Leo ni Si ya Uhuru wa Tanganyika
Leo (Desemba 9) ni Si ya Uhuru wa
Tanganyika
Rejea ya Historia ya nchi yetu inaonyesha kuwa leo
miaka 51 iliyopita ndipo Tanganyika ilipata uhuru wake. Siku kama ya leo hapo
mwaka 1961 Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokea Hati za Uhuru wa
Tanganyika kutoka kwa Prince Phillip, Mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza.
Mwalimu Nyerere ndiye Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika.
Ni siku ya kutafakari. Ni siku ya kupambanua.
Tukifanya hivyo hebu
tuimbe pamoja wimbo huu:
Na huu pia..
TAZAMA
RAMANI
Tazama ramani utaona
nchi nzuri
Yenye mito na mabonde
mengi ya nafaka,
Nasema kwa kinywa
halafu kwa kufikiri,
Nchi hiyo mashuhuri
huitwa Tanzaniaaaaaaaaaa....
Majira yetu haya,
yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi,
Nyerere
ameukomesha X2
Chemchem ya furaha
amani nipe tumaini,
Kila mara niwe kwako
nikiburudika,
Nakupenda sana hata
nikakusitiri,
Nitalalamika kukuacha
Tanzania.
Majira yetu haya,
yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi,
Nyerere
ameukomesha X2
Nchi yenye azimio
lenye tumaini,
Ndiwe peke yako mwanga
wa Watanzania,
Ninakuthamini
hadharani na moyoni,
Unilinde nami
nikulinde hata kufa.
Majira yetu haya,
yangekuwaje sasa
Utumwa wa nchi,
Nyerere
ameukomesha
X2
0 comments:
Post a Comment