Pekua/search

Thursday, March 22, 2012

Lowassa na Bomu lake la ajira kwa vijana; kama kweli anaguswa afanye haya badala ya kuwa domo kaya


Kama kweli Lowassa anamaanisha na kuguswa na hili 'bomu', kwanini badala ya kupayuka tuu mikutanoni afanye machache yafuatayo:


  • Akiwa Mbunge, tena anayedaiwa kuwa na ukwasi wakutosha, basi abuni na kuanzisha kampeni ya ajira jimboni kwake, hususanan kipindi hiki ambapo jamii ya wafugaji inakabiliwa na changamoto ya kutafuta livelihood mbadala, kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.


  • Kwa nafasi yake ua ujumbe wa NEC ya CCM anapaswa kuishawishi NEC nzima, iielekeze serikali kufanya moja, mbili tatuuu kuhakikisha 'bomu lake' linateguliwa. Hajafanya hivyo badala yake anapayuka tu kwenye media.

  • Kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa kamati ya Bunge mambo ya nje, ulinzi na usalama - anayo mengi ya kufanya zaidi ya kutusumbua na upuuzi huu wa 'bomu' kwenye media. Angeweza mathalan akashawishi ofisi zooote za ubalozi kuanzisha vituo vya kufundisha Kiswahili ambapo wahitimu wa kiswahili wataajiriwa; angeweza kushawishi na kuhimiza viongozi wetu waongee Kiswahili pale wageni wajapo nchini jambo ambalo lingewapatia vijana wa kitanzania ajira ya ukarimani na ufasili; angeweza pia kuhimiza uanzishwaji wa kampeni ya kuwaandaa na kuwatafutia watanzania ajira nje ya nchi.

Kama hawezi haya yaliyo katika uwezo wake, asitusumbue. Atulie. Lakini pia mnaompenda mumshauri kwa kamsemo haka, 'he should Respect the today's King, so as he is respected when his turn comes, if at all he will live to see it come'

2 comments:

AMANIO April 17, 2012 at 12:31 AM  

Ni mara yangu ya kwanza kutumia blog hii!! ila niseme kweli imenivutia hasa makala yako Adam lakini ningependa kusema wazi tusipende kuhukumu kwa ushabiki wa MEDIA na kukurupuka kama ulivyofanya wewe.. Lowasa ni mtanzania kama nilivyo mimi au wewe hivyo ana haki ya kutoa maoni yake kwa njia yeyote anayoipenda au anayoiona inafaa.

Angekuwa bado ni waziri mkuu hapo wengi tungesema mana angelikuwa ni mtendaji mwenyewe kwani nani ambaye hajui ya kwamba katika kipindi chake cha miaka miwili alikuwa active na mhimili wa serikali na uwajibikaji ulikuwepo toka kwa mawaziri hata wakuu wa wilaya, Najua utakataa labda kwa ushabiki au kwa chuki ambazo hazina umaana ambazo imekuwa ni kawaida kwa Tanzania hasa viongozi wetu kuchafuana kupitia magazeti au mtandao. yalianza toka kwa akina KAMBONA, BIBI TITI na hata SOKOINE sembuse LOWASA???? chuki, fitina na maslahi ni tatizo katka tanzania ni nchi nyingi za AFRICA, kwani ni dhambi kwa kiongozi kuwa tajiri?? huyo LOWASA KIHISTORIA AMEKUWA WAZIRI WA MAZINGIRA, MIFUGO NA MAJI WIZARA AMBAZO HATA BAJETI ZAKE NI HAFIFU NA KOTE KAONYESHA UTENDAJI MZURI TU UILINGANISHA HATA NA MWENYEKITI WA CHAMA HIVI SASA.. kwani nani hajui kuhusu IPTL tujiulize ilitokea kipindi gani? nani hajui mauza mauza yaliyotokea kipindi akiwa mambo ya nje?? hata kwenye fedha?? CCM ni tatizo kwa ujumla wake toka kimeanza kikiwa TANU mpaka sasa hakuna cha maana walichokifanya na huu ndo mwisho wa wao.. Nani aliemsafi CCMI?? AMA SERIKALINI?? NI AIBU TUPU HASA KWA CCM NA WOT
E WANAODANGANYIKA ETI LOWASA NDO TATIZO CCM NA TANZANIA??? SITA, MEMBE,MWAKYEMBE MALECELA WOTE NI WASAKA MADARAKA HAKUNA KINGINE CHOCHOTE WANACHOKITAKA NA KUKITAFUTA... Sita amekuwa TIC( Tanzania investment center) atueleze alifanya nini wakati serikali ilipokuwa ikiingia mikataba mibovu kupitia nafasi yake pale TIC lakini tusimsahau Membe alikuwa na kitengo kizuri tu ambacho hata angeweza kushauri aliyekua madarakani lakini hakufanya lolote zaidi ya kujitengenezea na kupata sifa lukuki za Siasa maji taka na unafiki.. WATANZANIA TUFIKIRIE MARA MBILI KAMA CCM KAMA CHAMA KUNA YEYOTE ANAWEZA KUTATUA KERO ZETU??? BILA SHAKA HAKUNA KATI YA WOTE BORA YA HUYO LOWASA, SITA ANACHUKIA UFISADI LEO ILA HAKUMBUKI ALIPOKUWA SPIKA ALIVYOMKEJELI Dr. SLAA na Hoja ya EPA??? aliporuhusu adhabu kwa ZITO KABWE eti MEREMETA ni UZUSHI MTUPU.. shahidi ni TIDO MHANDO, Prof. Peter Maina wa kitivyo cha sheria UDSM kwenye mahojiano ya TBC kuhusu kumpa adhabu ZITO.. BY Amanio

Adam April 17, 2012 at 2:39 AM  

Ndugu Amanio,
karibu sana. Nakushukuru kwamba baada ya kumaliza jazba kwenye para ya kwanza, walau ukatulia katika maelezo yako mengine kuhusu utetezi wako kwa Lowassa.

Naamini katika mijadala.Nimefurahia kusoma mchango wako maana japo umejinasibu kutopenda ushabiki, umeendeleza dhana hiyo. mimi nadhani sio dhambi kushabikia, muhimu ni kujitahidi kuwa objective japo kidogo.

kwenye mchango wangu (post mama) nimebainisha maeneo mengi tu muhimu ambayo mhe lowasa anayo nafasi ya kumake that difference kuliko kupiga soga majukwaani. Nadhani sijamshambulia popote na sijampigia debe mtu yeyote.

ukipata nafasi hebu jaribu kueleza mchango wa bwana lowassa hata kwa kupitia hoja nilizoweka hapo juu (post mama) ili tushawishike kuwa amekuwa tofauti na inahalalisha kutoa maoni yake kwa mwendo wa 'uchochezi' afanyavyo.

Ukifanya hivyo itakuwa nafuu zaidi, kuliko nguvu nyingiulizoelekeza katika kuwataja wengine wote na hata kudiriki kusema eti CCM yoooote haifai na haijafanya kitu, jambo nalodhani ni jazba na ushabiki uliyopita kipimo! Kama CCM hakijafanya kazi kabisa tangu TANU, ndiyo kusema hata bwana mkubwa unayemtetea naye ni takataka tu!

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP