Pekua/search

Monday, September 6, 2010

'TUNAMHITAJI SLAA KWA SABABU YA KICHWA CHAKE, SI KWA VIUNGO VYAKE VYA UZAZI'

'TUNAMHITAJI SLAA KWA  KICHWA CHAKE, SI KWA VIUNGO VYAKE VYA UZAZINa Ansbert Ngurumo

Naandika kukosoa dhana ya wale wanaopotosha ukweli juu ya upadri wa Dk Slaa.

Ameshasema mara kadhaa mbele ya vyombo vya habari. Labda kama hatusomi. Hata kama asingesema, historia yake inajulikana. Naomba kusisitiza mambo matatu.

1. Dk. Slaa hakufukuzwa upadri. Aliomba kuacha kwa hiari, akaruhusiwa. Hiari ilel ile aliyotumia wakati anaingia katika utumishi huo, ndiyo alitumia kuondoka katika upadi huo. Labda aligundua ukomo wa wito wake huo.

2. Kwa sababu hakufukuzwa, na kwa nafasi aliyokuwa nayo (Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu) aliomba akaruhusiwa kurejeshewa hadhi ya ulei (laicization).

3. Kwa sababu hiyo pia, aliomba na kuruhusiwa kuoa. Staili, wakati na mahali pa kutekeleza hayo yote anajipangia mwenyewe.


Kwa hiyo, ni vema tusahihishe hisia zetu kuhusu wito wake. HAKUASI UKATOLIKI WALA UPADRI. Na tusing'ang'anie wito wake aliouacha, badala ya kujadili huu anaoutumikia kwa sasa. Na wananchi wa Karatu ndio mashahidi wa kwanza. Akiwa hivi alivyo, amewatumikia vema kwa miaka 15 mfululizo, na kuibadili Karatu kwa kiwango kikubwa.

Na taifa limefaidi sana uzalendo wa Dk. Slaa. Ujasiri alioonyesha Bungeni haulinganishwi na wa mbunge mwingine awaye yote. Kwa kauli zake, ameokoa raslimali nyingi za taifa, amezisimamia na kuwasaidia wananchi wengi zaidi kuliko wana Karatu. Huyu ndiye mntaka kumbeza? Mnalinganisha na nani mnayemtetea?

Baada ya kuona haya yanayoibuliwa na wanaCCM dhidi yake, ili kujaribu kumvuta shati, mtu mmoja ametania akaniambia hivi: "Tunamhitaji Dk Slaa kwa sababu ya KICHWA chake, si kwa sababu ya viungo vyake vya uzazi."

Chanzo: Wanabidii

3 comments:

Anonymous September 8, 2010 at 4:04 AM  
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous September 8, 2010 at 4:05 AM  

Natamani sana wengi wangeufahamu ukweli huu,,
Mungu mpe silaha ya kushinda ndugu Slaa

haulledict September 8, 2010 at 1:16 PM  

nadhani tunahitaji vyote lakini tukiangalia kwa makini nikuwa hakuna mwenye haki ya kuanza mrushia jiwe Dr. slaa, amewaacha mbali sana kwa akili na utashi. viungo vya uzazi tunavyo sikuzote ila ubongo kama ule ndo hatuna tunauhitaji haswaaa

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP