharani tumkumbushe mambo mengi aliyotuahidi kabla na baada ya kuingia madarakani.
Hakika ndugu. Kwa kweli watu wengi wakijitokeza kuuliza maswali yenye 'akili' itakuwa safi. Nadhani si wakati wa kupiga ramli kuhusu kushindwa kwake kujibu maswali.Vema tuulize na vema tusikilize kwa makini majibu yake, tubaini nia yake has ya ndani ya kujimwaga hadharani. Kwa sasa wacha na tumpongeze kwa kujitoa kimasomaso kukabili 'hasira' ya umma.
Naupongeza uamuzi wa JK kuhutubia wananchi na kisha kupoke maoni na maswali yao kwa njia ya simu. Ukiungalia kwa haraka haraka uamuzi huu au wazo ili ni kama mbinu ya kuimarisha utawala bora. Lakini tujiulize maswali ya msingi, je, ni kweli kwa kipindi chote cha uongozi wake Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete asikii maona, kero au maswali ya wananchi? na je ameshughulikia kwa kiasi gani? je ni dalili kuwa taasisi zilizo chini ya rais kushughulika na kero za wananchi zimeshindwa kazi? wawakilishi wetu hawafikishi ujumbe toka kwa wananchi?
Naingojea kwa amu kubwa hiyo saa mbili na nusu kushauhudia kitakacho tokea, japo si jambo jipya kwa kiongozi mkubwa wa nchi kusikiliza kero za wananchi wake kupitia simu. Kwa wanokumbuka mwaka mmoja uliopita Gordon Brown waziri mkuu wa Uingereza alikua amejiweke utaratibu wa kupokea simu za wananchi wake nusu saa kabla kuingia kazini katika siku tano za juma, hii haikua ikionywesha moja kwa moja na vyombo vya habari. Lakini hii yetu itakua ukishuhudiwa na wananchi wengine. Haya ni maendeleo makubwa sana japo inanikumbusha kisa cha mfuga mbwa aliamka usiku na kuanza kubweke mwenyewe na kuwaacha mbwa wake wakimshangaa.
Post a Comment