Pekua/search

Wednesday, September 29, 2010

HELKOPTA, MIJIGARI, MBWEMBWE NA TAMBO ZA KAMPENI MSIBANI

Ukishuhudia mbwembwe na tambo wakati huu wa kampeni,
Ukiona mijigari mikubwa ilosheheni,
Na helkopta zikipasua mawimbi angani,
Picha za helkopta kutoka blogu ya mzee wa matukio
utaamini bila kudhani,watanzania twaishi peponi.


Ukiona tunavyoshangilia,
kwa mayowe na nderemo tukishabikia,
makofi ya uzito tukiwa pigia,
Utaamini sio sisi kila uchao tunaolia.Kama kawa kura tutawapigia,
Kisha tutaendelea kuwatumikia,
maana sisi zumbukuku tulopindukia,
Kutenda si yetu ada bali kulia

.

1 comments:

Anonymous October 4, 2010 at 11:44 PM  

Yes tumelogwa
Tukalogeka
Tumepumbazwa
Tukapumbazika

Hawatuambii ni bei gani
Kuyaweka hayo madege juu,
Ngoja tuendelee kushangilia
Ndilo tulijualo

Na Asifiwe

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP