Pekua/search

Thursday, February 24, 2011

MMILIKI WA DOWANS, WAHARIRI NA KUZUIWA KUPIGA PICHA

Katuni kutoka gazeti la Majira
Ingekuwa vipi waandishi wa habari wa Bongo wangegoma kukubali masharti na dharau ya 'mmiliki' wa DOWANS kutotaka kupigwa picha?: hutaki upigwe picha au kuwa recorded? Fine, kwa heri! they walk out! Hili nadhani hata magazeti ya New Habari House yasingebaki ukumbuni; ingekuwa vipi?
Uhariri mdogo umefanyika ambapo ni picha tu zilizoondolewa, mawazo ya wachangiaji yamebaki kama yalivyo. Soma, shiriki mjidala hii ya kitaifa.
Top of Form
Barrack Mwamakula Brother ni dharau kubwa,nadhani ilitakiwa tufanye hivyo,cjui kwann hatukufanya!
Lusajho Mwambipile Kwanini usitake kupigwa picha na kurekodiwa? sababu aliyoitoa mie sioni kama inaridhisha, kweli wangeondoka ingeweza kujenga heshima. Hiyo ni dharau na fedheha kubwa mno kwa waandishi wetu wa habari
Bernard Elias Dharau tosha, tulishaambiwa mmiliki hajulikani, kajileta na kasema Rost tamu ndo alimsukia dili, akagoma asionwe na wabongo. Huyu jamaa ni wa hapa hapa, tukimwona tutamfahamu tu.
Japhet Mwaipopo I hope ingekuwa poa. Sasa kama hataki kupigwa picha kwnn aliwaita waandish? Hata waandish wa bongo hawana msimamo mi nadhan kulikuwa hakuna hata haja ya kuandika habari yake wangeitia kapuni. Sema ttzo lipo pale ambapo magazeti kadhaa yangegoma basi magazeti ya wale ambao wanamiliki hiyo dowans bila shaka wangeandika kwa uzuri sana. Any way acha hivyo hivyo tutafika tu kama libya kimenuka basi yawezekana kuni ya akiba inakaribia kuwekwa na yenyewe iweze kuivisha chungu. Siku njema.
Linda Madeleka Kwa nini asipigwe picha - au there is a big possibility kuwa the so called "mmiliki" is not the real mmiliki anaogopa akipigwa picha ikatokea kwenye magazeti itajulikana siye mmiliki halisi?? Its strange kwa kweli and it only happens in Tanzania.
Bernard Rwebangira Nashindwa kuelewa kama aliwapora kamera au alisema tu nao wakatii, yaani umetuita kuongea nasi alafu watuwekea masharti?? ingekuwa vipi wote wakaondoka na kumwacha mwenyewe? hii ni dharau kwa kweli.
Kaka Gano Wangegoma vipi wakati wamelipwa kabla ya kuingia mkutanoni??
Bernard Rwebangira Njaaa hizi zinatuuuwa na kuua taaluma pia @Kaka
Gulila Nuru lawama zangu kwa waandishi,lakini kwa kuwa najua maisha ya bongo kibaba haya na taarifa za kiintelijensia nazo zilichelewa achukuliwe picha hata kwa sniper shots? ili angalau tumuone tumfananishe asije akawa mwarabu wa Kariakoo halafu tunaambiwa General huko kwao! ama kweli nchi pekee duniani ambayo unakuja maskini unaondoka tajiri wa kutupwa ni hii nchi ya JK!
Evance Mvamila kuna tofauti gani ya kutokumfahamu mmiliki wa Dowans,na kuletewa kwa masharti ya kutokupigwa picha wala kuwa recorded na kuruhusu waandishi wachache kwa masharti hayo magumu. Suala linabaki vile vile hatumfahamu,hatuwafamu,wameshinda vipi tenda hatufahamu wala rais wangu hamfahamu... wajinga ndio waliwao.. walisema mababu zetu, mungu awarehemu
kwanini amekuja basi, tukisema kila siku waandishi wetu njaa imezidi,wanaona watu wabaya..mwandishi wa habari unaenda sehemu bila nyenzo za kuchukulia habari kwelii!!! huo ndio uandishi wa habari, tukisema walinunuliwa ili wathibitishe kuwa... mmiliki wa Dowans yupo na sio lodilofa wala ro..bert watabisha. waandishi wanaipeleka wapi fani hii
kaka sasa bora tutulie tuepushe msongamano.... haina tofauti na hadithi za paukwa... pakawaSee More
Christina Sifael Mbise Nadhani tunahitaji Tsumani iondoe tabaka hili kije kizazi kianze upya maana every corner ni uozo. Sijui nini kifanyike kusafisha bongo za watanzania. akili finyu sana! unapokea hicho ila ukirudi kwako umeme juu, elilmu ola, afya ola, barabara utalia, etc hivi vijisenti hivyo ndo vimekusaidia nini? watoto wako na wajukuu wako unawaandalia nini??? sh............!......!
Bernard Rwebangira KANYABOYAAAAAAAAA!!! MTAKE MSITAKE,
Adam Gwankaja wallah hii ni hatari. so helpless. extremely hopeless!!! mweeeeeeeeee
Hamis Shimye Adam usihukumu habari corporations pekee bali rejea ni magazeti mangapi yaliyotoa habari ile nakuona upi mwelekeo wao hivo nashwishikia kuamini huo ndio uandishi wa tanzania
Adam Gwankaja ‎@Hamis, nakubaliana na uchambuzi wako juu ya mwelekeo wa uandishi wa Tz. Sikuhumu NHcorp la hasha, nimewapigia mfano kwa vile mgongano wa kimaslahi wa RA ni dhahiri! Tukubaliane kuwa picha haiko clear! Ni chengachenga tu!
Asubisye Mwamfupe Adam, mmiliki alikataa kupigwa picha kwasababu yeye mwenyewe haonekani hata ukikutana naye sasa ungepiga picha nini?
Oswald Bankobeza HII NDO TZ. KUNA SIKU MTU ATAAMBIWA KUPIGA MAGOTI ASALIMIE NDO ARUHUSIWE KULA! Mchakato wooote ni wa kifisadifisadi hata huyo huenda ana lake jambo lakini TAA NNE DISCO kama kawaita si waende tusaidiwe kumjua? MBONA WANAKWEPA?
Rashid Mkwinda Duu!!! mnacheza na mmiliki wa DOWANS nini ana uwezo wa kuwalisha Watz kwa miaka kadhaa ijayo na ana vijisent vya kula hadi dunia iishe,vijipaparazi na vijikamera vyao vya Mchina wapi na wapi,gharama ya kijikamera chake haizidi hata gharama ya Tai au kamba ya kiatu cha Mmiliki wa Dowans nyie mnafanya mchezo na Mihela nini?
Emmanuel Arsenal Imani Ingekuwa poa sana maana wanatuzingua tu na michezo yao!
Bottom of Form

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP