Mfumo DUME hauna UUME wala NDEVU
Mfumo DUME
hauna UUME wala NDEVU
Mambo yalikuwa hivi mkutanoni. Mama Sofia Simba kwambali kama anatamani kuinuka vile. Picha toka ukuta wa fb wa gazeti mwananchi. |
Ukiiangalia picha hii na ukifuatilia
kwa karibu zogo lililozuka kwenye mkutano mkuu wa uchaguzi wa Umoja wa Wanawake
wa CCM (UWT) huko Dodoma,unapata picha kwamba MFUMO DUME umetawala maisha yetu
Watanzania na ni hatari zaidi maana kuuondoa hakuishii tu kuongeza idadi kubwa
ya wanawake kwenye nafasi za maamuzi.
Ningetarajia kuuona MFUMO USAWA
ama basi MFUMO JIKE katika uchaguzi ule. Lakini kilichotawala pale ni mfumo
dume uliopindukia ule unaofanywa na wanaume. Kitendo cha kutaka baadhi ya watu
tena wenye dhamani WASIHOJIWE na WASITOE MAELEZO kwa wajumbe, kitendo cha
kutaka wajumbe WANYAMAE Ndiyo hasa MFUMO DUME wenye. Mfumo dume kwa sifa zake
na rangi yake halisi sit u kule kupendelea wanaume katika kufanya maamuz na
katika kupata na kutumia fursa, bali ni mfumo NYAMAZISHI, HODHI usiotaka HOJA
bali AMRI.
Mjumbe kamuuliza mgombea amefanya
nini ama juhudi gani kukiimarisha chama chao? Hilo linaletaje zogo? Badala ya
kujibu hoja na kuwafahamisha wajumbe mgombea anarusha vijembe juu ya uchanga wa
muuliza swali...’mgni huyu...hajui tulichofanya...JAMANI SI NDIO MAANA
ANAULIZA? Kama kawaida yao wapambe wamekuwa mstari wa mbele kutaka kumnyofoa
macho mjumbe aliye hoji..huu ndiyo mfumo dume hasa. Mfumo usiovumilia fikra
tofauti na mawazo mbadala.
Mlioko kwenye harakati dhidi ya
mfumo dume hamna budi kuutambua mfumo huu vizuri..hauna ndevu wala uume..ni
mfumo unaowaumiza wanawake kwa wanaume sawia..hata baadhi ya wanawake
wanautumia mfumo huu kuwaumiza na kuwakandamiza wanawake wengine.
4 comments:
Ni kwel kabisa, Tunataka kuona mfumo unaotoa haki na fursa sawa kwa watu wote, lengo si kuondoa mfumo dume na kuweka mfumo jike, Lengo liwe kuweka mfumo unaotoa usawa kwa watu wote. Ndio maana wanawake hawawezi kucompete kwa sabb wao kwa wao hawapendi kuinuana na kushirikiana na kupaza sauti zao kwa pamoja
Hakika. Mfumo sawia ama mfumo haki ndiyo unaohitajika, ila ndiyo tuko mbali sana. maana makamanda wenyewe ndiyo hao kina nanilii wanavuruga mambo.
Hawataki mawazo tofauti..hawana subira
Swadakta mlionitangulia kutoa maoni.. Mimi napendekeza tulichambue tukio hili, na dhana yote ya jinsia kwa kina zaidi. Tujiulize je dhana hii yote ya Jinsia haukuchangia tu, kama si kuanzisha na ku_instutionalize ubaguzi katika jamii? Je haya yote ya madkatari(wanawake), Chama (wanawake) nk hayatufikisha katika TAnzania (Wanawake), Je Mwl JK Nyerere alipotuasa tuache ubaguzi akifikiria mambo ya hivi pia? Je, divide and rule inafanya kazi hapa? Mengi tujiluize wabongo wenzangu, binaadamu wenzangu!
Saidi, shukrani kwa mchango wako mwanana kwa maana unafikirisha. Nadhani kuwepo ...wanawake, kwa maoni yangu sio msingi wa ubaguzi. ndiyo uhalisia wenyewe, kuna wanaume na wanawake katika taifa hili na wanauhitaji unaotofautiana katika mazingira na nyakati fulani fulani. Na ndiyo maana wimbo wetu wa taifa umekuwa miongoni mwa nyimbo zilizo gender sensite zzaidi duniani...Wake kwa waume na watoto...jamii sio homogenous.
Kamba ubaguzi ni state of mind, ndiyo msingi wa kuandika post hii hata kwa kutumia maneno yasiomazuri sana kama 'uume'. Nafsi ikishachafulika, basi utambagua hata mwanao wa kumzaa. ndicho kinachotokea, kuna wa kundi hili na wa kundi lile, basi wanajisahau kabisa kina mama hawa kuwa wote ni wana wake na ni wa tanzania.
Tuendelee kuchangia
Post a Comment