Pekua/search

Saturday, January 28, 2012

'CHADEMA WAMESABABISHA MGOMO WA MADAKTARI'

"Taarifa za kiintelijensia zimebaini kuwa Chadema ndio wamesababisha
mgomo wa madaktari, mgomo ambao umeendelea kwa siku kadhaa sasa na
umehatarisha maisha ya wagonjwa wengi na umesababisha hata madaktari
kuvuana uwanachama kwenye chama chao cha madaktari. Chadema ndio hao
hao wamekuwa wanaratibu migomo mingi kwenye vyuo vikuu, ndio haohao
wameratibu mgomo wa madereva wa maroli kule mbeya lakini pia ni
Chadema walio hakikisha na naibu waziri wa Afya anagoma kwenda kuonana
na madaktari pale kwenye ule ukumbi walio andaa wao maana protokali na
usalama wake ulikuwa hatarini.

Hawa Chadema hawafai maana wanataka nchi isitawalike, Wanafanya haya
wakijua kuwa raisi JK yuko kwenye mkutano wa uchumi duniani na kule
anakutana na kuongea ikiwa ni pamoja na kupiga picha na Bill Gates na
matajiri wengine wa dunia ili watusaidie kujikwamua kutoka kwenye
mkwamo wa njaa na uchumi mbovu. Chadema ndio hawahawa wamesababisha
sasa hivi shilingi yetu imeshuka thamani maana muda mwingi wanautimia
kuwasumbua watu waliokuwa wanajua matumizi ya shilingi na sasa
wamekasirika na matokeo yake shilingi imeshuka thamani.

Chadema ni watu wabaya sana maana baada ya mgomo huu wa madaktari
wataandaa mgomo mwingine waliouahirisha na walimu mwaka jana,
wanachowaza Chadema ni Migomo tu ili serikali idorore na nchi
isitawalike, Chadema ni chama cha fujo na maandamano, wamewezesha
mgomo mpaka ndani ya ccm na kusababisha wale makada wenye magamba
kugoma kuvua magamba yao! Hiki chama ni kibaya sana ndio maana
kimemtuliza hata yule Aminiel Mahimbo aliepokwa my wife wake na jamaa
anae walaza macho magamba.

Watanzania mtambue kuwa chadema ni chama kibaya sana maana ndio
kimesababisha minong'ong'o eti Dr Mwakyembe amewekewa SUMU! Nani
amuuwe Mwaki?! Mwaki hana tatizo kubwa anaugua tu mafua na hata ripoti
yake ni chadema haohao ndio wameizua maana wanajua kuwa ikiwekwa
hadharani ataleata tena mambo yake yenye harufu ya ki richmond,
chadema watu wabaya sana maana wamesababisha maisha magumu kwa kila
mtanzania, chadema wamesabibisha mpaka umeme unagoma mara kwa mara.
Tusiwaamini watu hawa maana wanataka kuiondoa serikali iliyoko
madarakani kwa maandamano.

Hii ni siri yako! Hata yale mafuriko yaliyosababishwa ndugu zetu
kuhamia kwenye majumba ya nguvu kule ma bwe pande ni jamaa hawahawa
wakiongozwa na makamanda wao. Hawa jamaa ni nuksi."

Mohamed Mtoi kutoka jukwaa la Wanabidii


KUSOMA MJADALA JUU YA MADA HII KWENYE FACEBOOK Bofya HAPA

6 comments:

Anonymous January 28, 2012 at 4:09 AM  

We uliyeandika hii ni nuksi tena kibaraka mkubwa wa CCM...sijui we in shoga wa kisiasa..huna mantinki..taarifa za kujenga chuki..huna lolote masikini mkubwa wewe mvivu wakufikiri...

Adam January 28, 2012 at 4:25 AM  

Duuu ukombozi Tanzania uko mbali kumbe kiasi hiki!!!? Kama aliyeandika ni shoga, ni maskini na mvivu wa kufikiri, wewe utakuwa nani? Umesoma kilichoandikwa? Umejaribu kuelewa? FUNGUKA. ACHA JAZBA, RUDIA KUSOMA. Jielimishe kushambulia hoja sio mtu. Nakusihi usome tena, uelewe, lete hoja zako tujadili. Matusi hayatakomboa nchi.

Anonymous January 28, 2012 at 4:37 AM  

duuuh hiyo coment ya kwanza inaonesha huyo ni mtu anayepelekwa na vichwa vya magazeti tu bila kujua ujumbe ndani yake...ndo tatizo la uzembe wa watu kutokusoma full info...hawezi jua kuwa aliyeandika kwa intelijensia yake ndogo tu inaonesha kabisa yeye ni chademu.

Adam January 28, 2012 at 4:46 AM  

kinachokarahisha ni mtu mzima kuporomosha mitusi migumuuu wakati hata hoja yenyewe hujaielewa!! Tusameheane tu jamani! tuelekezane tuuuuu!!! Jazba haijengi. tutofautiane lkn tusichukiane. ironically, jamaa anathubutu hata kutaja uvivu wa kufikiri. sasa mvivu wa kusoma aya chache tu zile na kuzielewa anawezaje kutokuwa mvivu wa kufikiri!!! mweeeee

mike January 28, 2012 at 4:52 AM  

daaaaah umeona eeh Adam....asanteeee, manake jamaa kapolomoka tu...

Adam January 28, 2012 at 5:11 AM  

Kweli Mike. Safari ni ndefu. Mmoja kwenye fb (waweza kuclick mwisho wa post) naye kakurupuka kaita majina yoooote. namshauri arejee asome na kutafakari kidogo tuuu aaa wapi, mpaka baadayeeee!!! yaani....

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP