Pekua/search

Friday, February 4, 2011

WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA hata watanzania wachanga 10 wanafukiwa ?


WAPI TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA hata watanzania wachanga 10 wanafukiwa (wakiwa hai au wamekufa) katika shimo moja jirani na Hospitali ya Mwananyamala. Afu mwaunda tume! Wapelelezi wameshindwa jamani? Oh sorry, wako bize kujadili siasa! Too bad! Quo va dis Tanzania? Wanakupeleka wapi mamaland?

Top of Form
Alphonce Assenga Kweli yatia huruma, hizo tume za kuundwa kila mara si jinsi ya kula kwa wanasiasa tu.

Atieno Kashy Albert Mwisho wa mambo yote umekaribia!

Adam Gwankaja Wandugu unaweza kuwa sio ule mwisho, ama mwisho wa mwanzo, bali kwa yakini huu ni mwanzo wa ule mwisho!

Patrick Lusiano Tsere Adam. I need clarification. Waliotupwa ni vitoto vichanga au ni foetuses? Au ambao ni still born. Nisichoelewa shuka ya hospitali iltumiwa na wazazi wako wapi?

Rashid Mkwinda Mmhhh hili jambo lataka wasaa inawezekana ni watoto waliokufa kabla ya kutimiza miezi wakiwa matumboni ktk hospitali kubwa kwa hiyo waliona njia ya kusitiri ni kuwazika katika kaburi moja...hebu tujadili hili na kulichunguza kwa undaani zakidi z it inawezekana unyama wa aina hii kufanywa na binadamu aliyeumbwa Mwenyezi Mungu na kuzaliwa kupitia tumbo la mama? impossible

Kiongozi Patrick, nilichosoma na kuelewa na kwa mujibu wa tag (birth tag kwa maana hiyo) iliyokutwa pale ikimtaja mama mmoja inaonyesha pre mature ambaye kwa kiswahili nandhani mtoto aliyezaliwa njiti! Pia kuna taarifa kuwa saba walikuwa nj...iti na watatu walishafikisha umri wa kuzaliwa kabisa, ndo kusema walizaliwa na sio abortion!picha nilizoziona kwenye uwazi kwa kweli hata kama mimi sio tabibu, watoto wengine walikuwa wakubwa kabisa wajameni! Walikuwa watoto! Hata waandishi habari akiwemo sam mahela wa itv aliyekuwepo eneo la tukio alimbishia mganga wa mwananyamala mbele ya DC Lugimbana kuhusu kuwa watoto hao wote saba walikuwa 'foetuses' !! Wazazi wako wapi, na ni nani aliwafukia (sio kuwazika) ndicho ambacho mimi nadhani kinahitaji CID sio siasa za tume jamani!ikumbukwe hili limetokea siku chache tu baada za ripoti ya mtanzania mwingine huko mwanza kutoonyeshwa maiti au walipozikwa mapacha wake! What a sub culture in medical field hapa kwetu!? Disgusting!See More

Nuswe Mwakiluma ‎...ndivo walivyo viongozi wetu hawawezi kujadili masuala ambayo hayaathiri maslai yao moja kwa moja na ambayo hayana maslai kwao..watajadili tu namna gani tuilipe DOWANS...lini wananchi wanaandamana na polisi waweke risasi ngapi kwenye binduki zao...hicho tu basi lakini si vinginevyo...its too bad

Ileta Taguaba kweli kabisa @adam, Usalama wa Taifa katika nchi yetu ni kitengo cha ajabu sana na imeshajengeka mazoea ikitokea tukio la kusikitisha ndani ya jamii ndo mwanya wa kutoa fedha kwa wajanja ndani ya serikali, si unajua mishahara haitoshi, ..disgusting zaidi ni pale chombo kilichopo badala kilete ufanisi wanaunda kingine kibovu zaidi. .we kaanzishe kipindi kama kile cha jerry muro..kama hayajakukuta.so sad jamani...natamani kupata mwandishi wakuandika ya ndani ya serikali ye2..maovu yote tuyaanike na kusambaza ulimwengu kote..

Hiyo ni kazi ya Police. Shuka ya hospital imekutwa pale ushahidi tosha wametoka Mwananyamala. Hivi hiyo hospitali vipi jamani mbona vituko kila wakati. Kawaida watu wanakabidhiwa vitoto vyao wakazike wenyewe na inaonekana hao ni watoto sio ...vimimba.

Adam Gwankaja ‎@Ileta, umenena vema kabisa. Imagine we have experts wa upelelezi wa makosa ya jinai na africa nzima ni miamba(taarifa za kiintelijensia nilizopata), halafu ati mwaunda tume!@Lucy, kweli kabisa! Hata vingekuwa cvimimba, ndo mtupe jalalani? Kwa sisi wenye imani haba, tukijumuisha matukio haya mawili la bugando na hili, there must be some terrible businesss behind this!

Ileta Taguaba aibu.unaweza ukakuta ndo system nzima ya mahospitali ye2..kwa wale marehemu wasio na ndugu...uenda ndo njia watumiayo mahospitali ya serikalii,,,na serikali inajua hilo..maana mfuko husika uenda hautoshi kufanya mazishi ya heshima.u neva know?

Adam Gwankaja Am telling u @Ileta, it might be a common practice for some benefit! Ndo unajiuliza, wapi taarifa za kiinteligensia? Anyway there is an end to everything, and here come!so many qns to be answered!

Salome Kitomari kwanz aumeona huo muundo wa tume yenyewe?ni sawa na kesi ya mahindi kumpelekea ngedere

Adam Gwankaja Kweli kabisa@salome,aibu! Tumezidi maigizo!

Michael Emanuel Karau intelijensia wanadai "UDINI" umezidi huku maiti 10 zikizikwa shimo moja. ingetokea UK, leo hata bibi yangu pale Umbwe Kibosho angesikia na kuona BBC waziri au kiongozi husika akiachia ngazi

‎@Ileta ..do not talk about usalama wa Taifa u know that guyz they think wao ni everything....Usalama wa Taifa iz u,ambaye ukiona nchi inahujumiwa una react mara moja kuona hakuna hujuma inayoendelea,usalama wa Taifa unaowadhani ndio hao ha...o wapo tunao na madudu ya DOWANS yanatokea na matokeo ya uchaguzi yanachakachuliwa na mengine ni hayo vitoto vinazikwa shimo moja kungekuwa na usalama wa Taifa hayo yasingetokea,yangeibuliwa kabla hata ya kutendeka na watu wangewajibika...

''EWE NCHI TANZANIA ILIYOZALIWA KUTOKANA NA NCHI MBILI AMANI ULIYONAYO NI HAZINA INAYOTOBOLEWA MATUNDU MATUNDU PUNDE ITAVUJA NA KUSHUHUDIA YANAYOTOKEA NCHI ZINGINE,SIMAMA WIMA EWE TANZANIA MWENYEWE BAINISHA NANI ANAFAA KUWA MLINZI WAKO''See More

Kweli@Rashid. Nadhani TISS ni miongoni mwa idara za ku overhaul! Vichwa vyenye fikra za enzi za vita vya ukombozi kusini kusini mwa afrika visipewe majukumu makubwa idarani. Wao wanadhani usalama wa nchi ni kulinda viongozi; kumbe mambo yas...hageukam hivi sasa its about uchumi, umaskini, rushwa nk. Hivi kenya watangaze knjaro na hujuma nyingine maafisa wako wapi?wanafanya nini?kwanini tanzanite iliuzwa kenya zaidi kuliko tz inakochimbwa?karamagi alitiaje saini kihuni hotelini mkataba wa buzwagi na mikataba mingi ya kilaghai, TISS wako wapi?See More

Ileta Taguaba kweli kabisa @rashid, kila mwananchi anawajibika na ulinzi wa nchi yake, wakati jeshi la usalama tuliyempa dhaman ya usalama wa raia umeshindwa kazi, mpaka iundwe tume kulisaidia jeshi la polisi.. sio wanadhani @adam.ndo hali halisi...nimependa manano ya ngo ya sikika..ya kutaka tume hewa ivunjwe na kuletwa nyingine isiyohusika na govt..big up sikika..ila wamesikika kweli?

Adam Gwankaja Aiseee sikika wanasikika!wasiposikizwa na wenye mamlaka, watasikizwa hata na mawe! Sikika pana vichwa naviheshimu sana!

Ileta Taguaba wacha wasikike,,,bt adam hapa hamna kesi...maana unadhani serikali ilivyo bahili kwa raia wake,,ndo itaenda nunulia sanduku mimba zilizoharibika..the same is done @muhimbili,na hospital zote za serikali,hii ya mwananyamala i think ni bahati mbaya kwao hawakuzika vema..mbona hata kwe2 wa2 wazima.2nazikana juu kwa juu..yaani maiti juu ya nyingine..coz makaburi yamejaa...sembuse vichanga..serikali itamke tu ukweli..na si kujikanyagakanyaga

Salome Kitomari tatizo wenye shibe hawawajui wenye njaa,tuna taifa la wafunga mikanda na walegeza mikanda,walegeza mikanda ni bomu linaloandaliwa kulipuka baadaye

Adam Gwankaja Na ikumbukwe pia kuwa mwenye njaa hana miiko! Ni bomu kweli kweli!

Rashid Mkwinda Ni bomu punde litaripuka,punde litaangamiza jamii,punde litaangamiza vizazi,punde litaangamiza rasilimali zetu na kuifanya nchi yetu kuwa kisiwa cha Upweke katika bahari ya Wanyonge wadhulumika na Wadanganyika
Bottom of Form

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP