Nyerere Alipohutubia Bunge Kwa Kiswahili
Nyerere Ahutubia
Bunge Kwa Kiswahili Kwa Mara Ya Kwanza
Leo (Desemba 10) Katika
Historia yetu
Mwaka 1962, mara baada tu ya Tanganyika kuwa Jamhuri, Rais
wa Kwanza wa Tanganyika Mwalimu Julius Nyerere alihutubia Baraza la Taifa
(National Assembly) Kwa kutumia lugha ya KISWAHILI. Awali lugha iliyotumika
kwenye baraza hilo ilikuwa Kiingereza.
Nia na dhamira ya dhati ya kukienzi Kiswahili, si kwa sababu
ya uzalendo tu bali pia kwamba ndiyo lugha inayoeleweka na watanzania wengi,
iliwekwa bayana tangu mwanzo. Leo hii tunasuasua kukifanya Kishwahili kuwa
lugha ya kufundishia licha ya tafiti mbali mbali kuthibitisha kwamba lugha ya
kufundishia inapaswa kueleweka vizuri baina ya mwalimu na mwanafunzi.
Licha ya ushahidi wa kutosha kwamba hata sasa walimu wetu
kutoka sekondari hadi chuo kikuu hawafundishi wakaeleweka pasipo kuchanganya
KISWAHILI katika ufundishaji wa masomo yao, mfano:
“Slaves were obtained through many ways such as...waylaying
yaani kuwavizia...”..Unaona ee mtu unajipitia ghafla unakamtwa sawa?”