Pekua/search

Thursday, April 17, 2008

Mama Salma Kikwete aigwe.(Reaction)

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu Wanazuoni.

Dada Catherine nashukuru kwa mawazo yako ambayo nayeheshimu, ila bado
hujanishawishi. Kwa hiyo RADHI SIOMBI.Pengine tungoje mitazamo ya
wengine. Hata hivyo ingekuwa hoja ni kushurutishana kuombaa radhi,
wallah leo hii ungeshurutishwa wewe kwa kuiona lugha adhimu ya
Kiswahili kuwa dhalili na kuiita 'kilugha'.

Ndugu zangu dhana ya 'vilugha' ni mabano (kwa lugha ya Chambi)
yaliyotengenezwa na wazungu (ambao dada Catherine unajaribu
kuwafagilia) . Lugha ni lugha, Kindengereko ni lugha 'yenye lahaja
zake' Kisukuma ni lugha 'yenye lahaja zake', vivyo hivyo Kiswahili ni
lugha 'yenye lahaja zake' sawa kabisa na Kiingereza ambayo pia ina
lahaja zake.Kwa hiyo ajenda ya 'kilugha' ni dharau tu ya Wazungu
iliyolenga kushusha kujiamini kwa wazalendo. Ikizingatiwa kuwa lugha
ndiyo mlango mkuu wa kuingilia utamaduni wa mtu.Kwa hiyo wazungu
wakauingilia utamaduni wetu, na kwa kweli wakaufanya vibaya na
pengine wanaendelea, wakitutumia sisi kama makuwadi.Je tuendelee
kuingiliwa?

Swali muhimu kuhusu hoja uliyoibua ya 'Lugha ya Kimataifa' ni je
lugha ya Kimataifa huota kama uyoga? Hapana, Historia ya lugha ya
Kiingereza inabainisha kwamba ni juhudi za maksudi (ikiwemo kuziita
lugha za watu wengine vilugha) za wenye lugha hiyo kuieneza, ndizo
zilizoifanya kuwa ya Kimataifa.Ni juhudi kama hizo ninazompongeza
mama Salma kwazo.Lakini nafurahi kwamba dada Catherine umekiri pia
kwa kusema 'wazungu wamekifanya Kiingereza lugha ya Kimataifa'

Pia, dadaangu tafadhali, tafadhali sana, usomi hauwezi kuwa
Kiingereza. Kujua kiingereza usiwe ndio usomi. Haigombi watanzania
kujua Kiingereza. Tatizo hapa ni fahari ambayo watu wanakipa
kiingereza. Huyo Baba wa Taifa hakupigania uhuru ati tu vile alijua
Kiingereza. Hilo pia ni upotoshaji wa Historia, ambayo bahati nzuri,
naifahamu kidogo. Machemba, Mkwawa, Milambo nk, walipambana na
wavamizi bara bara, je hawa walijulia wapi Kiingereza?? . Nyerere
alikuwa mstari wa mbele kuona Kiswahili kinakua, ndiye Nyerere
ninayemfahamu. Alijitahidi kukiweka Kiswahili kwenye ramani ya
dunia.Ni Kiswahili kilichowaunganisha watu ambao leo wanaitwa
Watanzania katika kuukataa ukoloni.

Mwisho, mimi sikatai matumizi ya Kiingereza. Lakini tunakitumia wapi?
Kwa minajili gani? Kwa ulazima upi? Wachina, wajerumani, wajapani, na
nchi kibao za Skandinavia na kwingineko, zinatumia zaidi lugha zao,
zimepungukiwa nini?

Kama Kiswahili si lugha ya Kimataifa, basi ni vema dada Catherine na
wooote wenye mapenzi mema, na tuanze sasa kukifanya kiwe, naam, na
kitakuwa.Kwa kwanzia twaweza kuunga mkono mwelekeo wa Mama Salma.

Ahsante.
Adam, L

--- In wanazuoni@yahoogrou ps.com, "cassianbabygirl"
wrote:
>
> Habari wakeleketwa,
>
> Adam kaka yangu tafadhali acha kupotosha uma nani kakwambia kwamba
> kiswahili ni lugha ya kimataifa?
>
> Hata Mama Salama anapata msaada kwa sababu ni Mke wa rahisi tu na
> bado anachekwa kwa ulimbukeni wake.
>
> Tafadhali note kwamba Hata wazungu wana viruga vyao lkn wamefanya
> Kingeleza kuwa lugha ya mataifa.
>
> Hivi leo hii kama kungekuwa hamna wasome nani angapigania uhuru
> wetu? Lugha ndio imemfanya hata baba wa taifa Marehemu Julius
> Nyerere kutetea Tanzania kwa sababu aliweza kuwasiliana na
> Waingereza.
>
> Kiswahili ni lugha ya Wazaramu , Wandengereko na Wayao Mimi na wewe
> tuna kilugha chetu tunachowasilina tunapokuwa vijijini kwetu.
>
> Hivi ni Kampuni ya nani leo hii itakuwapa kazi kama hujui kingeleza?
>
> Tafadhali naomba uombe radhi kwa kupotosha uma.
>
> Catherine

IChanzo: mjadala wa wanazuoni yahoogroup

0 comments:

SUBSCRIBE- Andika email yako hapa utumiwe habari mpya

Enter your email address:

Delivered by FeedBurner

  © Blogger templates 'Neuronic' by Ourblogtemplates.com 2008 modified by Subi nukta77

Go Back to TOP